Yaliyojiri Uchaguzi Mkuu wa TLS Dkt. Edward Hosea na mwenzake wamwaga fulana kwa wajumbe

Laroi Butata

Member
Oct 28, 2020
91
103
Uchaguzi wa rais chama cha wanasheria Tanzania (TLS) unaofanyika jijini Arusha umeshika kasi kukiwa na wagombea watano ila nimeona watu kadhaa wakiwa wamevaa t-shirt nyeupe zikiwa na picha za wagombea tofauti mmojawapo akiwa ni Dr. Hosea na Shehzad Wall.

Sijajua kwa nini wagombea hawa wawili kati wa wote watano wamekuwa na kampeni ya namna hii, nilipokuwa napita maeneo ya Sanawari hapa jijini arusha kuelekea mjini nilipishana na watu waliovaa nguo hizo.

Nilijaribu kuuliza kujua kulikoni ndiposa nikaambiwa hao wawili mmoja ndiye mwenye nafasi na hasa Dk Edward Hose aliyewahi kuwa boss pale Takukuru.

Naambiwa kesho ndiyo kinyang'anyiro cha kupiga kura na kinafanyika hapa arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC.

Nimeuliza na kupata majina ya wagombea wote kama ifuatavyo, Dk Edward Hosea, Albert Msando, Flaviana Charles, Shehzad Wall na Rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stolla hawa ndiyo wanaosubiri kudra za wajumbe kesho.

IMG_20210415_224236.jpg

Pichani kushoto ni Dk. Hosea katikati Flaviana Charles na kulia ni Shehzad Wall, nimekosa picha za Albert na Francis.

Kwa kudra za Allah kesho nitawapa kinachojiri kama nitafanikiwa kufika eneo la tukio.

Alamsiki.



UPDATES:
Tayari mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais kwa mwaka 2021 ametangazwa ambaye ni dkt. Edward Hosea ambaye amepata jumla ya kura zote 297.

Zaidi, soma: Breaking News: - Dr. Edward Hosea ashinda urais wa Tanganyika law society (TLS) , apata kura 297
 
Mmmh, hivi hii kitu mwaka jana ilifanyika kweli?, maana kama ulikuwepo uchaguzi au mikanda ilibana watu wakapotezea kujua kwa undani.

Nakumbuka alipokuwa Fatuma Karume na mzee wa Ubelgiji 😁!.
 
kwa macho yangu ya makengeza na mm sio mwanasheria naona picha umezi badili kushoto ndio Dr Hosea na kulia ni Shehzad Wall
Mkuu nimefuta muelekeo wa ukaaji wa picha nikasahau muelekeo wa msomaji kuwa atafuata anavyosoma 😂!.
 
Mkuu nimeafuta muelekeo wa ukaaji wa picha nikasahau muelekeo wa msomaji kuwa atafuata anavyosoma 😂!.
umefuata jinsi picha inavyotutazama? mbona una access ya kurudi post# na kurekebisha pale mara moja kwa kuwa post ni yako. futa kulia andika kushoto
 
Huyo mgombea wa Kike Flaviana Charles Jana Clouds Tv habari wamempigia sana kampeni indirectly. Sijui kama hii inaruhusiwa

Bad eneough wagombea wengine waliobaki hawakutajwa hata mmoja
 
Ninaomba kufahamishwa...hivi TLS Luna Ulaji was aina Fulani hadi watu wanaelekeza nguvu huko ili ,kuchaguliwa??
 
Huyo mgombea wa Kike Flaviana Charles Jana Clouds Tv habari wamempigia sana kampeni indirectly. Sijui kama hii inaruhusiwa

Bad eneough wagombea wengine waliobaki hawakutajwa hata mmoja
Kwa ninavyofaham, siku ya jana ndiyo ilikuwa chance yao kupiga kampeni na kuomba kura, so alikuwa sahihi.
 
Huyo mama flaviana hafai, arudi tu kwenye NGO, hana uwezo wa kuongoza.
kwa nini amepania sana mpaka clouds wanamfanyia kampeni?
 
Back
Top Bottom