suzie _barbie
JF-Expert Member
- May 2, 2017
- 1,523
- 3,073
Habari zenu wapendwa,
Jamani kilichonikuta jana, nilikua naelekea bank ndo kukutana na jamaa kachoka anajidai yeye mchimbaji mdgo mdgo kutoka Tanga anataka kubadilisha iwe Fedha nikamwambia simwelewi maana alikua anaongea haraka, ghafla akatokea mwanamke na jamaa akamsimasha na kuomba msaada uleule ndo yule mmama kusema dada umeshindwa kumsaidia nikwamwambia simwelew lakini yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake kisa kanisimamisha wa kwanza.
Sasa yule mama ndo kujifanya anaongea na padri ambaye huwa ananunua madini na kuwauzia Wachina. Sasa nikawambia si msaidiane but yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake na hamjui mtu mjini. Ghafla huyo padri kafika na dereva na kupima huyo mzigo kama uko sawa akaona ndiyo wakasema inabd tufungue account kwa jina langu kwasababu waliniuliza nilikua naenda bank kufanya nini nikawambia kufungua account ndo kujifanya tusaidie kufungua account tuwekee hzo mil.40 lkn inabidi tuwe na mil 2 ili kukamilisha.
Hapo jamaa akawa kashasema atanipa 3 million.Sasa hapo sielew chochote mara wakaomba simu zote na hela ili jamaa tusimtapeli.. (imagine) basi hela ikawa haijakamilika ndo kutoa jiwe moja sawasawa na mil.moja na nusu. Wakaniambia nishuke nitoe copy ya kitambulisho lakini nikawambia bank mbona photocopy machine ipo wakasema tunataka tukiingia bank tuharakishe zoezi.
Kutoka stationery sikuwaona wamechukua hela yangu na simu zangu mbili zote smartphone ndo kuulizia watu hapo Mwenge wakasema dada umeliwa. I was confused nikaenda Sonara kuwaonesa jiwe wakasema ni fake hiyo na huyo mdada kunisimulia story kama hizo nyingi tu kwasababu watu kila siku wanatapeliwa.
Wapendwa, kuweni makini sana mtu akikusimamisha na kukuongelesha sana na humwelewi usimjibu wanatumia dawa au muitie mwizi. And you kama unajijua ndo zako, may Fire Strike you.
Sasa hiyo namba yake niliisave kwenye line na line yangu ni BACKUP that means nikirenew naweza ipate. Je nikiipata nifanyaje?