Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
Mashekhe Wapo wengi na madarass pia. Wewe semea himaya ya nyumba yako tu

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Pepo lako kama limeangukia kwa Mwamposa, nenda naye tu. Muda ndio mwalimu wa kweli. Kwa sababu wachungaji wa aina hii wana wana vitu vitatu vinavyoshabihiana:
1) Muumini anafundishwa kuamini miujiza (kama kweli ipo/mazingaombwe) ya mchungaji. Mchungaji huwa ni Mungu mtu. Imani = na miujiza
2) Dini hizi huwa za ukoo. Baba mchungaji akifa, taasisi inakumbwa na migogoro na mara nyingi huhusisha mgawanyo wa mali- 99% dini nayo hufa, mfano Joshua,.
3)Wachungaji/viongozi huzungumzia mali kama msingi mkubwa wa dini hizi.

Kumradhi kama nimekosea! ila tafakari kama wewe ni muumini wa dini hizo.
Hata Yesu alitenda miujiza mingi Sana na hawakumwamini.
Ukiwa na Mungu lazima umiliki nchi ndo Bible inavyosema.
Kumbuka Mfalme Selemani alikuwa tajiri Sana.
 
Dah umenikumbusha Mwingira! Nenda Kibaha Kwamathias kuna sehemu inaitwa Umwelani kuna eneo kubwaaa la Mwingira, barabara zahumo ndani zina mpaka lami anawasomba watu toka Tanzania nzima anawavyonza mpaka nauli wanakosa maskini wa Mungu! Hawa watu huwaambii kitu wenyewe wanamwita Baba.
Wazungu wana msemo usemao "Dini ni bangi ya akili"
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Ushauri wangu ni kuwa ili uruhusiwe kuanzisha kanisa,ni lazima kuwa na mamlaka ya kupima vigezo vitakavyoweza kukuruhusu wewe kuwa na kanisa...
 
Ukiona wanaenda basi hujue mafuta yanawasaidia,wasipoenda basi hujue mafuta hayawasaidii mambo yao.
Kwaiyo kitu ambacho hakina faida kwako basi jua kina faida kwa wengine!
Mimi binafsi nishayatumia Maji na Mafuta ya Mwamposa kwa kumwaga ndani ya nyumba niliyokuwa nimepanga,aisee kuna vitu vya ajabu niliviona ndani ya ile nyumba;kuanzia mlangoni ninapoingilia,nilikuta dawa imefungwa na imewekwa kwenye fremu ya geti na ndani kwangu chini ya uvungu kuna Nng'e amekufa!siku zote nilikuwa sivioni ila baada ya kumwaga mafuta na maji niliviona.
Tangu nimeishi Ile nyumba kila pesa ninayoshika sioni imefanya kitu gani,baada ya kuhama ile nyumba leo namiliki mashamba na viwanja kibao.
Sikatai wapo Wahuni lakini mimi binafsi nimesaidiwa na Mafuta ya Mwamposa tena Wala sikuenda Dar es salaam,Mimi naishi Mwanza.Alipokuwa anaomba kwenye TV yake akasema chukua Maji na Mafuta na uelekeze kwenye TV,na nilifanya hivyo na leo mambo yangu yapo safi.
Kwaiyo kejeli siyo nzuri,mtu anamponda Mwamposa alafu kesho anaamkia kwa Waganga kuroga,sasa uyo mtu yeye ana usafi gani!!
Kwa nini kila mtu anatoa ushahidi wa hivi hivi mimi pia rafiki zangu wawili na ndugu zangu kadhaa wanasali hapo kwa mwamposa na wanatoa ushahidi wa kuona vitu kama hivyo baada ya kumwaga maji na mafuta wakiamka asubuhi wanakuta mlangoni vitu kama hivyo mara mijusi mara n'ge
Na wasi wasi labda hayo maji na mafuta ndio yanahivyo vitu.

Wamesha nishawishi sana kusali hapo ila mimi nilishasema siwezi kusali dini ya familia yaani katoka mtu huko kwake yeye na mkewe wameona njia ya kupata pesa ni ipi basi waanzishe kanisa ila huu ni ujinga sana.

Alafu swala jingine kwa nini anauza maji na mafuta na sadaka anachukua je dini ni biashara?
Mbona maji ya baraka wengine wanatoa bure iweje yeye anauza? Huu ni utapeli
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934

Yerricko bandiko lako ni zuri, na umeliwasilisha kwa umahiri mkubwa, je una uhakika gani hao watu kuwa hawajaenda mbinguni?
 
Kwahiyo tuache wauane tu?

Kama wanakwenda mbinguni kuna tatizo gani kaka? Ingekuwa ww una proof hawaendi mbinguni huenda ungekuwa sawa. Tunachokataa ni mtu kuua watu, sio hao wanaoridhia kufa waende mbinguni. Wao wameona hapa duniani hakuna raha kama mbinguni, kuna kosa lolote wao wenyewe kuridhia kwenda huko?
 
Wajinga bado wengi sana katika Dunia hiii haswa katika Bara la Afrika.

Hata hapa kwetu bado kuna baadhi ya makanisa yqnawatapeli sana waumini wake, wanatapeliwa sadaka n.k

Hilo la kutapeliana sadaka ni kwa madhehebu yote ya kikristo kuanzia Roman, KKKT, Anglikana nk, huko utakuta waumini wanalundikiwa michango hadi wanapoteza hamu ya kuendelea kuabudu.
 
Mawazo yako yakikubalika yatapelekea vurugu kubwa. Uabudu ni uamuzi binafsi wa mtu binafsi, hakuna mtu au mamlaka inayoweza kupima imani
Tukisema tutafute kanisa la kweli litabaki Katoliki peke yake na hata wewe hutakubali lakini ndio ukweli.

Sasa masuala ya kuoneana wivu kwa sababu tapeli mmojq wa kikristo anaibuka na kuwazidi matapeli wengine wa kikristo waliokuwapo kabla yake haifai kutumiwa kama kisingizio cha kuwakomoa matapeli wapya.

Ni kama ilivyo kwenye siasa za upiinzani karibia wote ni wasaka maslahi binafsi ila wanawadanganya wananchi kuwa wanawapigania mfano Zitto nk.

ni kweli watanzania wengi ni mbumbumbu katika maeneo .mengi na wajanja wameona furss ya kuvuna pesa kwa migongo yai ipo, wacha waendelee khvunwa:

Ilibidi kupiga marufuku imani itabidi pia baafhi ya wanasiasa nao wapigwe marufuku kwani wote wanatapeli.

Huwezi kuutoa ujinga ulioko kichwani mwa mtu kwa kutumia nguvu.

Nukuu: ' a thing continues to rest or move in straightvline (uniform motion) until acted upon by external force"..

Nimecheka kwa nguvu, eti mkiamua kutafuta kanisa la kweli litabaki RC, kwanini RC mkuu, au ni zile sanamu kule kanisani ndio kipimo cha ukweli wake?

Ukamalizia na kutoa mfano wa wanasiasa wa upinzani kuwa nao ni matapeli, ila kwenye hili hujawagusa CCM, huenda CCM umewafanananisha na hilo kanisa la Roma kuwa ndio wanasiasa wakweli. Nahisi umeishiwa na mifano ndio maana umeamua kugeuka futuhi.
 
Repose en paix...
Sijawahi kuona tajiri mwenye mapepo.
 
Ila kumpiga shetani kwa kumrushia mawe wewe ndio unaona hizo ni akili?
FB_IMG_1680344486235.jpg
Hii ndiyo akili?
 
Kwenye Bandiko lako ONDOA UISLAM, USIWEKE UISLAM kwenye UPUMBAVU wenu. Jikemeeni wajinga wenyewe
Wewe ni mpumbavu.

Hujui kujenga hoja una leta mihemko yako na hasira za itikadi kali za dini yako...

Nyie ndio mazwazwa mleta mada kafafanua kwa nia nzuri..

Una pachika itikadi zako za udini.
 
Hakuna kanisa linalosajiliwa kibinafsi, makanisa yote yanasajiliwa kama taasisi au shirika.
Mkuu. Mimi ni mkristo wa madhehebu ya kilokole kwa miaka zaidi ya ishirini. Hapo nilipokazia ni tatizo kubwa. Nayajua mengi pia khs hilo. Kuna makanisa mengine (huduma) ni mali za watu binafsi. Utawatambuaje: 1. Wao ndio alfa na omega. 2. Hakuna uchaguzi wa askofu wala... 3. Akifa yeye mkewe au watoto wanaweza kuchukua nafasi. Yapo mengi ndg acha tu.
 
Siungi mkono hoja yako Yericko. Kwa ufupi tu:-
1. Uchambuzi wako na ujenzi wako ni bias and subjection.

2. Dini zote zinazosimamiwa na Mashirika ya Ujusasi are merely "opium of the masses ". Hizo imani (mfano hao Orthodox Churches are traditionally puppets or instruments of Communism aggression).

Na pia hayo madhehebu ya aina hiyo kusambazwa na vyombo vya husika kwa malengo yao maalum - Mwenyezi Mungu huwa hayupo kwenye hizo dini/madhehebu. Je! hilo hulijui?

3. Kosa/jinai aina hiyo halihalalishi blanket assumptions ulizoziita "solutions"......

4. BTW, What if hao "mbweha" wa usalama wametengeneza au kuruhusu tukio kwa malengo yao? Vipi kama wameshiriki vipande vya hiyo "drama"?
After all, most cults are developed and spread by them, natumai hilo unalitambua.

Mwisho, niwape pole wafiwa wote.
Hao wahalifu wote wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria sambamba na uchunguzi wa kina ufanywe.
 
Nasikiliza radio toka Ngomeni kwa Kuhani Musa
"..... kufa kufa,
kufa kufaaa akate moto .. kufa kufaaa"
Ndivyo Yesu alivyo fundisha? [emoji848]
Nimejikuta nacheka kama mwehu

Dunia ya mwisho hii, imejaa maajabu kama sio mastaajabu
 
Back
Top Bottom