Mauaji ya visasi

Mauaji ya visasi

Kisa cha pili
Mauaji Mbezi Siku ya uzinduzi wa nyumba

Jamaa mmoia mwenyeji wa Moshi kwa akina Mamndenyi mtani wangu na Asprin babu kijana.. Huyu mwana alipiga dili ndefu na wenzake ila kwenye mgao akawazima wenzake akasepa na mzigo wote akapotea mazima..

Akaibukia Mbezi akanunua kiwanja akajenga nyumba nzuri kubwa ya kisasa kwa ile pesa ya dili aliyodhulumu wenzake! Akaandaa na sherehe ya kuizindua siku ya Jumapili.. Akamualika mama yake mzazi toka Moshi na ndugu na jamaa na marafiki wengine

Siku ya uzinduzi asubuhi ile ya Jumapili watu wengine wakiws wameenda kanisani, wengine waliobaki nyumbani wakiandaa vyakula nk.. Mama mzazi akawa yuko sebuleni anaangalia TV jamaa kalala ndani
Walifika watu watatu rika la mwanae wakaingia mpaka sebuleni na kumsalimia mama kwa heshima zote kisha wakamuulizia jamaa

Mama mzazi akidhani ni wageni waalikwa akamuita mwanae! Jamaa akatoka ndani akiwa na uchovu mwingi.. Ghafla uso kwa uso anakutana na wale jamaa zake aliowapiga
Jamaa bila kupoteza muda wakamwambia mama yake kwamba kilichowaleta pale ni roho ya mtoto wake! Jamaa akajaribu kuwaomba wasimdhuru atawapatia chao, lakini wakamwambia siku hiyo hawakuhitaji hela tena bali roho yake tuu..

Akala risasi tatu akafa palepale jamaa wakasepa bila kuchukua hata sindano..! Walioenda kanisani na wageni waalikwa wengine walikuta msiba badala ya sherehe za uzinduzi wa nyumba
Huyo nae aliyatafuta. Unacheza dili na wenzako wanarisk pengine maisha yao halafu unaleta mzaha mwishoni.
 
😳😳😳😳.. me ndio maana nimeacha kwenda Chapel... Mambo ya magumashi ni mengi mno.
Una shida zako tu bro. Mbona mambo yapo straight tu ila uzushi ni mwingi unaowapotosha vijana mnaokurupuka bila kutafakari. Kuna vitabu vingi ambavyo vinaeleza maisha ya Adam na Hawa na Mmandenyi anasema kitabu cha "Legends of Jews " ndicho kinachosema eti nyoka alimlala Hawa wakazaa Kaini. Huo ni upotoshaji, sasa nyoka(Shetani) ni Roho itawezaje kuzaa na Hawa(Mwili). Huo ni uongo ni sawa na uzushi "eti majini yanazaa na wanadamu"
 
Kuweni makini na hivi vitabu vingine vinaandikwa na secret society ambayo inalenga kuharibu maudhui ya mafundisho ya KIMUNGU na kuleta mafunzo ya kishetani. Kuweni makini sana.
Ni sahihi vingi vina upotoshaji wa haki ya juu. Vipo vingi ambavyo sio vya kibiblia na vina upotoshaji mkubwa. Hiyo asemayo mmandenyi kama "Legends of Jews " ndio kinasema "Nyoka alizaa na Hawa "
 
Mkuu reference ni bible kwa hiyo ukisema ni chai meaning Bible ndio chai sio Mimi nayeleta story kutokea humo.

Bible ipo clear kwamba "Wana wa Mungu" walizaa na hao binadamu na reference ni Mwanzo 6 na hiyo Yuda 1. Ukitaka kuona hili hata uzao wao haukufutika kwa gharika rejea Mwanzo 13 utaona wapo hao watoto wa cross breeding hii.

Kuhusu malaika kuwa na hisia, ndio hoja ya shape shifting inapoingia hao walioasi ni wale walikua "watchers" yaani walipewa jukumu la kuwafunza wanadamu mambo mengi kama kuwinda, kusoma nyota, medicine, engineering n.k sasa mfano wakati wanamtembelea Abraham malaika waliweza hadi kula chakula, walisikia njaa, na hata yule aliyepigana na Yakobo "alichoka" baada ya mpambano wa usiku kucha.

Nachojaribu kusema in reference kwa biblia Ina maana malaika wote waliofanya interaction na binadamu walivaa miili ya kibinadamu hivyo kuchukua character zetu kama vile njaa, kuchoka, na tamaa kama iliyowakuta hao malaika wanaotajwa kwenye Injili ya Yuda.
Mkuu Naona uko vzr kwenye bible Kuna madn nayapta mpak nataman kuifugua bibie aisee
 
Kiboko ni ile ya shujaa Mwamwindi alipochoshwa na maonevu na dhuluma za mkuu wa mkoa Dr. Kleruu......
Leo tarehe 25/12/2018, siku ya Krismasi, ni miaka 47 imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa.

Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.

Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR.

.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika, Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele.

Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo! Dr. KLERUU, mara kwa mara, alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara" na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo, bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula!.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa, kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.

Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu, Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho, hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

Jumamosi ya tarehe 24/12/1971, Dr. KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani, Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake, Jumapili ya tarehe 25/12/1971, Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba muda wa saa 11 jioni, Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake.

Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake(Mohamed) na watu wawili aliowaajiri( Yadi Chaula na Charles Mwamalata), Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo. Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya Peugeot 404 rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa. Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we".

MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool". Katika eneo hilo walikuwa wao wawili tu kwani watu wengine walikuwa mbali kidogo. Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu". MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba, ni mahali ninapozika ndugu zangu". Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema "Swela", akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo!!! MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa, akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

Mjini Iringa, watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni, MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo, mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi.

Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary". Kesho yake, siku ya jumatatu, mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani! Msako ulipoanza usiku huohuo, jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa!.

Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa, anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka- "Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU. Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti. Kwa mawazo yangu, Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa. Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."

Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE, wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali. Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima. Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL, MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mf Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi! Aidha, nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.

Ikabidi mwanae (AMANI MWAMWINDI)(21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsukitisha sana Mzee MWAMWINDI. AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE, nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo, MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe. Baada ya kupita siku kadhaa, wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo, Isimani. Hata hivyo, tafrani hiyo iliyokuwaimewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"!.

Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu. Kesi ilipoanza kusikilizwa, ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa "si wa nchi hii!.

Tarehe 2/10/1972, baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort", Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria(aliyehudumu Tanzania toka 1970-1973) alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa "provoked" na marehemu, Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo-mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha, pasina shaka, kwamba aliua kwa kudhamiria.
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI

. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu.

Baada ya msiba, familia ya DR. KLERUU ilirudi Kilimanjaro. Hata hivyo, Mwalimu NYERERE na KARUME na baadae ABDU JUMBE walikuwa karibu sana na mjane wa DR. KLERUU na wakawasomesha wanawe nchini Urusi na Bulgaria. Aidha, viongozi wengine waliwatia moyo na kuwafariji sana mf. Marehemu Mzee RASHID KAWAWA na mama GETRUDE MONGELA. Dr. KLERUU aliacha watoto wanne ambao ni Eva, Andrew, Carmen na Edwin.

Mwezi Machi 2014, familia ya DR. KLERUU na ya MWAMWINDI zilikutana kwa furaha ili kusameheana kwa tukio hilo. Bi. EVA KLERUU(60) ambaye ni mtoto mkubwa wa Dr. KLERUU na Bw. AMAN MWAMWINDI(67) (aliyekuwa Meya wa mji wa Iringa) walifanya jambo hilo la kihistoria na hivyo kuyaishi kivitendo maandiko ya vitabu vitakatifu yatutakayo wanadamu kusameheana. Picha hii chini inawaonesha wawili hao wakiwa na bashasha baada ya tendo hilo la kihistoria na lisilo la kawaida.

Mnara wa DR. KLERUU umejengwa kwenye "mji" wa MWAMWINDI mahali ambapo alipigwa risasi . Nyumba ya Mkuu wa Mkoa DR. KLERUU bado ipo. Picha hizi hapa chini zinamuonesha Mnyalukolo MWAMWINDI baada ya kujisalimisha polisi pamoja na nyumba ya DR. KLERUU.

REST IN PEACE:

1. Dr. W. KLERUU

2. S. A. MWAMWINDI
 
Asante. Historia safi kabisa iliyonyooka. Kama unaweza kuzipata hizo picha please ziweke tuzione.
 
Mwamba mwenyewe
WhatsApp%20Image%202019-01-15%20at%2023.12.58%20(1).jpg
 
Ninao wengi wa kuwalipa kisasi kiasi kwamba naishia kucheka na kusema acha ninywe bia maisha yaendelee. Hakika nimeamini nina hasira kali sana na Mungu ameota mbegu kuu njema ndani yangu.

Si muda sahihi wa kusema neno bali nashukuru yale mema niliyoyaongeza baada ya kusoma visa na simulizi kadhaa mahali hapa. Shukrani sana.
 
Nina visa viwili na kupitia visa hivi vimenifunza kuheshimu makubaliano na mtu/watu au kutokutoa ahadi bila kuitafakari!!!

Cha kwanza
ni 2004:jamaa alikuwa ni rafiki yake binamu yangu mkubwa sasa kutokana na mara nyingi kuwa naongozana na huyu binamu yangu (R.I.P) nikajikuta huyu jamaa nimekuwa nyoka wake,ilikuwa kawaida kupewa million mbili peleka kwa fulani nenda pale chukua hela kadhaa niletee so automatically nikajikuta nimeingia kwenye circle ya watu wake,imeenda hivyo sasa siku moja akanipa Tsh 700,000/=  akaniambia wapelekee fulani!

Jamaa walikuwa watu wa deal za sigara dk kama 17 baada ya kuachana nae nikiwa ndani ya Ki-Hiace akani-text rudi kufika pale nilipomuacha nikamkuta anaongea na simu kama wanatukanana na anayeongea upande wa pili siku tatu mbele wakamvamia jamaa kwake Mbezi Kibanda Cha Mkaa usiku wa saa mbili mbele ya mkewe,alivyotuhadithia mkewe jamaa alimtuma akachukue kwenye draw 3mill cash wamuache wakasema wao hawakutumwa pesa wakammaliza,alipigwa risasi moja makalioni nyengine shingoni kwa nyuma kwenye pingili za mgongo na shingo akafa on the spot na hawakuchukua chochote.

Kwa sababu nilishakuwa na muunganiko na jamaa zake kadiri siku zilivyoenda wakawa wananifungulia codes kwamba alipewa dili Canter imejaa sigara akapatana bei kwanza kwa kufika hela ndogo kisha akawaambia wapeleke mzigo wakiwa njiani akawakamatisha jamaa kwa askari then akazunguka upande wa pili kwamba yeye atamalizana na hao askari so wao wachukue sikumbuki bei but haikufika 2mill jamaa wakakubali but still akaiona ni nyingi akawapunguza tena hata walipokubali akawa pesa hawapi na mzigo askari mwenye file hanyooshi maelezo wakaja kutonywa na askari mwengine kwamba mzigo jamaa alishachukua na hata haukufika hapo kituoni.

Cha pili:mwaka 2017,huyu nae tulikutana kimjini mjini alikuwa mtu wa kupokea bond za magari (wenyewe wanaita hela za moto) Ila yeye alikuwa mtu akiacha gari bond anachonga funguo ya ziada siku mwenye nayo akiigomboa hakai nayo mwezi inapotea akajichanganya akakopesha watu wanaojuana bila yeye kujua akawapiga tukio wakaunga dots walimmalizia bar kaenda msalani kukojoa jamaa wakamfata huko huko wakammaliza.

Muhimu sana kuzingatia makubaliano au ahadi tunazowapa wenzetu.
Kuna watu huwa wanajifanya hawajui vibaya, hawa watu ndio huwa wanakutwa na haya matukio aiseee.
 
Leo tarehe 25/12/2018, siku ya Krismasi, ni miaka 47 imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa.

Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.

Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR.

.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika, Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele.

Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo! Dr. KLERUU, mara kwa mara, alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara" na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo, bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula!.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa, kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.

Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu, Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho, hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

Jumamosi ya tarehe 24/12/1971, Dr. KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani, Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake, Jumapili ya tarehe 25/12/1971, Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba muda wa saa 11 jioni, Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake.

Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake(Mohamed) na watu wawili aliowaajiri( Yadi Chaula na Charles Mwamalata), Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo. Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya Peugeot 404 rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa. Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we".

MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool". Katika eneo hilo walikuwa wao wawili tu kwani watu wengine walikuwa mbali kidogo. Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu". MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba, ni mahali ninapozika ndugu zangu". Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema "Swela", akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo!!! MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa, akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

Mjini Iringa, watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni, MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo, mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi.

Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary". Kesho yake, siku ya jumatatu, mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani! Msako ulipoanza usiku huohuo, jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa!.

Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa, anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka- "Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU. Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti. Kwa mawazo yangu, Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa. Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."

Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE, wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali. Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima. Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL, MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mf Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi! Aidha, nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.

Ikabidi mwanae (AMANI MWAMWINDI)(21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsukitisha sana Mzee MWAMWINDI. AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE, nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo, MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe. Baada ya kupita siku kadhaa, wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo, Isimani. Hata hivyo, tafrani hiyo iliyokuwaimewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"!.

Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu. Kesi ilipoanza kusikilizwa, ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa "si wa nchi hii!.

Tarehe 2/10/1972, baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort", Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria(aliyehudumu Tanzania toka 1970-1973) alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa "provoked" na marehemu, Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo-mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha, pasina shaka, kwamba aliua kwa kudhamiria.
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI

. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu.

Baada ya msiba, familia ya DR. KLERUU ilirudi Kilimanjaro. Hata hivyo, Mwalimu NYERERE na KARUME na baadae ABDU JUMBE walikuwa karibu sana na mjane wa DR. KLERUU na wakawasomesha wanawe nchini Urusi na Bulgaria. Aidha, viongozi wengine waliwatia moyo na kuwafariji sana mf. Marehemu Mzee RASHID KAWAWA na mama GETRUDE MONGELA. Dr. KLERUU aliacha watoto wanne ambao ni Eva, Andrew, Carmen na Edwin.

Mwezi Machi 2014, familia ya DR. KLERUU na ya MWAMWINDI zilikutana kwa furaha ili kusameheana kwa tukio hilo. Bi. EVA KLERUU(60) ambaye ni mtoto mkubwa wa Dr. KLERUU na Bw. AMAN MWAMWINDI(67) (aliyekuwa Meya wa mji wa Iringa) walifanya jambo hilo la kihistoria na hivyo kuyaishi kivitendo maandiko ya vitabu vitakatifu yatutakayo wanadamu kusameheana. Picha hii chini inawaonesha wawili hao wakiwa na bashasha baada ya tendo hilo la kihistoria na lisilo la kawaida.

Mnara wa DR. KLERUU umejengwa kwenye "mji" wa MWAMWINDI mahali ambapo alipigwa risasi . Nyumba ya Mkuu wa Mkoa DR. KLERUU bado ipo. Picha hizi hapa chini zinamuonesha Mnyalukolo MWAMWINDI baada ya kujisalimisha polisi pamoja na nyumba ya DR. KLERUU.

REST IN PEACE:

1. Dr. W. KLERUU

2. S. A. MWAMWINDI
Dah aiseee bonge la story na imeelezewa kwa ufundi na mtiririko mzuri sana kiasi kwamba hata kiziwi anaweza kuelewa bila kusikiliza.
 
Back
Top Bottom