Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Sawa.
Ila kuna sehemu umenikosea sana.
Kwamba kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kudhibiti mwenendo wa ukuaji wa kiroho!
Usijifanye unafahamu kila kitu, pengine ni kiburI cha uzima.

On the other hand, upo sahihi kabisa kuwa makanisa fulani na misikiti fulani haipo kwa ajili ya kumwabudu Mungu.
IPO KIBIASHARA au KUMUASI MUNGU.
 
Tatio hapa ni ujinga na umaskini na kukata tamaa kwa watu wetu walio wengi. Si Kenya tu, hata Tanzania wapo sema hawajauawa kimwili. Wanaibiwa kila siku kwa kuombewa upuuzi. Wanawatajirisha matapeli huku wao wakiendelea kuwa maskini. Hapa wa kulaumiwa siyo criminal Mackenzie bali serikali ya Kenya kwa kumwachia akafanya alivyotaka. Kuna tofauti gani kati yake na akina Gwajima, Mwakasege, Mzee wa Upako, na wengine wengi bila kumsahau Kakobe wanaliotajirika kwa kuwaibia wajinga na watu waliokwisha kata tamaa? Hawa ni wa kuchomwa moto kuliko hata vibaka. Hata hivyo, serikali haziwezi kuwaona kama ni tatizo kwa vile wote wanafanya kazi aina moja sema kwa staili tofauti. Muangalie tapeli Ruto anavyokenua kana kwamba waliokufa ni panya. Huyu hana tofauti na Mackenzie. Nakubaliana na Ruto kuwa huu ni ugaidi sawa na wale wanaojilipua au kuwalipua wenzao au wanasiasa wanaodanganya wananchi na kuishia kuwaibia
Kwa maoni yangu, Mwakasege mtoe kwenye kundi la akina Gwajima.
 
Mackenzie anasema alishafunga kanisa lake mwaka 2019.

Na anasema toka mwaka huo hajawahi kuhubiri, na anasema huku shambani kwake ambako alirithi hill shamba la familia alikuwa haendi kila wakati na hata kama alienda hafiki ktk shamba lote lenye heka 800.

Anasema hakujenga nyumba wala kizuizi iweje watu wafunge hadi kufa na hakuwafungia ndani ?

Anasema kuna watu waliwaingiza watu shambani kwake waka waua bila yeye kufahamu.
Yeye hajawahi kuwa Mchungaji toka mwaka 2019. Na Kanisa lake alifunga na lipo tu amegeuza godauni.
Anavyo ongea tena bila wasiwasi utajua kuwa wanamwonea.

Ila kwakuwa wapo walionusurika tena wamakonde sana wanasema ukweli ni nani aliwashawishi.
 
Nilichojifunza ni kuwa watu wanampenda sana Yesu Kristo. Wako radhi kufa njaa ili waonane Naye.

Ewe Kristo tupe ujasiri wanafunzi wako
Tunauwawa na Machungaji feki.

Tunauwawa na Waislamu Mujahidina.

Tunauwawa na ndugu zako Wayahudi.

Tunauwawa na kila muumini wa Ibirisi Shetani.

Tunauwawa na kila jamii

Lakini tunafuraha kwakuwa tunakujua wewe u nani.
 
Akhy relax....

Narudia tena...sidhani kama Yericko ameshambulia wanadini wote....na sidhani pia wewe unaamini kuwa ni "wakristo wote" ndio wako hivyo....kama sivyo basi utakuwa na fikra za "attacking others,prejudice,argumentum ad hominem and generalization" ndani ya bandiko hili la kujenga taifa bora zaidi.......

#SiempreJMT
Hawezi kukuelewa mkuu
SI kila bandiko lazima lieleweke kwa kila memba
 
Mackenzie anasema alishafunga kanisa lake mwaka 2019.

Na anasema toka mwaka huo hajawahi kuhubiri, na anasema huku shambani kwake ambako alirithi hill shamba la familia alikuwa haendi kila wakati na hata kama alienda hafiki ktk shamba lote lenye heka 800.

Anasema hakujenga nyumba wala kizuizi iweje watu wafunge hadi kufa na hakuwafungia ndani ?

Anasema kuna watu waliwaingiza watu shambani kwake waka waua bila yeye kufahamu.
Yeye hajawahi kuwa Mchungaji toka mwaka 2019. Na Kanisa lake alifunga na lipo tu amegeuza godauni.
Anavyo ongea tena bila wasiwasi utajua kuwa wanamwonea.

Ila kwakuwa wapo walionusurika tena wamakonde sana wanasema ukweli ni nani aliwashawishi.
Kuna survivor mmoja alikuwa anahojiwa na KTN News anasema fastening ilikuwa voluntary na hakuna aliyelazimishwa. Amehitimisha Pastor Mackenzie hatakiwi kulaumiwa kwa hiyo massacre.
 
Waislam kila siku wanavaa MABOMU kulipua wasio na makosa kisa tu kwenda peponi........
@ozark ulishawai ona hapa tz Kuna muislamu kajilipua na bomu??????

Hizo ni propaganda mzeee acha kufikiria kupitia makalio

Hizo ni western propaganda ili kuonyesha kwa mbuzi kama nyie kuwa uislamu haufai
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Idara za usalama zinaegemea zaidi kwenye kulinda nafasi za madaraka ya kisiasa badala ya usalama wa taifa (wananchi).
Mtazamo huu finyu husababisha idara hizo kushirikiana na kusaidia manabii wa uongo kuwadhibiti raia kwa faida ya wanasiasa (wachache).
Manabii wa uongo na wanasiasa walio madarakani, kwa kujua au kutokujua wanaweza kuwa maadui wa taifa wanaosaidiwa na idara za usalama.
 
Natamani hapa kwetu bongo wadondoke kama buku hivi, maana sikio la kufa halisikii dawa
 
@ozark ulishawai ona hapa tz Kuna muislamu kajilipua na bomu??????

Hizo ni propaganda mzeee acha kufikiria kupitia makalio

Hizo ni western propaganda ili kuonyesha kwa mbuzi kama nyie kuwa uislamu haufai
Muhammed Ghailan ililipua Ubarozi wa Marekani, Watanzania kadhaa walifariki.
Wengine walijihusisha na mauaji ya Kibiti.
 
Hao wakenya ni kikundi kidogo sana, yamewakuta ya kuwakuta na imekuwa study case. Duniani kuna dini za kipuuzi zenye wafuasi wengi kama nzige zina mambo ya ajabu, kwa kuwa hayajawafika mabaya sio ishu kuzungumziwa ila nako kuna upuuzi mwingi tu huko. Tuombe Mungu aepushe balaa jingine baya tusije kuandika yatakayotokea kwa ujinga huu huu wa kuaminishwa ujinga. Maana kuna kitu huwa wanakifanya ni cha hatari wasipochukua tahadhari kitawagharimu maisha yao
Kipi hicho, kufunga Ramadhan?

Hahahahahahahaha

We Islamophobe usitake kuchekesha watu.

Halafu si nilishakuambia useme wazi tu. Usifunge funge
 
Muhammed Ghailan ililipua Ubarozi wa Marekani, Watanzania kadhaa walifariki.
Wengine walijihusisha na mauaji ya Kibiti.
@Che mittoga kajilipua au kalipua?? Ulimuoana????

Wamarekani sio WA kuwaamini na ww acha mambo ya upinde ??? Washatoa statement mara ngapi hapa nchini za ugaidi?? Ushawai tokea huo ugaidi.? Hao ni mtu wao wamemituma wenyewe.
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Mimi nakubali andiko lako, uko vizuri. Lakini ukiona serikali iko kimya, kuna namna walio madarakani wanavyofaidika. Nashauri wasomaji wafuatilie stories ya GOLD MAFIA vizuri. Utauona ushiriki wa Uebert Angel [emoji116]

Balozi wa juu wa Zimbabwe anayehusika katika mpango wa magendo ya dhahabu

Huyu ni mteule wa Rais Mnangangwa. Lakini angalia mambo anayofanya.

Kwa hiyo, ukiona hawa manabii wananyamaziwa, au wanapewa hata teuzi na nafasi za kisiasa, chunga sana, kuna namna.

Kanisa na waumini wao, wanatumika kama 'smoke screen '. Ili kutuzuga sisi wengine tusijue mambo mazito yanayoendelea.
 
Mimi nimependa ulivyosema "mtu mwenye msongo wa mawazo anaaambiwa anamapepo"
 
@Che mittoga kajilipua au kalipua?? Ulimuoana????

Wamarekani sio WA kuwaamini na ww acha mambo ya upinde ??? Washatoa statement mara ngapi hapa nchini za ugaidi?? Ushawai tokea huo ugaidi.? Hao ni mtu wao wamemituma wenyewe.
Serikali ya Tanzania ilijiridhisha kuwa alifanya huo uhalifu, alikabidhiwa kwa Serikali ya Marekani ili akajibu mashaka yake.

Kwenye kesi yake ndugu zake walihudhuria na kushuhudia Mahakama ikimtia hatiani kwa ushahidi uliokamilika.

Katika tukio la Garisa Kenya kuna Mtanzania mwingine alikamatwa akishirikiana na Al-Shababu kuua wanafunzi wa Dini flani.

Wahalifu wapo katika kila vikundi vya jamii zetu.
 
Maneno unayotoa kwenye gazeti la sun au nipashe.
 
Back
Top Bottom