Matapeli wa Madini Mwenge, kuweni makini

Status
Not open for further replies.
Duh. Bado Kuna Wizi Huu Hadi Leo Hii? Nilikutana Nao Miaka 20 iliyopita. Kidogo Waniingize Mjini. Natamani Nipate Fursa ya Kukutana Nao Twende Sawa.
 
Habari zenu wapendwa,

Jamani kilichonikuta jana, nilikua naelekea bank ndo kukutana na jamaa kachoka anajidai yeye mchimbaji mdgo mdgo kutoka Tanga anataka kubadilisha iwe Fedha nikamwambia simwelewi maana alikua anaongea haraka, ghafla akatokea mwanamke na jamaa akamsimasha na kuomba msaada uleule ndo yule mmama kusema dada umeshindwa kumsaidia nikwamwambia simwelew lakini yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake kisa kanisimamisha wa kwanza.

Sasa yule mama ndo kujifanya anaongea na padri ambaye huwa ananunua madini na kuwauzia Wachina. Sasa nikawambia si msaidiane but yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake na hamjui mtu mjini. Ghafla huyo padri kafika na dereva na kupima huyo mzigo kama uko sawa akaona ndiyo wakasema inabd tufungue account kwa jina langu kwasababu waliniuliza nilikua naenda bank kufanya nini nikawambia kufungua account ndo kujifanya tusaidie kufungua account tuwekee hzo mil.40 lkn inabidi tuwe na mil 2 ili kukamilisha.

Hapo jamaa akawa kashasema atanipa 3 million.Sasa hapo sielew chochote mara wakaomba simu zote na hela ili jamaa tusimtapeli.. (imagine) basi hela ikawa haijakamilika ndo kutoa jiwe moja sawasawa na mil.moja na nusu. Wakaniambia nishuke nitoe copy ya kitambulisho lakini nikawambia bank mbona photocopy machine ipo wakasema tunataka tukiingia bank tuharakishe zoezi.

Kutoka stationery sikuwaona wamechukua hela yangu na simu zangu mbili zote smartphone ndo kuulizia watu hapo Mwenge wakasema dada umeliwa. I was confused nikaenda Sonara kuwaonesa jiwe wakasema ni fake hiyo na huyo mdada kunisimulia story kama hizo nyingi tu kwasababu watu kila siku wanatapeliwa.

Wapendwa, kuweni makini sana mtu akikusimamisha na kukuongelesha sana na humwelewi usimjibu wanatumia dawa au muitie mwizi. And you kama unajijua ndo zako, may Fire Strike you.

Sasa hiyo namba yake niliisave kwenye line na line yangu ni BACKUP that means nikirenew naweza ipate. Je nikiipata nifanyaje?
Umekuja lini dar? Mpk waibiwa style ya miaka ya 90
 
izi stori STAMICO sijui takataka gani zinaniuma sana....bi mkubwa wangu alipigwa million 1 akiwa anaelekea bank tena kwa msaada wa mwanamke mwenzie.
 
Utapeli wa mwaka 1990 huo wakati nasoma bunge primary std3
 
  1. Utapeli wa mwaka 1990 huo wakati nasoma bunge primary std3
    ht
Miaka hiyo ilikuwa hatari walikuwa natabia ya kunusa wenyana hela na Mimi nilikuwa nnazoza serikali kilichosaidia mjomba alikuwa tapeli hivyo tabia, ujanja na maelezo ya kuchota mtu nilisha fundishwa nilicheza nao kimtindo mwisho ili niitoe hela niliwaambia twendeni Monduli Jeshini tukazichukue kundi moja liliafiki na lingine lilikataa nami niliwasisitiza wakodi gari tukachukue mzigo mwisho walikubaliana wakatafute gari ya kutupeleka na kurudi wakaniacha wakisema tunakuja usiondoke baada ya muda sikuona gari wa zamani wafuata gari wakati wote nilikuwa nawachora wangejichanganya tu walete gari tuende, Aaah nashindwa kumalizia
 
Wote wanaotoa OMO hawajawahi tapeliwa.
Nafikiri kuna mambo ya kuya avoid. Hizi stori zipo sana. Kwanini uanze tu kupiga stori na stranger. Mimi huwa hata si entartin mazungumzo. Maana ukianza tu kusikiliza wanakuchota akili. Maana huyu aliyeibiwa inaioneka hakuwa anajua kitu kama hiki kipo. Tatizo wanacheza tu na saikolojia na wanahakikisha hawakupi nafasi ya kufikilia mara mbili ukichanganya na madawa yao ya kienyeji umekwisha.. Solution ni kutoanzisha mazungumzo ovyo na watu njia hata umkute ana shida gani we tembea maana wema wako utakuponza au utakuwa ndo mauti yako
 
Habari zenu wapendwa,

Jamani kilichonikuta jana, nilikua naelekea bank ndo kukutana na jamaa kachoka anajidai yeye mchimbaji mdgo mdgo kutoka Tanga anataka kubadilisha iwe Fedha nikamwambia simwelewi maana alikua anaongea haraka, ghafla akatokea mwanamke na jamaa akamsimasha na kuomba msaada uleule ndo yule mmama kusema dada umeshindwa kumsaidia nikwamwambia simwelew lakini yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake kisa kanisimamisha wa kwanza.

Sasa yule mama ndo kujifanya anaongea na padri ambaye huwa ananunua madini na kuwauzia Wachina. Sasa nikawambia si msaidiane but yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake na hamjui mtu mjini. Ghafla huyo padri kafika na dereva na kupima huyo mzigo kama uko sawa akaona ndiyo wakasema inabd tufungue account kwa jina langu kwasababu waliniuliza nilikua naenda bank kufanya nini nikawambia kufungua account ndo kujifanya tusaidie kufungua account tuwekee hzo mil.40 lkn inabidi tuwe na mil 2 ili kukamilisha.

Hapo jamaa akawa kashasema atanipa 3 million.Sasa hapo sielew chochote mara wakaomba simu zote na hela ili jamaa tusimtapeli.. (imagine) basi hela ikawa haijakamilika ndo kutoa jiwe moja sawasawa na mil.moja na nusu. Wakaniambia nishuke nitoe copy ya kitambulisho lakini nikawambia bank mbona photocopy machine ipo wakasema tunataka tukiingia bank tuharakishe zoezi.

Kutoka stationery sikuwaona wamechukua hela yangu na simu zangu mbili zote smartphone ndo kuulizia watu hapo Mwenge wakasema dada umeliwa. I was confused nikaenda Sonara kuwaonesa jiwe wakasema ni fake hiyo na huyo mdada kunisimulia story kama hizo nyingi tu kwasababu watu kila siku wanatapeliwa.

Wapendwa, kuweni makini sana mtu akikusimamisha na kukuongelesha sana na humwelewi usimjibu wanatumia dawa au muitie mwizi. And you kama unajijua ndo zako, may Fire Strike you.

Sasa hiyo namba yake niliisave kwenye line na line yangu ni BACKUP that means nikirenew naweza ipate. Je nikiipata nifanyaje?
Utapeli wa mwaka 1982 huo..afu unatapeliwa Leo 1987..unaniaibisha Dada angu
 
Nafikiri kuna mambo ya kuya avoid. Hizi stori zipo sana. Kwanini uanze tu kupiga stori na stranger. Mimi huwa hata si entartin mazungumzo. Maana ukianza tu kusikiliza wanakuchota akili. Maana huyu aliyeibiwa inaioneka hakuwa anajua kitu kama hiki kipo. Tatizo wanacheza tu na saikolojia na wanahakikisha hawakupi nafasi ya kufikilia mara mbili ukichanganya na madawa yao ya kienyeji umekwisha.. Solution ni kutoanzisha mazungumzo ovyo na watu njia hata umkute ana shida gani we tembea maana wema wako utakuponza au utakuwa ndo mauti yako
Kweli kabisa kiongozi.
 
Tamaa imekuponza hakuna ushirikina hapo kwa akili ya kawaida mtu hata hakujui akupe milioni tatu da yani wewe dada ni bonge la bashite
 
Alafu huu utapeli ni wa siku nyingi miaka ya 2000 huko
 
Niliwai pigwa kama elfu 40.Sinema ilianzia mbgala tukaenda Kigogo tukaishia Msasani.Kuna dawa wanatumia husijielewe,Sasa hivi sitaki hata salamu ya mtu nisiyemfahamu.Ila ilinibidi niingie kwenye hiyo field niyafahamu hayo mawe.Shukrani kwa Mrangi amekuwa Mwalimu bora kwangu.Ukitaka kunitapeli na hayo mawe jipange.
 
Mjini kumejaa chenga za Pele kila kona.
Mwana FA akiwaambia 'msije mjini'... basi mnanuuuna to the fullest.
Your last mistake is your best teacher!
Bongo DarSlum. Pole dada'ake.

-Kaveli-
 
Wiki iliyopita nilikuwa kanisani Roman Catholic Sinza misa ya kuaga msiba,mama mmoja akashushwa kutoka kwenye Porte nyeusi ikaondoka halafu yule Mama akauliza kwa mlinzi kama Padre Peter yupo,mlinzi bila ajizi akamjibu yule mama tayari umeshatapeliwa yule mama akazimia kina mama waliopo pale wakamsaidia huduma ya kwanza alippzinduka akasimulia habari kama yako kuhusu madini
Yeye aliwatolea Bank shs.milioni 9
Alitokea Mbeya na hela chama chao cha akina mama
Nilisikitika sana
 
pole sana mie niliwahi tapeliwa nilivyokua natoka chuo kule cbe 2009 wanatumia dawa hao wanakupumbaza yani usije jaribu hata kumjibu mtu mmoja umeisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom