Maisha bana yana raha yake na karaha zake,kwenye ujana nako kuna mambo haya pia
Leo nimekutana na mtu ambae alinisababisha nikakumbuka mbali sana,nimekutana na binti mmoja ambae alinipa "wehu sana" miaka hiyo ya 2000
Binti huyu nili "mpenda" sana,wakati huo nilikuwa mwoga kiasi kwa wadada lakini huyu nilijikuta namvagaa na kumweleza shida yangu,wakati huo alikuwa anasoma kidato cha 5,aliniambia atafikiria na atakuja kun ipa jibu
Nilikaa huku kiroho kikinidunda kusubiria jibu,kwa namna nilivyokuwa siwajui wadada kwa kipindi kile nilijidanganya kuwa kweli atakuja kunipa jibu,nilisubiri sana huku nikijipitisha pale kwao na kumsalimia bila kuuliza chochote nikitarajia atakuja kuniambia mwenyewe
Ulipita mwezi mmoja kimya,kuna jamaa yangu akanishauri nimvagae kwenda kumuuliza,kiukweli mimi kwa tabia nina aibu kwenye kufa bnya jambo ambalo litaonekana sio la kistaarabu,nilijifikiria sana kuhusiana na jambo hili na nikajipa wiki na kusema kama hatanijibu basi namvagaa,wakati huu alikuwa akimuagiza mara kwa mara rafiki yake shida ya fedha mara kwa mara na mimi nilikuwa natoa,si nilipenda bana?
Wiki ilikatika bila majibu yoyote yale,niliamua kumuandikia kabarua kwasababu wakati huo sikuwa na simu ya mkononi kwani zilikuwa ndio zinaingia ingia na zilikuwa ghali kweli kweli,baada ya kuandika nilimuagiza rafiki yake ampelekee,kesho yake nilipokutana na huyu rafiki yake baada ya kutoka shule nilimuuliza na aliniambia kuwa alimpa na hakumjibu chochote hata baada ya kusoma
Nilijiuliza na iliona kama hanitaki hivi,sikujisikia vizuri kwakweli nakumbuka kuanzia siku hiyo nilikuwa napata hamu ya kula kwa taabu sana ...lol,ulipita uda huku nikiteseka kwapenzi la huyu dada na ilifikia wakati nikawa silali kabisa kwa kukosa usingizi,maisha yalikuwa magumu sana na siku moja niliamua kumfuata ili nijue hatma yangu
Nilimkuta akipika kwao na nilimuita na hakuja wala hakunijibu chochote,roho iliniuma sana na nakumbuka hadi nililia siku hiyo nilipofika nyumbani,nakumbuka kaka yangu aliniuliza kulikoni na nilimuambia na alinicheka sana,aliniambia kama mwanamke hanitaki si niachane nae? Nilimwambia kuwa nampenda na hakunielewa na aliniambia kuwa nitakuja kufa kwasababu ya mapenzi
Nilikonda kwakweli ....lol,muda uliendelea kupita na hali yangu kiafya na kifikra haikuwa nzuri kwakweli,siku moja niliamua kumvagaa wakati anatoka shule na kumuuliza kulikoni na aliniambia ataniandikia ujumbe na atamtuma yule rafiki yake,kidogo nilifarijika kwasababu alinijibu vizuri
Baada ya kuniambia hivyo nilihisi na njaa maana sikuwa hata nasikia njaa kwa mawazo,nilikwenda kula na nilirudi nyumbani na kusubiri majibu,muda wa saa moja usiku ulifika na niliona yule rafiki yake alkija na kijibahasha,nilijipa matumaini kuwa huenda nimetunukiwa "dhahabu"
Lahaula ....nilichokikuta humo yalikuwa ni majonzi tu,kwa kifupi binti huyu aliniambia kuwa ana mtu na hana kabisa mpango na mimi na nikiendelea kumfuatilia atamuambia huyo jamaa yake ili aninyooshe,kiukweli mimi huwa sipendi mavurugu,nilinyong'onyea na nilihuzunika sana siku hiyo,nakumbuka sikuweza kula vizuri kwa mwezi mmoja na nilipata ugumu sana kwenye shughuli zangu za kila siku kwa mwezi mzima ule
Lakini nashukuru sana kwani kwa tukio hili na mengine nilikuja kujifunza mengi sana kuhusiana na hawa wadada kwani ni viumbe wa kustaajabisha sana kwa asiewajua hasa hawa wavulana na wanaweza hata kujiua kabisa
Binti huyu kwassasa ni kke wa mtu na nilipokutana nae leo alinichekesha baada ya kunikumbusha yale ya kipindi kile na nilimuuliza sababu ya kunipa kile kibuti na aliniambia kuwa mimi mwenyewe ndio nilisababisha kwa kuonesha nampenda kupita kiasi
Mnaweza kuona kuwa kuna cha kujifun za hapo kuhusu hawa wadada ....
Wewe una kipi unakumbuka kuhusu kibuti cha nyakati hizo ambacho kilikupelekesha na ambacho ulijifunza?