Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Stress tu za maisha watu wanapagawa. Serikali iwekeze kwenye kilimo kwa kutoa ruzuku za pembejeo, ishuke gharama ya chakula. Watu wawe na akili Timamu
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Wahuni wahuni tu 🤣🤣
 
Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa

19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA MADHEHEBU HAYA MAWILI



Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha ktk utumishi kwa dini na jamii kwani yeye ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni na Shia yanayo shambuliana kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao.

Amewataja Sheikh Mziwanda na Samir wa upande wa Sunni huku upande wa madhehebu ya Shia kupitia Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Abdul na wenzie watatu wakijitetea.

Na pande hizi mbili za madhehebu haya yakinukuu kile wanachoamini kwamba ni sawa kwa upande wa madhehebu yao.

Pande hizo zimewekuwa zikirushiana maneno yanayotishia amani za kila aina mfano amani ya viungo, amani ya roho, kuvunjiana heshima n.k huku wote wa pande hizi mbili wakiwa na wafuasi wao hivyo kutishia amani kwa ujumla ya Tanzania maana wafuasi wa pande hizi mbili zinaweza kukabiliana kutetea pande zao na viongozi wao .

Mfumo wa uendeshaji wa mijadala hii imeleta ukakasi mkubwa huku maneno ya kutishiana uhai baina ya pande hizo yakitamkwa asema Sheikh Abuu Iddi kwa masikitiko makubwa.

Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......

Soma zaidi : source : Sheikh Abuu: Tujihadhari, amani inaweza kuvunjika kupitia mijadala ya kimadhehebu inayoendelea
 
Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Umeongea nukta (point) kubwa hapa .
 
Toka maktaba:

Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Mambo yanaendelea naona pastor ezekiel wa kenya nae kakamatwa Kuhusishwa na ishu hio. Uenda hawa mapasta wanafanya biashara za viungo vya binadamu. Pasta ezekiel yupo kwenye list ya watumishi wa uongo ya east africa huku wa Tanzania wakiongoza.
 
Kwa hiyo kumwabudu Muumba mbingu na nchi ndio kufanya haya ya:-
1)Kibwetere,Mc Kenzie?
2)Ugaidi kule Kibiti Rufiji ,Mapango ya Amboni ,Garissa ,Cabo Delgado n.k?
3)Kuchonganisha jamii kwa "ramli" zinazopigwa ndani ya baadhi ya nyumba za ibada?
4)Kufufua wafu ,kuwaletea watu utajiri na mafanikio,kuwatoza wenye shida mapesa mengi?
5)Kujenga mahekalu na kuishi kikwasi kama wafanyavyo baadhi ya watu?

RiP the late father of our nation ,El Comandante JKN you said well that enemies of the nation among them is IGNORANCE[emoji120]

#SiempreURT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Umejibu vema. Haya yote uliyoaandika mwasisi wake ni shetani si Mungu. Nikuambie tu ndugu yangu mwenye huu ulimwengu ni shetani. jiulize tu kwamba mbona mambo ya gay yankuwa na nguvu sana. Kwa sababu mwanzilishi ni shetani ili kuharibu kizazi hiki. Ndugu yangu tuko hatarini sana huko mbele ni giza. Tumwombe Mungu atuepushe na yatakayoikumba hii dunia. Kuna siku itachomwa moto.
 
26 August 2019
NEWLIFE PRAYER CENTRE & CHURCH - Ev. Ezekiel Odero - Deliverance And Healing Service


Source: New Life TV KENYA

27 April 2023
Maafisa wa DCI wamkamata pasta Ezekiel Odero.


1682765013998.png


28 April 2023

'Pasta’ Ezekiel Odero Alipanga Kuenda Tanzania Aliponaswa – Polisi



NA WINNIE ATIENO mwandishi gazeti la TaifaLeo


MAMIA ya waumini wa dhehebu linaloongozwa na mhubiri Ezekiel Odero, jana Alhamisi walitakiwa kuandikisha taarifa kwa polisi baada ya mhubiri huyo kukamatwa.


Makachero walimnasa Bw Odero katika nyumba yake ya kifahari iliyo Mavueni, Kaunti ya Kilifi, huku duru zikisema alikuwa akijiandaa kusafiri kuenda Tanzania.

Wakati akipelekwa kituo cha polisi huku maafisa wakiondoa waumini kanisani, mkewe, Bi Sarah, alikuwa akiendelea kupeperusha mahubiri kupitia mitandao akiondolea waumini wasiwasi.

Mmoja wa wahubiri alidai kuwa walikuwa wanapanga mahubiri ya hadhara jijini Dodoma, Tanzania kuanzia leo.

“Hatuna uhakika kama alikuwa anahepa kukamatwa au alikuwa akienda kwa mkutano wa mahubiri ya hadhara ilivyodaiwa kwa sababu hatujaona matangazo yoyote ya mkutano huo unaodaiwa kuwepo Tanzania,” afisa anayefahamu kuhusu uchunguzi unaoendelea, aliambia Taifa Leo.

Awali Jumanne, maafisa wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) wa Kilifi walikuwa wamemhoji mhubiri huyo maarufu ili kubainisha uhusiano wake na mhubiri Paul Mackenzie, ambaye yuko kizuizini kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya halaiki ya waumini aliowashawishi kufunga kula na kunywa ili waende mbinguni.

Afisa Mratibu wa Ukanda wa Pwani, Bi Rhoda Onyancha, alisema Bw Odero alikamatwa jana Alhamisi kuhusiana na vifo vinavyodaiwa kutokea katika kiwanja chake cha ekari 65, ambacho kimejengwa kanisa, vyumba vya kukodishia waumini wanaowasili kutoka pembe tofauti za nchi, shule, na majengo mengineyo.

“Tumechukua hatua pia ya kufunga kituo chake cha maombi. Tunafahamisha umma kwamba kituo hicho cha maombi kimefungwa na yeyote aliyekuwa hapo ameondolewa. Tutawapa habari zaidi tunapoendelea na uchunguzi,” akasema Bi Onyancha.

Kupitia kwa taarifa, Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki, alisema zaidi ya waumini 100 waliopatikana katika kituo hicho cha Mavueni watatakiwa kuandikisha taarifa kwa polisi.

Bw Odero, ambaye alikuwa ameandamana na wakili wake, Bw Jared Magolo, aliwasili kwa gari lake la kifahari linalokadiriwa kugharimu takriban Sh17 milioni huku akibeba Biblia.

Wakili huyo alimtetea mteja wake akisema, haikuwa haki polisi kuzingira nyumba yake ya kibinafsi alfajiri wakitaka kumkamata.

“Polisi wanafanya uchunguzi, watatueleza wanachotaka punde wakimaliza uchunguzi wao. Kwa sasa hakuna sababu ya kumzuilia,” akasema.

Mhubiri huyo huwa na ufuasi mkubwa nchini na Afrika Mashariki, ambapo baadhi ya waumini wake ni vigogo wa kisiasa na wandani wao.

Bw Odero alizaliwa katika Kisiwa cha Rusinga, Suba, Kaunti ya Homa Bay, kwa familia anayotaja kuwa maskini. Alisafiri hadi Mombasa baada ya kumaliza Shule ya Upili kutafuta riziki. Ameishi Pwani kwa takriban miaka 21 sasa.

Alijiunga na Kanisa la Maximum Miracle Centre na kuokoka mnamo Desemba 2001. Ana mke, ambaye pia ni mhubiri, Bi Sarah, na wana watoto watatu
 
Umejibu vema. Haya yote uliyoaandika mwasisi wake ni shetani si Mungu. Nikuambie tu ndugu yangu mwenye huu ulimwengu ni shetani. jiulize tu kwamba mbona mambo ya gay yankuwa na nguvu sana. Kwa sababu mwanzilishi ni shetani ili kuharibu kizazi hiki. Ndugu yangu tuko hatarini sana huko mbele ni giza. Tumwombe Mungu atuepushe na yatakayoikumba hii dunia. Kuna siku itachomwa moto.
Hakika mkuu....

Aaamin aaaamin[emoji120]

Maombi yako ayapokee Muuumba mbingu na nchi ,aaamin[emoji120]

#DoNoTDoHarm
#YetzerHatov[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom