Matokeo ya NACTE yametoka?

Matokeo ya NACTE yametoka?

Jaman kwa anaejua tatizo litakua nn mie mpaka leo nikiingia kwenye profile yangu nakuta system still running
 

Attachments

  • Screenshot_2017-09-20-07-30-39.png
    Screenshot_2017-09-20-07-30-39.png
    15.5 KB · Views: 139
Sorry, ya ualimu nayo yametoka maana mie nikiingia kwenye profile yangu nakuta system still running cjui kunatatizo gani, kwa anaejua plz
Ualimu mbona yalitoka ila joining instructions ndio wanasema muwe wavumilifu mpaka sasa mimi chuo nilichopngiwa hakijathibitisha naandikiwa pending labda kama kuna mwingingine anisaidie kama chuo kimethibitisha hii hali ina kera kweli kuanza masomo wizara ya elimu inasema tarehe 25 ila uthibitisho toka chuoni bado pending
 
Kibaha na muhimbili mwsho one ya 10 NAaa ivi kwa maelezo yao jana nlienda uko kuuliza nkachokaaa
Mtu mwenye ufaulu huo kwa nini asiende A-level? Diploma ni kitu kidogo ...unakwenda kwa vile umekosa A-level au hujiamini kuwa A-Level hauta perform vizuri ukiangalia na grade za sasa kuingia say medicine, engineering etc!!
 
Ualimu mbona yalitoka ila joining instructions ndio wanasema muwe wavumilifu mpaka sasa mimi chuo nilichopngiwa hakijathibitisha naandikiwa pending labda kama kuna mwingingine anisaidie kama chuo kimethibitisha hii hali ina kera kweli kuanza masomo wizara ya elimu inasema tarehe 25 ila uthibitisho toka chuoni bado pending
Umechaguliwa Chuo gani
 
Kwa wale ambao hawakupata, wametoa tangazo kuwa waingie kwenye profile zao. Ukiingia hupati option/window ya kufanya new applications au ku reload hizo hizo za mwanzo. Kwenye profile kuna matokeo ya kutochaguliwa na sababu. Unafanyaje if you have any idea.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA MAOMBI YA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Date Posted: 20th September 2017 04:18:26 Posted By: NACTE

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

looogo.png






TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA MAOMBI YA UDAHILI

KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA

MWAKA WA MASOMO 2017/2018



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kufahamisha umma kuwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Udahili, awamu ya pili imefunguliwa kuanzia tarehe 18 Septemba, 2017 hadi tarehe 1 Octoba, 2017 kwa vyuo vyote ambavyo bado vina nafasi wazi za udahili.

Hivyo wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari wenye sifa za kujiunga na programu za Astashahada na Stashahada, walioomba na hawakufanikiwa kupata nafasi katika awamu ya kwanza na wale ambao hawajaomba hadi Udahili ulipofungwa tarehe 20 Agosti, 2017 watume maombi ya Udahili kwenye vyuo vya serikali na binafsi.

Kwa wanaotaka kuomba vyuo vya Serikali/Umma kwa fani za Ualimu na Afya watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz kwa kubonyeza kitufe cha Apply online (SAVS) kama ilivyokuwa awali. Kwa wale ambao wamekweisha fanya maombi kwenye mfumo na hawakuchaguliwa wanaweza kubadili machaguo yao kwa kurekebisha programu walizo chaguo au kada kwa kutumia kurasa (Profile) binafsi zao.

Baraza linatoa taarifa kuwa vyuo na kozi zilizodahili wanafunzi wa kutosha hazitaonekana tena wakati wa maombi ya awamu hii ya pili. Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kuwa wafanye maombi yao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho za kufunga dirisha la Uhakiki.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 20/09/2017
 
Back
Top Bottom