Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Hata mimi namsubiri Maggid Mjengwa na utabiri wake wa kinajimu.
Kachakacha
Hata mimi namsubiri Maggid Mjengwa na utabiri wake wa kinajimu.
Mlituona wajinga hapa wakati tunawajenga watu kisaikolojia na kiuwezo ili waweze kuwatumikia wananchi.Hivi kweli sugu anafaa kwenda bungeni au ushabiki tu
Wewe unafikiri nani anafaa? usiwe na mawazo mgando wewe!
Kama mji unarindima watawezaje ndio imetoka hiyo. Maggid tupe news?
uanauliza SUGU, huyo mganga wa kienyeji maji marefu na darasa lake la saba anafaaa??Hivi kweli sugu anafaa kwenda bungeni au ushabiki tu
October 31, 2010
BREAKINGNEWs MATOKEO YA UCHAGUZI HALI SI NZURI KWA CCM IRINGA
Na Francis Godwin,Iringa
MATOKEO ya awali katika jimbo la Iringa mjini, Njombe Kaskazini na Njombe Magharibi yameanza kutoka jana usiku huku vituo mbali mbali wagombea wa ubunge na urais wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakionekana kung'ara zaidi .
Katika jimbo la Njombe Magharibi mgombea ubunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo zaidi ya vituo 10 vya kata ya Ilembula ,Mdandu na Saja ameonyesha kufanya vizuri ukilinganisha na mgombea wa CCM Gyerson Lwenge kama ilivyo katika jimbo la Njombe Kaskazin ambako mgombea wa Chadema Alatanga Nyagawa akionyesha kuvutaka shati mgombe wa CCM Deo Sanga katika maeneo ya Lupembe ,Wangama na baadhi ya maeneo ya Makambako ambako hata hivyo kata ya mji mwema uchaguzi wa udiwani haujapata kufanyika baada ya karatasi ya kupigia kura kukosewa kwa zile za Rukwa kuja kata hiyo na kata hiyo kwenda Rukwa.
Katika jimbo la Iringa mjini mbali ya kujitokeza kasoro kadhaa kwa baadhi ya wana CCM katika kata ya Nduli kushindwa kupiga kkura zao baada ya kukosa majina yao katika daftari la wapiga kura kama ilivyo kituo cha stendi kuu ya mabasi ya mikoani ambako idadi kubwa ya wana Chadema walizuiliwa kupiga kura kwa matatizo kama hayo ,bado Chadema imeonyesha kufanya vizuri katika uchaguzi huo.
Matokeo ya awali katika jimbo la Iringa mjini ambayo yalikuwa yamebandikwa vituoni hadi jana majira ya saa 3 usiku ni pamoja na kituo cha Stendi kuu ambako mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete alipata kura (50) mgombea wa Chadema Dk Willibrod Slaa ( 33) na Prof.Ibrahim Lipumba (1).
Ubunge mgombea wa CCM Monica Mbega (36) ,mgombea wa Chadema,Mchungaji Peter Msigwa (97) na mgombea wa NCCR-Mageuzi Mariam Mwakingwe ( 1)
Kituo cha Ngome namba moja mgombea urais wa CCM Dk Kikwete ( 58) Dk Slaa (74) APPT-Maendeleo Peter Mziray (1),wakati nafasi ya ubunge mgombea wa CCM Mbega ( 39)Msigwa wa Chadema( 90) na Mwakingwe wa NCCR-Mageuzi ( 5)
Kituo cha Umati namba moja Kikwete ( 98) Dk Slaa 108 Mziray (1) ubunge Mbega ( 82) Msigwa ( 120) Mwakingwe ( 5),Kituo namba 2 umati Kikwete (97) Dk Slaa( 98)Mziray (1) na TLP (1) huku ubunge Mbega ( 73),Msigwa (114) Mwakingwe(8) na kituo cha umati namba 3 Kikwete ( 64) Dk Slaa(57)Prof LIpumba (1) ,ubunge CCM( 58) Chadema( 64) NCCR-mageuzi(1).
Kituo cha FFU namba 1 Urais CCM(47) Chadema( 63) huku ubunge CCM(36) Chadema(68),NCCR-Mageuzi (3) na kituo cha FFU namba 2 Urais CCM( 64) Chadema( 57) na CUF( 1), ubunge CCM(58)Chadema( 64) na NCCR-Mageuzi (3).
Kituo cha IDYDC namba 1 nafasi ya Urais CCM( 62) Chadema(75) na ubunge CCM ( 46) Chadema(84) na NCCR-mageuzi (5) na kituo cha IDYDC namba 2 Urais CCM (82) Chadema(68) na NCCR Mageuzi (1) Ubunge CCM( 67) Chadema(78) na NCCR mageuzi (7).
Kituo cha THB Urais CCM (97) Chadema(138) CUF( 3) na ubunge CCM(75) Chadema(159) na NCCR-Mageuzi (2) kituo cha Gangilonga urais CCM( 88),Chadema(70) NCCR-Mageuzi (1) na kituo cha Zimamoto namba 1 Urais CCM(84)Chadema(94) na CUF(2) kituo namba 2 Urais CCM( 103) Chadema(84) CUF (1) NCCR-mageuzi (1) ubunge CCM (87) Chadema(106) NCCR-Mageuzi (8) kituo cha soko la Kitanzini namba 1 Urais CCM( 79) Chadema(49) na CUF (1) kituo namba 2 Urais CCM(84) Chadema(68) na CUF(1),ubunge CCM( 70) Chadema(82) na NCCR Mageuzi (1) kituo cha Makorongoni ofisi ya mtendaji kata CCM Urais (66) Chadema( 77) na CUF( 1) ,ubunge CCM( 49) Chadema(96) NCCR-Mageuzi (1), kituo namba mbili ofisi ya mtendaji kata ya Makorongoni Urais CCM (81) Chadema(81) ,CUF(2) UPDP(1)Ubunge CCM(78)Chadema(108) na NCCR-mageuzi (5)
Hata hivyo matokeo hayo baadhi ya vituo hadi majira ya saa 3.30 usiku yakiwa bado kubandikwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwa wamekaa nje ya vituo hivyo wakisubiri kutangazwa kwa matokeo hayo huku FFU wakizunguka zunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kulinda amani japo hakuna vurugu zozote zilizopata kutokea jimbo la Iringa mjini