Mauaji ya visasi

Mauaji ya visasi

Mauaji ya visasi (kulipa kisasi) ni dhambi ya tatu kuzaliwa duniani
Dhambi ya kwanza ngono na usaliti pale Eden, lakini hii ina mazonge mengi kwakuwa uongo na kutotii maagizo vyote vinaingia hapo! Ni dhambi yenye vipengele A, B C na D

Dhambi ya tatu ni mauaji, ambayo asili yake ni choyo na wivu, pale Kaini alipofanya uchoyo wa kutoa sadaka iliyonona na matokeo yake ikakataliwa.. Ya mdogo wake Abel ilipokelewa na ndipo roho ya chuki ilipomuingia Kaini na kuamua kumuua mdogo wake kwa mama. Adam hakuwa babayake wa damu.

Tangu hapo mkeka wa mauaji ya visasi uliasisiwa ulimwenguni.. Tangia hapo maelfu kwa maelfu wameuawa kwa mauaji ya visasi. Nimekisoma kisa cha kijana wa Songwe aliyeuwawa mbele ya mkewe na mwanae na wauaji wakaondoka bila kuchukua chochote! Visa hivi ni vingi mno na nitasimulia baadhi kadiri ya kumbukumbu zangu, nakukaribisha nawe uungane nami kama kuna chako unakikumbuka!

Maisha haya hutukutanisha na wengi lakini pia na mengi, kuna watu kwa sababu zozote zile wanajiona ya kwamba wao ndio wao na wengine si kitu.

Wao ndio wanastahili kupata
Wao ndio wanastahili maisha mazuri
Wao ndio wanaijua pesa kuliko wengine
Wao ndio wanastahili maisha na vitu vizuri kuliko wengine

Visa hivi vya mauaji ya visasi vina asili moja! Wauaji hawachukui chochote! Visa hivi vyanzo vyake ni
Usaliti wa kibiashara/dili
Usaliti kwenye mapenzi/mahusiano
Harakati za kisiasa na madaraka
Wivu wa maendeleo/kupata kwa wengine
Dhuluma
Utemi
Ubabe nk nk
Kwenye hili kuna wauaji wa kukodi ama baadhi hutekeleza mauaji wenyewe tena kwa taarifa kabla ya kutekeleza mauaji.

Sometimes kwenye haya mambo ukishindwa kusamehe lipa kisasi! Haikuongezei kitu lakini inakupunguzia maumivu! Ila usiijaribu hii njia imejaa mabaya!

Mnamkumbuka yule traffic aliyeuliwa kwa risasi pale sayansi ? Jamaa alikuja na boda akamuuliza Afande unanikumbuka? Jamaa akajibu ndio.

Jibu hilo lilitosha kummininia risasi zilizoondoka na uhai wake
Nitakuja na visa vingine.
Nilichojifunza kwenye maisha haya ni kwamba ukizisoma amri kumi za Mungu na ukazielewa utakuwa salama duniani na huko utakapoenda baada ya kufa. Barikiwa sana brother mshana.
 
Kibiblia "Nyoka'' amekua hivi alivyo baada ya laana. Ila kuna maeneo mengi tu kizazi cha "Nyoka" kinatajwa soma Mwanzo 6, 13, na Injili ya Yuda sura nzima utaona kizazi chake kilipoanzia.

"Nyoka" biblically ana uwezo wa shape shifting kuwa sio tu binadamu ila hata malaika: 2 Wakorintho 11:14.
Inakuwaje sasa kiumbe kilichoumbwa kwa moto (Lucifer/Malaika) kuwa na na hisia za kibaiolojia hadi atamani kiumbe kilichoumbwa kwa udongo (Binadamu)?

Inamaana Malaika kabla ya kuasi nao walikuwa wana Humans biological hormones kuratibu gametiume/gametiuke hadi wawe na ashki/nyege za kugegedana na Binadamu?

Mbona kama kamba hii
 
Kisa cha saba
Mauaji ya mchina hivi karibuni
Wote mnakikumbuka hiki kisa.. Ni wivu wa mapenzi, aliyeachwa aliwekeza pesa nyingi sana kwa mwanamke! Aliyeuwawa ni mtu tu aliyekuwa kamhifadhi mrembo baada ya kuachana na jamaa yake
Muuaji gari yake ilikutwa Iringa kaitelekeza kando ya barabara.. Alidhamiria kuwaua wote wawili lakini mwanamke akasalimika kimiujiza.. Kuna zawadi ya milion 700 kwa atakayefanikisha kumpata muuaji
Chifu jazia nyama tafadhali maana si kila kinachoendelea duniani sote tuwe tunakijua sababu wakati mwingine tunakuwa tuko bize ktk ujenzi wa Taifa
 
umenikumbusha kisa kilichotokea kanda ya ziwa jamaa alieua familia nzima mpk kichanga....inasikitisha na kuogopesha
Weka hapa hicho kisa Unforgettable, kama Kingsmann kashindwa kukutunza mkulingwa nipo nitakulea kimatunzo tu ila ki-baiolojia ni big NO(utani)
 
Inakuwaje sasa kiumbe kilichoumbwa kwa moto (Lucifer/Malaika) kuwa na na hisia za kibaiolojia hadi atamani kiumbe kilichoumbwa kwa udongo (Binadamu)?

Inamaana Malaika kabla ya kuasi nao walikuwa wana Humans biological hormones kuratibu gametiume/gametiuke hadi wawe na ashki/nyege za kugegedana na Binadamu?

Mbona kama kamba hii
Mkuu reference ni bible kwa hiyo ukisema ni chai meaning Bible ndio chai sio Mimi nayeleta story kutokea humo.

Bible ipo clear kwamba "Wana wa Mungu" walizaa na hao binadamu na reference ni Mwanzo 6 na hiyo Yuda 1. Ukitaka kuona hili hata uzao wao haukufutika kwa gharika rejea Mwanzo 13 utaona wapo hao watoto wa cross breeding hii.

Kuhusu malaika kuwa na hisia, ndio hoja ya shape shifting inapoingia hao walioasi ni wale walikua "watchers" yaani walipewa jukumu la kuwafunza wanadamu mambo mengi kama kuwinda, kusoma nyota, medicine, engineering n.k sasa mfano wakati wanamtembelea Abraham malaika waliweza hadi kula chakula, walisikia njaa, na hata yule aliyepigana na Yakobo "alichoka" baada ya mpambano wa usiku kucha.

Nachojaribu kusema in reference kwa biblia Ina maana malaika wote waliofanya interaction na binadamu walivaa miili ya kibinadamu hivyo kuchukua character zetu kama vile njaa, kuchoka, na tamaa kama iliyowakuta hao malaika wanaotajwa kwenye Injili ya Yuda.
 
hajui kuwa hata malaika waliwahi shuka duniani na kutembea na wanadamu na kuzaa nao watoto!
 
Kisa cha nane
Huyu hakuuliwa bali alitiwa kilema cha chongo kwenye biashara ya mirungi

Ni kisa cha miaka ya 80 mwishoni huko Tanga milimani
Jamaa waliandaa mzigo wa kama roba kumi hivi za mirungi, wateja wakiwa wako Mombasa Kenya.. Mmojawao aliyekuwa na kazi ya kupelekea wateja mzigo akaingiwa na tamaa baada ya kuuza mzigo wote Tanga mjini na kutimkia Dar mazima

Baada ya mwaka mmoja kupita akakutana na wale jamaa zake aliowapiga mzigo mitaa ya manzese(kumbe walikuwa wanamfuatilia)

Walimkuta jamaa bar moja ya uswazi Manzese midizini, jamaa akashikwa na taharuki na kujaribu kujitetea kwamba alikamatwa na mzigo ukataifishwa naye akafungwa miezi 9 jela

Jamaa zake wakajifanya kusikitika sana na kumpa pole nyingi na bia zikaendelea kunyweka huku wakichoma mishkaki kwenye jiko la mkaa karibu yao
Miaka ile mishkaki ilichomekewa kwenye spoke za baiskeli zilizochongwa vema
Basi walimzuga jamaa mpaka woga ukamuisha na ku relux kabisa. Kumbe kati ya zile spoke kuna moja iliwekwa kwenye mkaa na ikakolea moto mpaka ikawa nyekundu kabisa

Kwa ghafla sana wale jamaa watatu walisimama na kumkamata jamaa
Mmoja akambana kichwa
Mwingine akambana miguu na mikono
Ma wat mwisho akaichukua ile spoke iliyokolea moto akamfunua jicho na kumchoma nayo
Baada ya pale walimwachia huku akipiga kelele nyingi za maumivu na jamaa wakatimka wakapotea!
 
Kisa cha tisa
Mauaji ya Ilala! Chanzo dhuluma
Jamaa waliuziana gari, mnunuzi akalipa pesa ya kianzio lakini akashindwa kumaliza
Mwenye gari kila akikumbushia pesa yake jamaa anampiga kalenda
Siku ya siku mdaiwa akamuita mdai wake afike nyumbani kwake Ilala ampatie pesa yake

Jamaa akafika home kwa anayemdai, akakaribishwa vema lakini kufika ndani kumbe mwenzake alikuwa na lake moyoni! Akamuua na kumzika karibu na mashimo ya vyoo kisha akasakafia vema kabisa
Mauaji yalikuja kujulikana miaka takriban mitatu baadae
 
Yule jamaa wa kipemba. Mshkaji alimwonea sana, gari analo, fedha hajalipa na bado akamuua muuzaji
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
Sasa mbona mkuu umesema Abel hakuwa mtoto wa ndoa? Na huko unasema Kaini alikuwa mtoto wa ibilisi?
 
Ndio huyo huyo aisee sijui kesi yake imefikia wapi
Nimeona mitandaoni kuwa ndio inasikilizwa sasa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo tarehe 15.09.2022 shahidi wa kwanza upande wa Mashtaka alianza kutoa ushahidi wake na kesi ikaahirishwa mpaka kesho yake tarehe 16.09.2022, nafikiri itakuwa inaendelea kusikilizwa au kusubiriwa uamuzi kama mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
 
Asante mkuu jamaa bado yuko mahabusu tangu 2014
 
Nimeona mitandaoni kuwa ndio inasikilizwa sasa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo tarehe 15.09.2022 shahidi wa kwanza upande wa Mashtaka alianza kutoa ushahidi wake na kesi ikaahirishwa mpaka kesho yake tarehe 16.09.2022, nafikiri itakuwa inaendelea kusikilizwa au kusubiriwa uamuzi kama mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya mauaji inayomkabili Hemed Ali, ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa huyo alivyoishi ndani ya nyumba yake na baadaye kupokea taarifa kuwa kuna mtu alifukiwa katika nyumba hiyo na mshtakiwa.

Shahidi huyo, Hamjat Nassoro ambaye ni mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi mshtakiwa maeneo ya Ilala Sharif Shamba mkoani Dar es Salaam, alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Grace Lwila, Hamjat alidai kuwa Hemedi alianza kuishi katika nyumba hiyo Julai 23, 2013 kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao uliisha Julai 23, 2014.

“Awamu ya kwanza tulikuwa na mkataba, awamu ya pili alinilipa kodi bila mkataba lakini hakumaliza muda alikaa miezi mitano akasema anahama amenunua nyumba Magomeni,” alisema shahidi huyo.

Aliendelea kudai akiwa ndani ya nyumba hiyo mshtakiwa alitoa malalamiko kuwa kuna tatizo la shimo la maji taka kujaa mara kwa mara, hivyo aliomba amruhusu aende kwa mjumbe akaombe kuchimba shimo nje ya nyumba ili atapishe maji taka naye akamruhusu.

Alidai hata hivyo mjumbe hakutoa ruhusa hiyo na Ali alirudi kwa Hamjat akimwomba amruhusu achimbe shimo kwa ndani ya uzio wa nyumba.

“Aliponiomba nikamruhusu lakini nilimwambia achimbe kama ana hakika atafukia vizuri kama palivyokuwa, alichimba katika eneo la dirisha la mbele, baada ya hapo sikufuatilia tena kilichoendelea kwa sababu mimi nikishampangisha mtu huwa sitaki kumbughudhi,” alidai.

Alidai baada ya miezi mitano ya awamu ya pili akiwa safarini mshtakiwa alihama bila kumwambia na aliporejea ndipo alipompa taarifa kwamba amehama na akamtuma mtu apeleke ufunguo kwake.

Akielezea tukio la kuzikwa mwili kwenye nyumba hiyo, Hamjat alidai Februari 9, 2015 alipokea simu kutoka kwa polisi wakimtaka aende katika nyumba yake kuna tukio mshtakiwa alilifanya naye akaenda.

“Nilipofika niliwakuta polisi na watu wa afya kutoka Hospitali ya Amana, waliniambia kuna mwili umezikwa na wanataka kufukua niliwaruhusu. Niliondoka eneo hilo kwa kuwa sikuwa najisikia vizuri kushuhudia tukio hilo hivyo sikushuhudia mwili ukitolewa mahali hapo,” alisema.

Kabla ya ushahidi kuanza mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake ambapo ilidaiwa Juni 12, 2014 alimuua ,Farahani Abdulsalum, mashtaka ambayo aliyakana mbele ya Hakimu Minde. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo.
 
Back
Top Bottom