Natafuta rafiki wa kweli — kwenye shida na raha

1995_No_Ku_Fake

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
1,427
Reaction score
3,075
Habari wanaJF,

Leo nimeamua kuandika uzi huu kwa sababu nimegundua jambo moja kwenye maisha: kuwa na watu wengi sio sawa na kuwa na rafiki wa kweli.

Unaweza kuwa na contacts nyingi kwenye simu, watu wengi unaowafahamu na hata watu unaocheka nao kila siku, lakini inapofika kwenye wakati mgumu ndipo unagundua ni nani kweli anakujali na ni nani alikuwa anakufahamu kwa sababu tu ya mazingira.

Mimi kwa sasa natafuta rafiki wa kweli. Sio lazima awe mtu mwenye pesa nyingi, cheo kikubwa au maisha ya kifahari. Ninachotafuta ni mtu mwenye moyo wa utu, heshima, uaminifu na anayejua maana ya kushikamana.

Nataka urafiki ambao sio wa kuonekana kwenye raha tu. Leo tukacheke pamoja, tukipeana mawazo na kufurahia maisha; lakini kesho mmoja wetu akipitia changamoto, mwingine awepo hata kama ni kwa kumpa ushauri, moyo au msaada unaowezekana.

Maisha yana kupanda na kushuka. Kuna siku utakuwa vizuri na kuna siku utahitaji mtu wa kukusikiliza tu bila kukuhukumu. Kuna wakati utahitaji ushauri, connection, mawazo mapya au mtu wa kukuambia “usikate tamaa, mambo yatakuwa sawa.”

Na mimi niko tayari kuwa mtu wa aina hiyo pia. Sitafuti mtu wa kunisaidia mimi pekee. Natafuta urafiki wa kusaidiana pande zote mbili.

Siamini kwamba urafiki wa kweli unatakiwa kuanza kwa kujua mtu ana pesa kiasi gani. Unaweza kuanza kwa salamu, story ndogo, kushirikishana mawazo na kadri muda unavyokwenda, trust inajengwa.

Kama wewe ni mtu ambaye unaamini rafiki wa kweli anatakiwa kuwepo kwenye shida na raha, basi karibu. Huenda tukawa wageni leo, lakini baada ya muda tukawa watu muhimu sana kwenye maisha ya kila mmoja.

Sijui huu uzi utamfikia nani, lakini kama umeusoma mpaka hapa na umejisikia kwamba na wewe unatafuta mtu wa aina hii, usipite kimya.

Tuanzie hapa. Andika comment au nitumie PM.

Urafiki wa kweli hauanzi kwa kujua utafaidika nini; unaanza kwa kujua unaweza kuwa msaada gani kwa mwenzako. ❤️🤝

#RafikiWaKweli #ShidaNaRaha #Urafiki
 
Urafiki hautafutwi mtandaoni au kuandikiana barua

Urafiki hutokea automatically mzee wewe ingia hapa upate ma comrade ☺️😊
 
Sana tu mkuu. Dogo anatufungulia nyuzi sisi wanaume wenye nguvu nyingi za kiume pale tusipoonekana jukwaani kwa muda.
😂😂 Kabisa mkuu, jamaa anajua namna ya kutukumbusha uwepo wetu jukwaani. Huyu ni mtaalamu wa kutufufua! 😄 Au kutifuliwa
 
Back
Top Bottom