Mauaji ya visasi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,659
698,430
Mauaji ya visasi (kulipa kisasi) ni dhambi ya tatu kuzaliwa duniani
Dhambi ya kwanza ngono na usaliti pale Eden, lakini hii ina mazonge mengi kwakuwa uongo na kutotii maagizo vyote vinaingia hapo! Ni dhambi yenye vipengele A, B C na D

Dhambi ya tatu ni mauaji, ambayo asili yake ni choyo na wivu, pale Kaini alipofanya uchoyo wa kutoa sadaka iliyonona na matokeo yake ikakataliwa.. Ya mdogo wake Abel ilipokelewa na ndipo roho ya chuki ilipomuingia Kaini na kuamua kumuua mdogo wake kwa mama. Adam hakuwa babayake wa damu.

Tangu hapo mkeka wa mauaji ya visasi uliasisiwa ulimwenguni.. Tangia hapo maelfu kwa maelfu wameuawa kwa mauaji ya visasi. Nimekisoma kisa cha kijana wa Songwe aliyeuwawa mbele ya mkewe na mwanae na wauaji wakaondoka bila kuchukua chochote! Visa hivi ni vingi mno na nitasimulia baadhi kadiri ya kumbukumbu zangu, nakukaribisha nawe uungane nami kama kuna chako unakikumbuka!

Maisha haya hutukutanisha na wengi lakini pia na mengi, kuna watu kwa sababu zozote zile wanajiona ya kwamba wao ndio wao na wengine si kitu.

Wao ndio wanastahili kupata
Wao ndio wanastahili maisha mazuri
Wao ndio wanaijua pesa kuliko wengine
Wao ndio wanastahili maisha na vitu vizuri kuliko wengine

Visa hivi vya mauaji ya visasi vina asili moja! Wauaji hawachukui chochote! Visa hivi vyanzo vyake ni
Usaliti wa kibiashara/dili
Usaliti kwenye mapenzi/mahusiano
Harakati za kisiasa na madaraka
Wivu wa maendeleo/kupata kwa wengine
Dhuluma
Utemi
Ubabe nk nk
Kwenye hili kuna wauaji wa kukodi ama baadhi hutekeleza mauaji wenyewe tena kwa taarifa kabla ya kutekeleza mauaji.

Sometimes kwenye haya mambo ukishindwa kusamehe lipa kisasi! Haikuongezei kitu lakini inakupunguzia maumivu! Ila usiijaribu hii njia imejaa mabaya!

Mnamkumbuka yule traffic aliyeuliwa kwa risasi pale sayansi? Jamaa alikuja na boda akamuuliza Afande unanikumbuka? Jamaa akajibu ndio.

Jibu hilo lilitosha kummininia risasi zilizoondoka na uhai wake
Nitakuja na visa vingine.
 
Kaini kumuua mdogo wake, kisa kikuu siyo sadaka but ni mwanamke aliyepaswa kuolewa na mdogo wake

Kaini siyo mtoto wa Adam ?

Visa vya mauaji ni vingi na miaka hii vimezidi

Just go ...
Mtani soma hii

Siku moja Kaini na Abeli walimtolea Yehova dhabihu. Je, unajua dhabihu ni nini? Ni zawadi ya pekee. Yehova alifurahishwa na dhabihu ya Abeli, lakini alichukizwa na dhabihu ya Kaini. Jambo hilo lilimkasirisha sana Kaini. Yehova alimwonya Kaini kwamba hasira ingeweza kusababisha afanye jambo baya. Hata hivyo, Kaini hakusikiliza.

Badala yake Kaini alimwambia Abeli hivi: ‘Twende shambani.’ Walipokuwa peke yao shambani, Kaini alimshambulia ndugu yake na kumuua. Yehova alifanya nini? Yehova alimwadhibu Kaini kwa kumfukuza aende mbali na familia yao. Kaini hakuruhusiwa kurudi tena nyumbani.
 
Kumbe masingle mama waliolewa kitambo tuu afu hapa kila siku tunakatazana !!!!hapana sijapenda imetajwa hapo Abeli hakuwa mtoto wa ndoa
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
 
20220718_134038.jpg
 
Kisa cha pili
Mauaji Mbezi Siku ya uzinduzi wa nyumba

Jamaa mmoia mwenyeji wa Moshi kwa akina Mamndenyi mtani wangu na Asprin babu kijana.. Huyu mwana alipiga dili ndefu na wenzake ila kwenye mgao akawazima wenzake akasepa na mzigo wote akapotea mazima..

Akaibukia Mbezi akanunua kiwanja akajenga nyumba nzuri kubwa ya kisasa kwa ile pesa ya dili aliyodhulumu wenzake! Akaandaa na sherehe ya kuizindua siku ya Jumapili.. Akamualika mama yake mzazi toka Moshi na ndugu na jamaa na marafiki wengine

Siku ya uzinduzi asubuhi ile ya Jumapili watu wengine wakiws wameenda kanisani, wengine waliobaki nyumbani wakiandaa vyakula nk.. Mama mzazi akawa yuko sebuleni anaangalia TV jamaa kalala ndani
Walifika watu watatu rika la mwanae wakaingia mpaka sebuleni na kumsalimia mama kwa heshima zote kisha wakamuulizia jamaa

Mama mzazi akidhani ni wageni waalikwa akamuita mwanae! Jamaa akatoka ndani akiwa na uchovu mwingi.. Ghafla uso kwa uso anakutana na wale jamaa zake aliowapiga
Jamaa bila kupoteza muda wakamwambia mama yake kwamba kilichowaleta pale ni roho ya mtoto wake! Jamaa akajaribu kuwaomba wasimdhuru atawapatia chao, lakini wakamwambia siku hiyo hawakuhitaji hela tena bali roho yake tuu..

Akala risasi tatu akafa palepale jamaa wakasepa bila kuchukua hata sindano..! Walioenda kanisani na wageni waalikwa wengine walikuta msiba badala ya sherehe za uzinduzi wa nyumba
 
Dah Aisee....

Vipi kuhusu mwendazake, unaweza kutupa story kidogo ni nini kilimkumba akadedi wakati mzee wa Namungo alituhakikishia mdingi yuko rijali anachapa kazi.....??
 
Kisa cha nne
Mauaji siku ya kipaimara Tegeta
Familia ikiwa imeenda kanisani na ndugu wengine kwenye kipaimara cha first born baba alibaki nyumbani kwa maandalizi ya sherehe
Kwenye saa tano hivi walikuja watu wawili wakagonga geti na kufunguliwa na msichana wa kazi.. Bila kujua nia yao ovu walimuuliza kama baba yupo naye akawajibu yupo na kuwaongoza mpaka sebuleni
Jamaa hawakuwa na maneno mengi walimmiminia risasi za kutosha na kutokomea kusikojulikana..
Sherehe za kipaimara zikageuka msiba wa baba wa familia
 
Vipi kuhusu yule marehemu aliyefufuka mochware wakati unakagua maiti, afu ukamshindilia mangumi ili adedi tena.... Kisa chake ilikuwa nini?
 
Back
Top Bottom