Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Kuna mjinga Mmoja anadai eti hata akiwa shoga hivyo ndivyo mungu ametaka awe ..na nimhubiri sijui nabii eee jamani ukristo umekuwa kituko..sema hatusomi vitabu wandishi wengi wameongelea utapeli wa viongozi wa dini,mfano mzuri ni Wole Soyinka ktk tamthilia "The Trials of Brother Jero"mhusika mkuu Jeroboam (brother Jero) anawaita waumini wake kwa Siri eti my costumers, wateja wake.ni wakati Sasa serikali kuhakikisha Kila anaefungua kanisa awe ni vigezo ikiwemo elimu ya chuo kikuu ili kudhibiti hawa wahuni
Ndo maana kanisa lake limefungiwa Asap, mnafikri serikali haioni na kuchukua hatua?
 
Kwa Jiji la Mbeya hii ni aibu sana sana!kila kona kuna kanisa na mengine hayana usajili na Mamlaka zipo!

Mbunge wa Iringa jana kaongea Bungeni kuwa watu wetu hawana afya ya akili "utakuta Mama ndani ya pochi lake kabeba maji ya upako,chumvi ya baraka,mara kitambaa cha bahati..." Hizi ni dalili za watanzania wengi hawana afya ya akili,Jesca Mtavambangu Mbunge wa Iringa anasema!

Wakati haya yanatokea Mtume Mwamposa pale Mbeya maeneo ya Ifisi kama unaelekea Songwe Airport kajenga Bonge la Hotel yake binafsi!Wizi huu kwa masikini haukubaliki!

Naunga mkono hoja sana!
Jesca anaongea nn wakati ye mwenyewe ana kanisa hapa?
Aisee🤔
 
Miongoni mwa waumini wa kanisa la mchungaji Paul Makenzie wa nchini Kenya 🇰🇪 waliookolewa walipokuwa porini kwenye maombi ya kufunga ili kuonana na Yesu.

Ila pamoja na kuokolewa bado hawataki kula, wameshikilia msimamo wao wa kuendelea kufunga mpaka kufa ili wakakutane Yesu.

Hadi sasa waliokutwa wamezikwa baada ya kufariki wamefika watu 79 ambao tayari miili yao imefukuliwa na zoezi la uokozi bado linaendelea.
 
Attachments

  • CamScanner 04-26-2023 16.12_1.jpg
    CamScanner 04-26-2023 16.12_1.jpg
    67.6 KB · Views: 2
  • IMG-20230426-WA0002.jpg
    IMG-20230426-WA0002.jpg
    58.8 KB · Views: 2
"NINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU".

Kama wa moto awe moto sio wavuguvugu, hii mada haikupaswa kuingizwa hata neno Uislam.

Miaka mingi sana, sisi tulikemea haya makanisa yasiyo na mbele wala nyumba hasa matapeli kutoka MBEYA, IRINGA, ARUSHA hayo maeneo yana wapumbavu wengi sana.
mkuu,si vyema kujumuisha hukumu kwa kundi au kanda kwani kwa wasiyo
usika ni ubaguzi
 
Siyo kila cha Kenya kinatuhusu nasisi!! Mbona mnapenda kushobokea mambo ya Kenya alafu mazuri hatujitabirii bali mabaya!!! Ufala huu mtauacha lini Nyerere feki
 
Tanzania iwe makini na mhuni mmoja anayeuza mafuta chumvi na unga wa upako. Mwamposa, Lusekelo, Geor Devie wa Nguvumo ya upako, suguye wa kutaka watu walete nywele za utosi, mbarikiwa wa Mbeya aliyewachanganya vijana wanaonekana kama wanavuta bangi, na wengine wanaofanana na hao.

pia, sheria iwekwe, kama mtu anauza mafuta, keki na maji, atoe kodi. na aeleze yeye ni mhudumu wa injili au ni mfanya biashara. mwamposa ameuza mafuta hadi kajenga hotel mbalizi mbeya. tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
 
Mi nina mdogo wangu mke wake wa ndoa amehama nyumbani kwake, ameenda kwenye kachumba ka kupanga eti wanakesha na watumishi wakiomba na kuabudu, mpaka ndoa imeshatetereka, hasikii cha ndugu, Mume, wala watoto wake, kila kitu mpaka amsikilize "Nabii" kwanza atakachompangia!! Amekonda kama mtoto mdogo, anakesha bila kula vizuri, hapati usingizi, hela zote anapeleka fungu la kumi kwa nabii, yaani inasikitisha , Serikali kuna haja ya kuwafuatilia hawa manabii , nadhani wengi ni wachawi tu
😁
 
Kuna ombwe la kiroho kwenye hizi dini kubwa ambalo linajazwa na hawa wafia dini matapeli.

“Asili haivumilii ombwe”!

Lakini suluhisho sio udhibiti wa dola isipokuwa tu pale sheria za nchi zinapovunjwa ambapo upelelezi wa kawaida wa kipolisi unapaswa kuhusika na hata idara ya usalama wa taifa kama ikibidi.

Kwa haya yaliyotokea Kenya na Uganda kwa uchache, bila kumsahau Mwamposa na mafuta yake hapo Moshi, Jeshi la polisi linatakiwa kuwa na kitengo cha makosa ya jinai ya kidini(religous crimes) cha uhakika, kama bado hakipo.

Ila hizi oganaizesheni kubwa za kidini hasa makanisa ya kikiristo, zinapaswa kujitathmini na kujitafakari kuwa mvuto wao, hasa kwa vijana, ni wapi umepotelea.

Zote zimepungua.
 
Mimi ni secular-theist.
Siamini sana katika dini, lakini nikienda mbele na kurudi nyuma I have some respect kwa makanisa ya kilokole. Pia respect kwa wasabato kuliko madhehebu mengine ya kikristo. Hali kadhalika kwa waislam.
Mchango wangu!
Makanisa ya kilokole ndio chanzo cha tatizo linalojadiliwa.
Hivyo, wewe ni muhanga wa fikra hatarishi za kilokole.
 
Ngoja tu mwamposa atasema siku Moja tujimalizeni watu wanajimaliza tupo hapa hapa
 
Hata hilo Kanisa katoliki linaonekana la kweli kwa wakatoliki wenyewe ila sio kwa Wasabato, walokole, mashahidi wa Yehova n.k
Suala siyo kuwa wakweli.
Suala ni halielekezi watu kuingia katika utapeli wa kiroho. Hii inajumuisha kudhuru afya na uchumi wa watu( Mfano: kumwambia mtu auze kila kitu Kisha atoe sadaka). Hao uliowataja ni makundi yaliyoanzishwa kwa ajili ya kupingana na kanisa katoliki( protestants).
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Nashauri Kila kanisa lihakikishe mafundisho yake yanatoka kwenye Biblia.Hakuna kufanya jambo lolote hadi utoe ushahidi wa kimaandiko.Ninaposema Biblia namaanisha ile yenye vitabu 66.Sio kipande cha Biblia (agano jipya).Serikali ingezingatia hili hata hiyo ya kukanyaga mafuta isingetokea
 
Hizo dini kubwa zinazojinasibu ni safi ni hopeless kabisa ndio maana waumini wao wanakimbilia kwenda kwingine kulishwa matango pori kuliko kusalia huko
 
Tukio la watu kukanyagana na kfa pale Moshi, majasusi walikuwa likizo?
 
Back
Top Bottom