Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 682
- 1,031
Usafiri wa boda boda umekuwa kipimbilio la vijana wengi kupata kipato.
Wengi wanaofeli shuleni na wale wanaohitimu na kukosa ajira hukimbilia kwenye shughuli hii ya kusafirisha watu na/au mizigo.
Usafiri wa boda boda una changamoto nyingi ambazo humpata mwendesha boda boda na abiria wake pia.
Mojawapo ya changamoto hizo ni mauaji holela na ya kikatili ya waendesha boda boda (mbali na ulemavu na vifo vitokanavyo na ajali). Katika sehemu mbalimbali ya nchi yetu kumekuwa na kesi nyingi za vijana waendesha boda kujeruhiwa au kuuawa na pikipiki zao kupotea.
Matukio mengi ya mauaji hufanyika nyakati za usiku kwenye vichochoro, misituni nk.
Simulizi nyingi ni za boda kupata abiria ambao huwaomba kupelekwa sehemu fulani ambapo mtego huwekwa wa kufanya uporaji wa chombo kwa kumjeruhi au kumtoa uhai mhusika.
Miili yao hutelekezwa ikiwa na majeraha ya kutisha ya vitu vyenye ncha kali, alama za kunyongwa au ikiwa imefungwa kwa kamba.
Kwenye matukio hayo ya uporaji waathirika wengi miongoni mwa waendesha boda boda ni wale ambao wana vyombo vipya, wanaoanza kazi hiyo kwa mara ya kwanza nk.
Mbali na mambo mengi yanayosababisha matukio haya kuna la waendesha boda boda kuchongeana wao kwa wao.
Ukilitafakari jambo hili utaona kwamba hata baadhi ya waendesha boda boda wenyewe kwa wenyewe hushiriki kuwapora, kuwajeruhi au kuua wenzao na kutoweka na vyombo vyao.
Unakuta kwenye vijiwe wenye vyombo vipya ndiyo waathirika wakubwa. Sasa utaujiuliza hao waporaji au wauaji wanajuaje kwamba kwenye kijiwe kuna pikipiki mpya na hivyo kuanza kumfuatilia au kumwinda mhusika?
Jamii sasa inashuhudia umwagaji wa damu na mauaji ya kikatili ya waendesha boda boda wasio na hatia na mwisho wake ni laana kwa jamii.
Matukio mengi ya mauaji ya waendesha boda boda hayafuatiliwi au kuchunguzwa kwa kina ili kubaini wahusika hivyo kukomesha kabisa matukio hayo.
Tusipochukua hatua tutaendelea kuwapoteza vijana wetu na kuijaza nchi yetu laana ya damu.
Tupendane, tulindane, tudumishe haki, tudumishe amani na usawa kwa watu wetu wote.