Mkuu haya mambo sio ya kujadili juujuu tu.Ni saa ngapi mtu atatekwa tuamini na ni saa ngapi mtu atatekwa tupuuze wakati kuna waliotekwa na wakatoweka hadi leo hawajaonekana!
Nahisi ni hawa hawa watekaji ndio wanacheza na akili za watu wakitumia advantage ya serikali kutokufanya uchunguzi japo kwa serikali tukio lolote wanatakiwa kulichukulia seriously.
Kwa kuwa wanaotekwa ni watu wanaoonekana kuikosoa serikali hii inatufanya tuamini kuwa ni wao ndio washukiwa wakuu wa uhalifu huu.
Asante Sana kwa taarifa na hata ukanipa na Art ya katiba inayokataza maandamano bila kibali. Hoja yangu, nipe tena kifungu kilichokufanya tume ya uchaguzi kuwanyima mawakala wa Chadema barua za utambulisho kama wasimamizi siku ya kupiga kura. Na kama tume ilikataa kutoa barua, Chadema walitakiwa wafanye kitu gani au wafuate utaratibu upi tofauti na kuandamana. Kumbuka pia tukio lilitokea Tare 16/2 na uchaguzi ulifanyika Tare 17/2.Maandamano yalianza usiku (baada ya saa 12 jioni.) Kinyume cha sheria walizojiwekea wenyewe vyama vya siasa.
Maandamano hayakuwa na kibali cha polisi. Sheria ya kikatiba. Ibara ya 20(1) ya Katiba ya JMT ya 1977.
CDM walivunja sheria 2 pale. Ulitaka polisi wafanye nini?
Waandamanaji walikuwa na silaha za mawe. Polisi kadhaa walijeruhiwa.
Binafsi tangu yule dereva wa rip Chacha Wangwe aliyejulikana kwa jina la Malya alipoonekana akiwa katika msafara fulani akielekea Libya nimekuwa siwaamini kabisa baadhi ya vijana wa Chadema. Hapa najiuliza tu Nyani Ngabu alijuaje kuwa Nondo hajatekwa bali kajiteka?!!....Ngabu nijibu tafadhali maana haya mambo yanatuchanganya sana!
Lissu alijipiga risasi? Alphonce Mawazo alijiua kwa kujikata mwenyewe mapanga? Akwilina kajiua mwenyewe kwa kujipiga risasi? Diwani Luena kajiua mwenyewe kwa kujikata mapanga? Katibu wa Chadema kata ya Hananasifu alijiua mwenyewe?Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.
Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.
Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.
Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Ngabu huyu aliyekuwa anamshambulia mgombea wa CCM 2015 ni lini amehama Chadema?!!nyani siku hizi ni pro- government hawezi kuwa na ubiased view kuhusu tukio lolote linalohusisha tuhuma dhidi ya gov. anatumia zaidi mapenzi na hisia kuliko reasoning.
Halafu huyo mshikaji baadaye akaja kuonekana ni Mlinzi wa wakuu fulani.Kuna jamaa alitenguliwa uteuzi wake akamuandaa mshikaji wa kumtolea bastola akishuka kwenye gari kuelekea kwenye press conference aliyohadaa kuwepo kwake, kumbe ukiangalia kwa jicho la TATU , alipanga kujiteka ili shutuma ziende kwa mteuzi......courtesy of CCMizi
Alitekwa vipi wakati alionekana amejideula kwenye New Force!ww unajuaje kama alitekwa??