Mauaji ya visasi

Mauaji ya visasi

Kisa cha pili
Mauaji Mbezi Siku ya uzinduzi wa nyumba

Jamaa mmoia mwenyeji wa Moshi kwa akina Mamndenyi mtani wangu na Asprin babu kijana.. Huyu mwana alipiga dili ndefu na wenzake ila kwenye mgao akawazima wenzake akasepa na mzigo wote akapotea mazima..

Akaibukia Mbezi akanunua kiwanja akajenga nyumba nzuri kubwa ya kisasa kwa ile pesa ya dili aliyodhulumu wenzake! Akaandaa na sherehe ya kuizindua siku ya Jumapili.. Akamualika mama yake mzazi toka Moshi na ndugu na jamaa na marafiki wengine

Siku ya uzinduzi asubuhi ile ya Jumapili watu wengine wakiws wameenda kanisani, wengine waliobaki nyumbani wakiandaa vyakula nk.. Mama mzazi akawa yuko sebuleni anaangalia TV jamaa kalala ndani
Walifika watu watatu rika la mwanae wakaingia mpaka sebuleni na kumsalimia mama kwa heshima zote kisha wakamuulizia jamaa

Mama mzazi akidhani ni wageni waalikwa akamuita mwanae! Jamaa akatoka ndani akiwa na uchovu mwingi.. Ghafla uso kwa uso anakutana na wale jamaa zake aliowapiga
Jamaa bila kupoteza muda wakamwambia mama yake kwamba kilichowaleta pale ni roho ya mtoto wake! Jamaa akajaribu kuwaomba wasimdhuru atawapatia chao, lakini wakamwambia siku hiyo hawakuhitaji hela tena bali roho yake tuu..

Akala risasi tatu akafa palepale jamaa wakasepa bila kuchukua hata sindano..! Walioenda kanisani na wageni waalikwa wengine walikuta msiba badala ya sherehe za uzinduzi wa nyumba

Mkuu samahani hiki kisa ni kile cha miaka ya 2008 kurudi nyumba, mbezi beach, alipigwa risasi mbele ya familia yake na watoto walikuepo, au nakosea ndugu Mshana
 
Mauaji ya visasi (kulipa kisasi) ni dhambi ya tatu kuzaliwa duniani
Dhambi ya kwanza ngono na usaliti pale Eden, lakini hii ina mazonge mengi kwakuwa uongo na kutotii maagizo vyote vinaingia hapo! Ni dhambi yenye vipengele A, B C na D

Dhambi ya tatu ni mauaji, ambayo asili yake ni choyo na wivu, pale Kaini alipofanya uchoyo wa kutoa sadaka iliyonona na matokeo yake ikakataliwa.. Ya mdogo wake Abel ilipokelewa na ndipo roho ya chuki ilipomuingia Kaini na kuamua kumuua mdogo wake kwa mama. Adam hakuwa babayake wa damu.

Tangu hapo mkeka wa mauaji ya visasi uliasisiwa ulimwenguni.. Tangia hapo maelfu kwa maelfu wameuawa kwa mauaji ya visasi. Nimekisoma kisa cha kijana wa Songwe aliyeuwawa mbele ya mkewe na mwanae na wauaji wakaondoka bila kuchukua chochote! Visa hivi ni vingi mno na nitasimulia baadhi kadiri ya kumbukumbu zangu, nakukaribisha nawe uungane nami kama kuna chako unakikumbuka!

Maisha haya hutukutanisha na wengi lakini pia na mengi, kuna watu kwa sababu zozote zile wanajiona ya kwamba wao ndio wao na wengine si kitu.

Wao ndio wanastahili kupata
Wao ndio wanastahili maisha mazuri
Wao ndio wanaijua pesa kuliko wengine
Wao ndio wanastahili maisha na vitu vizuri kuliko wengine

Visa hivi vya mauaji ya visasi vina asili moja! Wauaji hawachukui chochote! Visa hivi vyanzo vyake ni
Usaliti wa kibiashara/dili
Usaliti kwenye mapenzi/mahusiano
Harakati za kisiasa na madaraka
Wivu wa maendeleo/kupata kwa wengine
Dhuluma
Utemi
Ubabe nk nk
Kwenye hili kuna wauaji wa kukodi ama baadhi hutekeleza mauaji wenyewe tena kwa taarifa kabla ya kutekeleza mauaji.

Sometimes kwenye haya mambo ukishindwa kusamehe lipa kisasi! Haikuongezei kitu lakini inakupunguzia maumivu! Ila usiijaribu hii njia imejaa mabaya!

Mnamkumbuka yule traffic aliyeuliwa kwa risasi pale sayansi ? Jamaa alikuja na boda akamuuliza Afande unanikumbuka? Jamaa akajibu ndio.

Jibu hilo lilitosha kummininia risasi zilizoondoka na uhai wake
Nitakuja na visa vingine.
 
😳😳😳😳.. me ndio maana nimeacha kwenda Chapel... Mambo ya magumashi ni mengi mno.
Mkuu, inapendeza pale ambapo hujaelewa jambo UULIZE usikae kimya halafu ukajiridhisha kwamba ni magumashi. Nakushauri nenda Chapel na uwaulize maswali hao utakaokuwa unawasikiliza. Chukua muda wako japo dk chache sio masaa pitapita kwenye maandiko.
NB: Sio kila kinachohubiriwa ni sahihi. Mengine KWELI ni magumashi ya kiwango cha 4G.
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
Nyoka aligegeda mtu
 
Dhambi ya tatu ni mauaji, ambayo asili yake ni choyo na wivu, pale Kaini alipofanya uchoyo wa kutoa sadaka iliyonona na matokeo yake ikakataliwa.. Ya mdogo wake Abel ilipokelewa na ndipo roho ya chuki ilipomuingia Kaini na kuamua kumuua mdogo wake kwa mama. Adam hakuwa babayake wa damu.

Kaini siyo mtoto wa Adam ?
zitto junior pitia hapa.
 
kaka ambiere, unashaurije kuhusu kulipa kisasi?je tumuachie MUNGU kama bible inavyosema kwetu wakristo?au tumalizaane na wabaya wetu tu wenyewe!maaana unafanyiwa mambo yenye kuumiza sana mpaka unakua na uchungu mwingi kiasi kwamba unatamani kulipiza ili uchungu uondoke!ila dini ndo zinatuzuia tuu!yaani aiseee

Ukishindwa kusamehe lipa kisasi
 
Kisa Cha tano;
Kuna jamaa alifumaniwa akimla mke wa mwenzie mida ya saa Saba usiku.Baada ya kustukiwa akaambiwa achague sehemu ambayo angependelea kutupwa Kati ya mtoni na barabarani baada ya kuuaua.
Mgoni akachagua barabarani ili aweze kuokotwa na watu wakamzike.

Jamaa akafanyiwa full body massage kwa muda wa lisaa limoja,akapigwa kichapo kikali Sana mixer kukakatwa katwa mapanga kila sehemu.Akakata Moto.

Picha linaisha jamaa akasafirishwa kwa umbali wa kilomita tatu kutoka eneo la tukio akatupwa kando ya barabara kwenye mtaro.Ikawa imeisha hiyo.
 
Ndio kwanza natoka msibani...na bila shaka nitausindikiza msiba mpaka kaskazin... yes visas...na kisa kipo hivi...

Ilikuwa siku ya jumapili usiku nipo pub flan napiga kilaji huku nasubiria vitasa vya mandonga...akatokea dogolas yupo na rafiki yake...wakanipa hi thn wakajongea kwenye meza yao na nikamuita muhudum nikamwambia wasikilize wale...basi akawasikiliza nikawaanzishia vinywaji vya kama 25,000 hivi...na mim nikawa na jamaa yangu tunazipasua bia na k vant..

Ilipofika mida ya saa tano usiku...nikawa nimechoka so nikaenda zangu lala...Asubuh ya jumatatu nasikia taarifa za msiba dada mmoja kauwawa na kubakwa..kudadis kumbe ni mke wa mdogo wangu sio wa damu lakin nimempita umri...

Jana nikaenda msiban na nikakutana na dogo na akaanza nisimulia kisa kilivyo tokea...

Nikamuuliza ilikuwaje..akaniambia pale ulinipo niacha..tulihama bar na kuhamia bar nyingine...ambayo hyo bar ipo karibu na kwao..sasa kuna jamaa alitokea na ni jiran yao na wamekua wote...akamwambia mwana amnunulie bia kwel dogo akamnunulia bia 2...mchiz akanywa akasepa kumbe mchiz ana jamaa yake hapo washapanga kuwa kwa kuwa dogo yupo hapa basi mkewe atakuwa nyumban peke yake so lazima akampige machine kwan anamtamanig muda mrefu...

Akamuacha jamaa yake pale amlie rada dogo yy akaenda nyumban kwa dogo akavunja mlango...akamkuta mke wa dogo na mtt kama wa miaka 7 wa kike...akamtia ngum mke wa dogo kumtoa wenge...akaanza kumkaba na kumvua ngoa sasa yule mke wa dogo ikasemekana akakosa pumzi ...jamaa akala mzigo mid kama ya saa tisa usiku

Kaka yake na dogo akawa anarudi gafla anakutana na mtu anatoka mbio...na anajigonga ukutan sasa yy akajua ni mwiz akaanza mkimbiza bila kujua mchiz kafanya unyama gan ndan...akamkimbiza sana lakin hakufanikiwa kumkamata lakin alimihis kama ni mtu fulan...hivyo akarud home akakuta umeme umekatika...sasa anaita shemej wala haitiki...akakutana na mtoto wa dogo...akamwambia mama kavamiwa na kaka fulan akawa anampiga...kwenda chumban anamkuta shemeji yake kama kazimia na damu nyingi kitandan...sasa nyumba yao ipo karibu na kituo cha polisi na hata hospital ya rufaaa ipo karibu na kwao...

Kaka mtu akambeba mtoto kwenda nae polis kutoa taarifa...huku nyuma dogo anarud nyumban...yupo na jamaa yake anakuta mazingira ambayo hayaelewi...anaingia chumban anakutana na mke wake hajielewi...anamtafuta mtt hamuon...ikabid ambebe mkewe kumpeleka hospital...mke anachukuliwa vipimo taarifa inatoka amefariki...jamaa anawaza kama wamemuua mke basi na mtt atakuwa wanemuua kupoteza ushahid...sasa daktar wakamwambia aende polis kureport tukio...anaenda polis anakutana na kaka yake pamoja na mtoto wake

Dogo anafika kituon anamwambia kaka yake wameniulia mke...kaka yake anamwambia hyo mtu nimekutana nae na nimemkimbiza...dogo akauliza amevaaje..akamwambia amevaa mabuti na kofia...dogo akavuta hisia na kumwambia kaka yake au ni muddy?? Kaka mtu akamwambia atakuwa ni yy caz alihis hicho kitu lakin hakuwa na uhakika

Wakatoka na defender pale mpaka eneo la tukio...polis wakachukua picha na mlangon kuna alama ya viatu alivyo kuwa anauvunja...

Wakaenda mpaka kwa kina muddy ni nyumba ya pili tu ni jiran sana..

Wakagonga na kuna mtu akafungua polis wakahoji muddy yupo jamaa akawa mbishi akapigwa rungu moja tuu...akasema muddy anakaa chumba cha tatu...polis dogo na kaka yake...wakagonga sana mlango bila mafanikio...ikabid wauvunje..muddy anaamka anajifanya ametoka usingizin na hajui lolote...

Polis wakamuhoji viatu vyako vipo wap...akawaonesha lakin baada ya upekuz zaid wakakuta ameficha lile buti...kwel ni yy..wakamwambia umechukua nn nyumba ya hapo jiran akatoa simu na suti...dogo anajua paswed ya mkew..kuiweka ikafunguka..pemben kulikuwa na shoka dogo akachukua akataka kumkata kata muddy na polis walimdhibit asifanye ivo..

Wakamchukua muddy kwa mahojiano zaidi...dogo analia tu muda wote...jana walimuhoji taarifa ya habari...kumuuliza kama walikuwa na bifu na muddy akanijibu hapana lakin kuna rafik yake muddy aliiba mtaani na dogo alimuona so alienda kureport polis na wakamueka ndan week mbili..na alivyotoka akamwambia dogo nitakuonesha...sasa ndio wakaungana na muddy kufanya malipiz...
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
Mmmmhh rudi kwenye uganga wa kienyeji sasa. Huku utatuia kwenye dhambi bure.
 
Nina visa viwili na kupitia visa hivi vimenifunza kuheshimu makubaliano na mtu/watu au kutokutoa ahadi bila kuitafakari!!!

Cha kwanza
ni 2004:jamaa alikuwa ni rafiki yake binamu yangu mkubwa sasa kutokana na mara nyingi kuwa naongozana na huyu binamu yangu (R.I.P) nikajikuta huyu jamaa nimekuwa nyoka wake,ilikuwa kawaida kupewa million mbili peleka kwa fulani nenda pale chukua hela kadhaa niletee so automatically nikajikuta nimeingia kwenye circle ya watu wake,imeenda hivyo sasa siku moja akanipa Tsh 700,000/=  akaniambia wapelekee fulani!

Jamaa walikuwa watu wa deal za sigara dk kama 17 baada ya kuachana nae nikiwa ndani ya Ki-Hiace akani-text rudi kufika pale nilipomuacha nikamkuta anaongea na simu kama wanatukanana na anayeongea upande wa pili siku tatu mbele wakamvamia jamaa kwake Mbezi Kibanda Cha Mkaa usiku wa saa mbili mbele ya mkewe,alivyotuhadithia mkewe jamaa alimtuma akachukue kwenye draw 3mill cash wamuache wakasema wao hawakutumwa pesa wakammaliza,alipigwa risasi moja makalioni nyengine shingoni kwa nyuma kwenye pingili za mgongo na shingo akafa on the spot na hawakuchukua chochote.

Kwa sababu nilishakuwa na muunganiko na jamaa zake kadiri siku zilivyoenda wakawa wananifungulia codes kwamba alipewa dili Canter imejaa sigara za mazabe akapatana bei kwanza kwa kufika hela ndogo kisha akawaambia wapeleke mzigo wakiwa njiani akawakamatisha jamaa kwa askari then akazunguka upande wa pili kwamba yeye atamalizana na hao askari so wao wachukue sikumbuki bei but haikufika 2mill jamaa wakakubali but still akaiona ni nyingi akawapunguza tena hata walipokubali akawa pesa hawapi na mzigo askari mwenye file hanyooshi maelezo wakaja kutonywa na askari mwengine kwamba mzigo jamaa alishachukua na hata haukufika hapo kituoni.

Cha pili:mwaka 2017,huyu nae tulikutana kimjini mjini alikuwa mtu wa kupokea bond za magari (wenyewe wanaita hela za moto) Ila yeye alikuwa mtu akiacha gari bond anachonga funguo ya ziada siku mwenye nayo akiigomboa hakai nayo mwezi inapotea akajichanganya akakopesha watu wanaojuana bila yeye kujua akawapiga tukio wakaunga dots walimmalizia bar kaenda msalani kukojoa jamaa wakamfata huko huko wakammaliza.

Muhimu sana kuzingatia makubaliano au ahadi tunazowapa wenzetu.
 
Ndio kwanza natoka msibani...na bila shaka nitausindikiza msiba mpaka kaskazin... yes visas...na kisa kipo hivi...

Ilikuwa siku ya jumapili usiku nipo pub flan napiga kilaji huku nasubiria vitasa vya mandonga...akatokea dogolas yupo na rafiki yake...wakanipa hi thn wakajongea kwenye meza yao na nikamuita muhudum nikamwambia wasikilize wale...basi akawasikiliza nikawaanzishia vinywaji vya kama 25,000 hivi...na mim nikawa na jamaa yangu tunazipasua bia na k vant..

Ilipofika mida ya saa tano usiku...nikawa nimechoka so nikaenda zangu lala...Asubuh ya jumatatu nasikia taarifa za msiba dada mmoja kauwawa na kubakwa..kudadis kumbe ni mke wa mdogo wangu sio wa damu lakin nimempita umri...

Jana nikaenda msiban na nikakutana na dogo na akaanza nisimulia kisa kilivyo tokea...

Nikamuuliza ilikuwaje..akaniambia pale ulinipo niacha..tulihama bar na kuhamia bar nyingine...ambayo hyo bar ipo karibu na kwao..sasa kuna jamaa alitokea na ni jiran yao na wamekua wote...akamwambia mwana amnunulie bia kwel dogo akamnunulia bia 2...mchiz akanywa akasepa kumbe mchiz ana jamaa yake hapo washapanga kuwa kwa kuwa dogo yupo hapa basi mkewe atakuwa nyumban peke yake so lazima akampige machine kwan anamtamanig muda mrefu...

Akamuacha jamaa yake pale amlie rada dogo yy akaenda nyumban kwa dogo akavunja mlango...akamkuta mke wa dogo na mtt kama wa miaka 7 wa kike...akamtia ngum mke wa dogo kumtoa wenge...akaanza kumkaba na kumvua ngoa sasa yule mke wa dogo ikasemekana akakosa pumzi ...jamaa akala mzigo mid kama ya saa tisa usiku

Kaka yake na dogo akawa anarudi gafla anakutana na mtu anatoka mbio...na anajigonga ukutan sasa yy akajua ni mwiz akaanza mkimbiza bila kujua mchiz kafanya unyama gan ndan...akamkimbiza sana lakin hakufanikiwa kumkamata lakin alimihis kama ni mtu fulan...hivyo akarud home akakuta umeme umekatika...sasa anaita shemej wala haitiki...akakutana na mtoto wa dogo...akamwambia mama kavamiwa na kaka fulan akawa anampiga...kwenda chumban anamkuta shemeji yake kama kazimia na damu nyingi kitandan...sasa nyumba yao ipo karibu na kituo cha polisi na hata hospital ya rufaaa ipo karibu na kwao...

Kaka mtu akambeba mtoto kwenda nae polis kutoa taarifa...huku nyuma dogo anarud nyumban...yupo na jamaa yake anakuta mazingira ambayo hayaelewi...anaingia chumban anakutana na mke wake hajielewi...anamtafuta mtt hamuon...ikabid ambebe mkewe kumpeleka hospital...mke anachukuliwa vipimo taarifa inatoka amefariki...jamaa anawaza kama wamemuua mke basi na mtt atakuwa wanemuua kupoteza ushahid...sasa daktar wakamwambia aende polis kureport tukio...anaenda polis anakutana na kaka yake pamoja na mtoto wake

Dogo anafika kituon anamwambia kaka yake wameniulia mke...kaka yake anamwambia hyo mtu nimekutana nae na nimemkimbiza...dogo akauliza amevaaje..akamwambia amevaa mabuti na kofia...dogo akavuta hisia na kumwambia kaka yake au ni muddy?? Kaka mtu akamwambia atakuwa ni yy caz alihis hicho kitu lakin hakuwa na uhakika

Wakatoka na defender pale mpaka eneo la tukio...polis wakachukua picha na mlangon kuna alama ya viatu alivyo kuwa anauvunja...

Wakaenda mpaka kwa kina muddy ni nyumba ya pili tu ni jiran sana..

Wakagonga na kuna mtu akafungua polis wakahoji muddy yupo jamaa akawa mbishi akapigwa rungu moja tuu...akasema muddy anakaa chumba cha tatu...polis dogo na kaka yake...wakagonga sana mlango bila mafanikio...ikabid wauvunje..muddy anaamka anajifanya ametoka usingizin na hajui lolote...

Polis wakamuhoji viatu vyako vipo wap...akawaonesha lakin baada ya upekuz zaid wakakuta ameficha lile buti...kwel ni yy..wakamwambia umechukua nn nyumba ya hapo jiran akatoa simu na suti...dogo anajua paswed ya mkew..kuiweka ikafunguka..pemben kulikuwa na shoka dogo akachukua akataka kumkata kata muddy na polis walimdhibit asifanye ivo..

Wakamchukua muddy kwa mahojiano zaidi...dogo analia tu muda wote...jana walimuhoji taarifa ya habari...kumuuliza kama walikuwa na bifu na muddy akanijibu hapana lakin kuna rafik yake muddy aliiba mtaani na dogo alimuona so alienda kureport polis na wakamueka ndan week mbili..na alivyotoka akamwambia dogo nitakuonesha...sasa ndio wakaungana na muddy kufanya malipiz...
Dah mbaya sana hii poleni sana mkuu
 
Back
Top Bottom