Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Hujawahi kusikia visa vya ulawati RC katika nchi mbalimbali hadi Papa analazimika kuzungumzia?
Ulawiti uko Kila corner na Sheria Kali huchukuliwa pia kuwepo ulawiti haihalalishi mambo ya kijinga yaruhusiwe kuendelea
 
Haya makanisa makubwa yanatumika zaidi kisiasa nayo.
Heri kisiasa kuliko kina mwamposa kudhulumu na kudaganya raia maskini huku wao wakitajirika imagine watu wanaumwa magonjwa yanayohitaji tiba ya hospital yeye anawadaganya kukanyaga mafuta na kupona. So hyo ya siasa ni minor case
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Kichwa kikubwa Yericko. Mhehe mwenye akili
 
Mi naombea wale wa mwamposa aje awalishe sumu kwenye zile keki
 
Kuna manabii wameibuka na hapa TZ kuwajaza watu ujinga na kuwapora watu pesa zao, unakuta kanisani Nabii anaheshimika kuliko mume nyumbani, yaani Nabii anachomuambia mkeo huko kanisani ndicho hicho hicho atafanya akirudi nyumbani.

Wanawake ni kundi lilolo kwenye risk kubwa katika haya makanisa ya kisasa, ndoa nyingi tunaona zinavurugika sababu ya hawa manabii uchwara, tusipokuwa makini tutashuhudia makubwa zaidi ya hayo ya Kenya.
 
Kagame ni mtu next level yule kwanza tu anavo deal na wahuni huko Rwanda ndio maana ana majasusi Hadi nje ya nchi yaliyomkomesha yule general aliyekimbia na kuuliwa south Africa so sio wa mchezo mchezo kabisa. Kuhusu Hawa wakujiita manabii uchwara kawakomesha hasa Tena sio degree ya theology tu wawe kwanza na bachelor nyingine na ndio iwe hyo ya theology.

Pia ugumu wa maisha Sasa hivi watu wanakimbilia kuanzisha hizo huduma na kwenda kutafta uganga wakutabiria watu na kupiga hela za maskini na desperate wa maisha [emoji28][emoji28] Sasa huyo jamaa ako mnaogida pombe eti naye kaanza kuwa mtume soon atajiita nabii alienda Nigeria akirudi atakusanya nyomi la watu wenye shida mbalimbali. Hata. Huyo mwamposa anawadaganya wajinga huku yeye akila na Malaya na wengine kuwajengea ma gorofa na kuwazalisha michepuko huku akiwadaganya wajinga wapande mbegu ili wapone huku yeye akitajirika na ku enjoy na michepuko.

Pia na serikali ipunguze umaskini Kwa raia iweke mazingira rafiki ya kuajiriwa na kujiajiri maana ugumu wa maisha unawafanya watu wafikirie kutafta msaada kimiujiza.
Pia kupitia wizara ya maendeleo ya jamii itoe elimu Kwa wanawake ya kujitambua na kujielewa maana wengine ni single mothers wamezalushwa na wanaume tofauti tofauti na kukimbiwa Sasa ule mzigo wa kulea wanakuwa chambo Kwa manabii eti wanaume wawarudie au kuolewa. In short serikali iboreshe elimu na mambo ya kazi
[emoji2956][emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ukweni nilikoowa najulikana kama "mmiliki wa pesa za misukule" baada ya kumnyima mkopo shemeji yangu wa kike,na bora hata hizo hela ningekuwa nazo basi hela zenyewe sina na hii yote ni baada ya kuambiwa na huyo fake priest kwamba ameoteshwa kuna mtu ameandaliwa atamkopesha pesa.

Kuja kwangu akaniambia anataka nimkopeshe 1mill mtaji wa biashara kosa langu ni mimi kumuuliza je hiyo biashara unayotaka kwenda kuanzisha umejipanga wewe binafsi na shilling ngapi?akaniambia hana chochote nikamwambia nipe mchanganuo wa hiyo biashara kutulia na hesabu zangu nikaona hata nikimpa hiyo hela na biashara anayosema anaenda kuianza ni sawa na kuipoteza maana angetoa mahitaji ya msingi kama maandalizi angebaki na cash mtaji kama 200,000/= tu nikamwambia hujanishawishi ndiyo kurudi kwa huyo kuhani akamwambia yule hela zake alijua akikupa wewe nikiziombea misukule wake watakosa nguvu.

Hovyo sana hawa watu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.
Tanzania jambo pekee tunalofanya kwa uhakika na kwa uimara ni Uchaguzi tu ili CCM iendelee kubaki madarakani.
 
Ndugu yangu CARDLESS kuna ukweli kausema. Huu uzi ujadiliwe bila kuuhusisha Uislam kujifanya mna balance.

Mbona zikija mada za ugaidi na matukio ya kigaidi yanayohusisha Waislam huwa zinajadiliwa kwa kuwahusisha Waislam peke yake? Hakuna balance yoyote. Huyu Yeriko mfano akichambua kuhusu Ugaidi unaohusishwa Waislam unadhani atawataja LRA, KKK, Babbar Khalsa, nk, ili a balance? Sidhani.

Ukweli ni kwamba matukio kama lile la Kenya huyasikii katika Uislam na inajulikana ni watu gani wana hilo tatizo. Sio sawa kufananisha hali mbili zisizofanana ili kujifanya analeta balance. Kushamiri kwa ibada za kiislam ambazo zinajulikana kabisa na misikiti ikaongezeka sio tatizo.
Anachokifanya Yericko Nyerere ni kutaka kubalance story, hao waislamu wanaokwenda huko alshabaab n.k ni extremists ambao wanapigwa vita na uislamu dunia nzima wala hukuti waislamu wamefungiwa ndani eti wapo kwenye swaumu ili kumuona mtume muhammad alayhi sswalaatu wa ssalaam.

Tunachokisema dini kukosa mwongozo na kukosa wasimamizi matokeo yake ndio haya kila mtu ni nabii na mtume na analeta mafundisho kulingana na atakavyoamka siku hiyo, jambo la ajabu kabisa wasituhusishe kwenye mambo yao kwa kweli.
 
Mkuu kuna kitu hujakijua bado. Hakuna Mtumishi awe feki au original Tz anaweza kukuja huduma yake bila kuwa na Mkono Mrefu wa CCM
Hakuna.

hawa wapuuzi wanajua entrence nzuri ili wasibughudhiwe.

Nabii Tito alikuwa akiongoza ibada amevaa sale za CCM
Kuna linkage kubwa kati ya Imani potofu na wanabii wa uongo na cxm kwa hapa Tanzania. So uisdhani kuwa hawajui. Au kwamba wameshindwa. La HASHA!


UZI BORA WA MWAKA.

HII INAONYESHA TISS KUWA DHAIFU NA SABABU KUU NI NAMNA YA KU-RECRUIT HAO VIJANA.

TISS MKO WAPI KATIKA UJASUSI WA KIUCHUMI,UJASUSI WA KIDINI,


KAMA MNAPIGA KAZI KAMA ILIVYO KADA YENU KIMYAKIMYA ILA KWENYE SWALA LA DINI MMEFELI

KUNA TAPELI MMOJA ANASEMA ETI WAENDE NA KUCHA NA NYWELE WAOMBEWE

SHIT
 
Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi.
Kwa hiyo serikali iwe na dini yake?!!!
 
Back
Top Bottom