Matokeo ya Mandonga pale zenji jana mbona mi sijayaelewa?

Clever505

JF-Expert Member
Jul 27, 2020
1,099
2,032
Kwa uelewa wangu mdogo wa boxing baada ya kuufatilia ni kwamba,

Points zinapotangazwa mfano 56 kwa 59 bila kutaja majina ni kwamba yule bondia aliyeingia mwanzo points zake ni zile zinazotajwa mwanzo na zinazotajwa mwisho ni za bondia wa mwisho kuingia. Na hata majina yanavyoandikwa kwenye tv jina la aliyeingia mwanzo linaandikwa mwanzo kisha linafata la mwenzake,.

Sasa Jana pambano la Mandonga, yule jamaa aliyepigana nae aliingia mwanzo na jina liliandikwa mwanzo
Othman kiluwa V Karim Mandonga
Na points zilipoanza kutajwa, points za mwanzo zilikuwa ndogo kuliko za pili kwa majaji wote nikashangaa Mandonga hatangazwi mshindi.

Naomba wenye uelewa zaidi wa hili Jambo anijuze.
 
Mkuu, kuna jambo halikwenda sawa. Hata kwenye runinga, alama za Mandonga aka Mtu Kazi zilionesha kuwa ndiye mshindi.

Cha kushangaza, Wasiwasi Mwabulambo akamtangaza yule Mzenji kuwa mshindi.

Sasa ni dhahiri kuwa Mandonga anaonewa na kukandamizwa waziwazi. Atendewe haki yake!
 
Mkuu, kuna jambo halikwenda sawa. Hata kwenye runinga, alama za Mndonga zilionesha kuwa ndiye mshindi. Cha kushangaza, Wasiwasi Mwabulambo akamtangaza yule Mzenji kuwa mshindi. Sasa ni dhahiri kuwa Mandonga anaonewa na kukandamizwa waziwazi. Atendewe haki yake!
Hata zilipokuwa zikitajwa points ukimuangalia Mandonga alikuwa anafurahia kila zikitajwa na alijua wazi yeye ndo mshindi, mwisho aliduwaa kuona hatangazwi mshindi.
 
Mkataba wetu sisi kati ya mandonga na mashabiki ni LAZIMA apigwe,sasa akipiga anakuwa katoka nje ya makubaliano yetu.
Kama ndo mkataba wenu na Mandonga inabidi apigwe kweli sasa sio ashinde yeye kisha ushindi apewe mwingine.
 
Mkuu, kuna jambo halikwenda sawa. Hata kwenye runinga, alama za Mandonga aka Mtu Kazi zilionesha kuwa ndiye mshindi.

Cha kushangaza, Wasiwasi Mwabulambo akamtangaza yule Mzenji kuwa mshindi.

Sasa ni dhahiri kuwa Mandonga anaonewa na kukandamizwa waziwazi. Atendewe haki yake!
Hii sio poa kabisa, uhuni huu
 
Kama ndo mkataba wenu na Mandonga inabidi apigwe kweli sasa sio ashinde yeye kisha ushindi apewe mwingine.

Tupo katika mchakato wa kuongezea hicho kipengele katika mkataba kuwa hata akishinda atangazwe mpinzani wake ndo kashinda ili shughuli inoge
 
Back
Top Bottom