Maumivu na raha ya kukataliwa

Maumivu na raha ya kukataliwa

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,919
Maisha bana yana raha yake na karaha zake, kwenye ujana nako kuna mambo haya pia.

Leo nimekutana na mtu ambae alinisababisha nikakumbuka mbali sana,nimekutana na binti mmoja ambae alinipa "wehu sana" miaka hiyo ya 2000.

Binti huyu nilimpenda" sana, wakati huo nilikuwa mwoga kiasi kwa wadada lakini huyu nilijikuta namvagaa na kumweleza shida yangu, wakati huo alikuwa anasoma kidato cha 5, aliniambia atafikiria na atakuja kunipa jibu.

Nilikaa huku kiroho kikinidunda kusubiria jibu, kwa namna nilivyokuwa siwajui wadada kwa kipindi kile nilijidanganya kuwa kweli atakuja kunipa jibu, nilisubiri sana huku nikijipitisha pale kwao na kumsalimia bila kuuliza chochote nikitarajia atakuja kuniambia mwenyewe.

Ulipita mwezi mmoja kimya, kuna jamaa yangu akanishauri nimvagae kwenda kumuuliza, kiukweli mimi kwa tabia nina aibu kwenye kufa hamna jambo ambalo litaonekana sio la kistaarabu, nilijifikiria sana kuhusiana na jambo hili na nikajipa wiki na kusema kama hatanijibu basi namvagaa, wakati huu alikuwa akimuagiza mara kwa mara rafiki yake shida ya fedha mara kwa mara na mimi nilikuwa natoa, si nilipenda bana?

Wiki ilikatika bila majibu yoyote yale, niliamua kumuandikia kabarua kwasababu wakati huo sikuwa na simu ya mkononi kwani zilikuwa ndio zinaingia ingia na zilikuwa ghali kweli kweli, baada ya kuandika nilimuagiza rafiki yake ampelekee, kesho yake nilipokutana na huyu rafiki yake baada ya kutoka shule nilimuuliza na aliniambia kuwa alimpa na hakumjibu chochote hata baada ya kusoma.

Nilijiuliza na niliona kama hanitaki hivi, sikujisikia vizuri kwa kweli nakumbuka kuanzia siku hiyo nilikuwa napata hamu ya kula kwa taabu sana, ulipita muda huku nikiteseka kwa penzi la huyu dada na ilifikia wakati nikawa silali kabisa kwa kukosa usingizi, maisha yalikuwa magumu sana na siku moja niliamua kumfuata ili nijue hatma yangu.

Nilimkuta akipika kwao na nilimuita na hakuja wala hakunijibu chochote, roho iliniuma sana na nakumbuka hadi nililia siku hiyo nilipofika nyumbani, nakumbuka kaka yangu aliniuliza kulikoni na nilimuambia na alinicheka sana, aliniambia kama mwanamke hanitaki si niachane nae? Nilimwambia kuwa nampenda na hakunielewa na aliniambia kuwa nitakuja kufa kwa sababu ya mapenzi.

Nilikonda kwa kweli, muda uliendelea kupita na hali yangu kiafya na kifikra haikuwa nzuri kwa kweli, siku moja niliamua kumvaa wakati anatoka shule na kumuuliza kulikoni na aliniambia ataniandikia ujumbe na atamtuma yule rafiki yake,kidogo nilifarijika kwasababu alinijibu vizuri.

Baada ya kuniambia hivyo nilihisi na njaa maana sikuwa hata nasikia njaa kwa mawazo, nilikwenda kula na nilirudi nyumbani na kusubiri majibu, muda wa saa moja usiku ulifika na niliona yule rafiki yake akija na kijibahasha, nilijipa matumaini kuwa huenda nimetunukiwa "dhahabu".

Nilichokikuta humo yalikuwa ni majonzi tu, kwa kifupi binti huyu aliniambia kuwa ana mtu na hana kabisa mpango na mimi na nikiendelea kumfuatilia atamuambia huyo jamaa yake ili aninyooshe, kiukweli mimi huwa sipendi mavurugu, nilinyong'onyea na nilihuzunika sana siku hiyo, nakumbuka sikuweza kula vizuri kwa mwezi mmoja na nilipata ugumu sana kwenye shughuli zangu za kila siku kwa mwezi mzima ule.

Lakini nashukuru sana kwani kwa tukio hili na mengine nilikuja kujifunza mengi sana kuhusiana na hawa wadada kwani ni viumbe wa kustaajabisha sana kwa asiewajua hasa hawa wavulana na wanaweza hata kujiua kabisa.

Binti huyu kwa sasa ni mke wa mtu na nilipokutana nae leo alinichekesha baada ya kunikumbusha yale ya kipindi kile na nilimuuliza sababu ya kunipa kile kibuti na aliniambia kuwa mimi mwenyewe ndio nilisababisha kwa kuonesha nampenda kupita kiasi.

Mnaweza kuona kuwa kuna cha kujifunza za hapo kuhusu hawa wadada.

Wewe una kipi unakumbuka kuhusu kibuti cha nyakati hizo ambacho kilikupelekesha na ambacho ulijifunza?
 
Yeah!!
Hii sifa nadhani wanayo wanawake wengi, kama sio wote, hawapendi mwanaume anayeonekana anawapenda sana, wanachukulia ni udhaifu..
Ukimpenda sana, you will not command her, they like someone firm, who will direct them what to do, command them, and if neccessary beat them.

My current girlfriend is angry with me because I have never beat her, she is saying it plainly, she want me sometimes to give her some beating!!
 
Hii ni kweli kabisa mkuu na kuna wengine wanadhani huwapendi kama hutakuwa harsh wakati mwingine

Najua wanaweza kuja hapa na kuanza kubisha lakini huu ni ukweli na kubisha kwao ni moja kati ya tabia yao ya kutokukubali

CC: Ennie , snowhite ....!!
 
Last edited by a moderator:
Kuna mmoja nilimpeenda, baadaye nikaona ujinga nikampiga kibuti lakini hakuamini. Na ilichukua muda sana kuamini.

Yaani siku hizi hata akiwa bafuni na nikampigia simu aje,anaweza kuja kwangu kwa spidi na kusahau hata kuvaa chupi!!
 
Kweli nimejifunza hawa viumbe hawahitaji uwapende saana.

Hii dhana ya kwamba ukimuonyesha mwanamke kwamba unampenda sana atakusumbua mmeipata wapi..?
Pili: Kwani mapenzi yanapimwa kwenye mizani na kusema kwamba wataka kumpenda robo tu au nusu tu..?
Ninachojua mie once umependa huwezi kujiwekea limit kwamba nipende mwisho hapa bila ya wewe mwenyewe kujiumiza.. Maana kupenda siyo tendo la hiari mpanga upange.. Hii dhana inajengwa na mfumo dume ambao unatafuta justification za kuuendeleza mfumo huu hata katika mapenzi.. Jiachieni kwenye mahaba bila ya kuogopa kauli hizi za ati atakusumbua mwanamke ukimuonyesha anakupenda..
 
My current girlfriend is angry with me because I have never beat her, she is saying it plainly, she want me sometimes to give her some beating!!

Hmm....are you for real? She must be a glutton for punishment unless you're talking about another kind of beating...

Yeah..that kinda beating where you beat "it" up like nobody's business.
 
Nakumbuka kama bado siku mbili kufanya necta nikamtongoza dada fulani aiseee akanichomolea halafu alikuwa ndio mwanamke wa kwanza kumtongoza kwa kweli nilikaa mwaka mzima bila kutongoza
kila nikifikiria inaniuma alikuwa mzuri kweli.

Kuna huyu mwengine tulikuwa tupo mahali tunasoma ni mzuri kweli baba yake alikuwa professor udsm kipindi hiko simu zinzingia room ya computer nikafika hadi alipokaa nikachukua simu yake nikaipiga namba yangu kisha nikarudi pa kukaa Nakumbuka usiku wake alinitumia good night aiseee sikulala siku hiyo nilikuwa namuogopa mpaka basi baada ya masomo nilimkuta anadrive mkoko mimi nimeshika bomba kwenye daladala akanipa hi nilitamani nijifiche kwa kweli

Kuna huyu alikuwa jirani yetu kipindi hicho hapa Dar kuna vipori tulikuwa tunafuga mbuzi kulikuwa kuna msichana fulani hivi anasoma olympio kipindi hicho ni ya kishua basi kila nikionana naye namhadithia kwamba kwetu kuna mbuzi mpaka akapata akili sasa hivi ana mtoto huyu ndio namjutia kwa kweli najiona mjinga kila nikikutana naye

Hao ndio niliwakosa kwa kweli
 
Yeah!!
Hii sifa nadhani wanayo wanawake wengi, kama sio wote, hawapendi mwanaume anayeonekana anawapenda sana, wanachukulia ni udhaifu..
Ukimpenda sana, you will not command her, they like someone firm, who will direct them what to do, command them, and if neccessary beat them.

My current girlfriend is angry with me because I have never beat her, she is saying it plainly, she want me sometimes to give her some beating!!

weweee mi nataka nwenye upendo hadi basi
 
Kuna mmoja nilimpeenda, baadaye nikaona ujinga nikampiga kibuti lakini hakuamini. Na ilichukua muda sana kuamini.

Yaani siku hizi hata akiwa bafuni na nikampigia simu aje,anaweza kuja kwangu kwa spidi na kusahau hata kuvaa chupi!!
Ndio wanavyokuwa hawa mkuu ....!!
 
Hmm....are you for real? She must be a glutton for punishment unless you're talking about another kind of beating...

Yeah..that kinda beating where you beat "it" up like nobody's business.
Hahahaaaa .......!!
 
Leo humu.......mbona tutajibeba.........
 
Hii dhana ya kwamba ukimuonyesha mwanamke kwamba unampenda sana atakusumbua mmeipata wapi..?
Pili: Kwani mapenzi yanapimwa kwenye mizani na kusema kwamba wataka kumpenda robo tu au nusu tu..?
Ninachojua mie once umependa huwezi kujiwekea limit kwamba nipende mwisho hapa bila ya wewe mwenyewe kujiumiza.. Maana kupenda siyo tendo la hiari mpanga upange.. Hii dhana inajengwa na mfumo dume ambao unatafuta justification za kuuendeleza mfumo huu hata katika mapenzi.. Jiachieni kwenye mahaba bila ya kuogopa kauli hizi za ati atakusumbua mwanamke ukimuonyesha anakupenda..
Una umri gani?
 
Back
Top Bottom