Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
unataka kusema waislamu hamna madhehebu?
 
Mambo ya kiimani ni magumu Sana kudili nayo. Nadhani idara ingeanza kuthibiti waganga kwanza hawa ni worse zaidi kuliko hata hao mitume na manabii.
Waganga ndio uwapa nguvu majambazi, wezi na vibaka kudhuru na kuua.
Ndio wanawapa dawa michepuko kusambaratisha ndoa za watu watoto wanateseka kukosa malezi,
Ndio wanawapotosha wanasiasa.
 
Hapo sasa ndipo lawama zote kwa TISS na mamlaka. Hivi kweli mpumbavu mmoja anayejiita yesu wa tongareni sijui anaweza kuachwa na mamlaka kufanya upumbavu ulie? Kesho wakiskia amewazika watu kadhaa baada ya kuwaua tutashangaa nini.
Hapo ni ishu ya ufahamu wa maandiko,anaejua maandiko hawezi angaika na Yesu wa Tongaren,bali atahangika na Yesu wa Nazareth.
 
"NINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU".

Kama wa moto awe moto sio wavuguvugu, hii mada haikupaswa kuingizwa hata neno Uislam.

Miaka mingi sana, sisi tulikemea haya makanisa yasiyo na mbele wala nyumba hasa matapeli kutoka MBEYA, IRINGA, ARUSHA hayo maeneo yana wapumbavu wengi sana.
Haya ni lazima yatokee yasingetokea biblia Ingekuwa ni kitabu cha uongo.
Maandiko yanasema ukiyaona haya ni moja ya dalili za kiama.
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Mwamposa dahh.... tapeli huyu atakuja fanza ya ajabu.
 
Mi nina mdogo wangu mke wake wa ndoa amehama nyumbani kwake, ameenda kwenye kachumba ka kupanga eti wanakesha na watumishi wakiomba na kuabudu, mpaka ndoa imeshatetereka, hasikii cha ndugu, Mume, wala watoto wake, kila kitu mpaka amsikilize "Nabii" kwanza atakachompangia!! Amekonda kama mtoto mdogo, anakesha bila kula vizuri, hapati usingizi, hela zote anapeleka fungu la kumi kwa nabii, yaani inasikitisha , Serikali kuna haja ya kuwafuatilia hawa manabii , nadhani wengi ni wachawi tu
Una uhakika hana bwana huko kwa nabii
 
Mambo ya kiimani ni magumu Sana kudili nayo. Nadhani idara ingeanza kuthibiti waganga kwanza hawa ni worse zaidi kuliko hata hao mitume na manabii.
Waganga ndio uwapa nguvu majambazi, wezi na vibaka kudhuru na kuua.
Ndio wanawapa dawa michepuko kusambaratisha ndoa za watu watoto wanateseka kukosa malezi,
Ndio wanawapotosha wanasiasa.
Waganga huwezi kuwadhibiti; serikali iliamua kuwasajili ili kupata kodi tu.
Kiutendaji mganga/ mchawi hahitaji kibali kufanya kazi yake,, wewe unaenda kumtembelea binafsi mnafanya mazungumzo anakupa unachohitaji nawe unampa anachohitaji.

Usisahau mwanasiasa inapofika uchaguzi anaenda kwa mganga huyo huyo kuomba .msaada wa kumshinda hasimu wake sasa akikikalia kiti amgeuke! Pia kila baada ya muda fulani huyo huyo mwenye madaraka anaenda kutazama upepo unavyokwenda kwa mganga ( kama kuna watu wanapanga ubaya dhidi yake) halafu eti amuandame mganga! Yeye hajitaki?
 
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2598934
Umeongea vyema kiongozi, mungu akuongezee maarifa ipo siku watayasikia na kuyafanyia kazi.
 
Haya Makanisa yamekuja kuchukua hata kile kidogo cha masikini kwa ufinyu wetu wa akili.

Maombezi ya usiku nayo imekuwa chanzo cha ndoa kuvunjika, watu wametoa dhana ya kuhangaika kutafuta pesa badala yake wanaaminishwa watatajirika kwa maombi.

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa."
 
Shida kubwa Iko kwenye haya makanisa ya kilokole ya watu binafsi kanisa kama RC hamna huo ujinga maana ni mfumo na mapadri wengi Wana shule, zamani kanisa common yalikuwa RC na KKkt hakukuwa na huu ujinga wa makanisa ya miujiza na unabii tangu yaongozeke na raia kuharibikiwa akili kumezidi plus ufikiri duni na uvivu wa kufikiri na kufanya kazi. I think serikali iwe strictly kuongeza vigezo Kwa makanisa na yawe regulated
 
Unachanganya vitu viwili, kuna kanisa yani Church na kuna huduma yani Ministries.

Shida ipo kwenye hizi ministry.
 
Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
Duh mbona umekuwa mkali hivyo na jazba juu!
 
"NINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU".

Kama wa moto awe moto sio wavuguvugu, hii mada haikupaswa kuingizwa hata neno Uislam.

Miaka mingi sana, sisi tulikemea haya makanisa yasiyo na mbele wala nyumba hasa matapeli kutoka MBEYA, IRINGA, ARUSHA hayo maeneo yana wapumbavu wengi sana.
Ila wewe una nongwa na unaharibu mada nzuri tu.
Utasababisha kuwatoa watu kwenye mada na kuanza kujadili ya kwako
 
UKITAFAKARI SANA JUU YA HILI UTAONA NI AFADHALI MADHEHEBU YETU PENDWA YAKAIMARISHWA NA HAYA MENGINE YA UPIGAJI YAKAFUTWA, TUKABAKIA NA LUTHERAN, CATHOLIC, ANGKIKAN AND SO LIKE NA SI HAYA YA UPAKO, THEY ARE FOR SPIRITUAL BUSINESS.
I agree with you zamani RC, KKKT Hali ilikuwa shwari ila haya makanisa mapya yanatumika ka waganga wa kienyeji na kuongeza matatizo ya akili Kwa watu wenye matatizo
 
Back
Top Bottom