Matapeli wa Madini Mwenge, kuweni makini

Matapeli wa Madini Mwenge, kuweni makini

Status
Not open for further replies.
Hakuna cha mizizi wala nini...mie walitaka kuingia kwenya anga zangu mwaka juzi mitaa ya Azikiwe natoka CRDB bank naenda kutuma kama 6m Kenya kwenye Equity Bank....akaanza kuniongelesha nikajua tabeli..nikatoa 6m nikamuonesha alafu nikamwambia inama 'nikufir...e' ili nikupe maana njia anayoitumia kutaka kunitapeli ni ya 'kisengerema' ...mshikaji akajishtukia akatimka.
Hahahaha
 
Kuna majamaa siku moja walitaka kunitapeli.

Nilijifanya mjinga kwa kuwalazimisha wao waende na spidi yangu badala ya mi kuendana na spidi yao.
Mwisho wa siku walinikimbia wote na simu zao wakazima na kutupa line kwa jinsi nilivokuwa nikiwaandama bili kuwapa pumzi.
 
Tatizo hujakutana nao, kina Tomaso mpaka muone. Unafikiri wote wanaolizwa kichwani hamnazo.
Mkuu, mi nishakutana nao,, lakini kitu nilichowafanyia hawakuamini...badala ya wao kutaka kunitapeli nilitaka kuwatapeli wao.. Kilichofuata sasa...
 
Mambo mengine ni ya kujitakia, wala hakuna cha dawa wala nini. Kama ni dawa sijui uchawi tuambie unafanyaje kazi mpaka kweli ufanyiwe hivyo. Wale wezi wanatumia psychology kutokana na muonekano wa mtu, na jinsi anavyotembea, na kushangaa shangaa kila kitu anachokiona, na kutazama vitu vya kawaida kwa muda mrefu.

Askofu Dr Gwajima alishatoa ushauri wa kupiga selfie kwanza na kutuma instagram kabla ya kuendelea na shughuli nyingine.

Ushauri wangu, watu mnapokuwa na fedha nyingi na kuwepo barabarani mjitaidi kuwa wawili, halafu hakuna kuongea na mtu wala kupoteza muda wa kusimama simama.
Hili ntalifanyia kazi, kibubu kikiwa kimetuna navaa wa mbuzi mpaka nakoenda.
 
Wenzetu ke wepesi kudanganyika! Hata ukiwambia mi ndiyo Mungu njoo mniabudu, watakuja wengi tu! Sijui wanashinda gani hawa jamaa!
 
Hapo hakuna kutumia dawa wala nini. Hapo uchawi uliotumika kukupumbaza ni tamaa yako ya kupata pesa ya bure tena ya haraka. Mimi nishakutana nao mara moja nikamwambia yule aliekuja kudakia mazungumzo yetu na kujifanya anawajua jamaa wapo Ubungo Plaza wana contact za wateja wao wazungu wa Straburg wananunua madini kwa magendo, nikamwambia "embu msaidie huyu jamaa mimi nawahi shughuli zangu.." nikavuka barabara fasta nikasepa.
 
Habari zenu wapendwa,

Jamani kilichonikuta jana, nilikua naelekea bank ndo kukutana na jamaa kachoka anajidai yeye mchimbaji mdgo mdgo kutoka Tanga anataka kubadilisha iwe Fedha nikamwambia simwelewi maana alikua anaongea haraka, ghafla akatokea mwanamke na jamaa akamsimasha na kuomba msaada uleule ndo yule mmama kusema dada umeshindwa kumsaidia nikwamwambia simwelew lakini yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake kisa kanisimamisha wa kwanza.

Sasa yule mama ndo kujifanya anaongea na padri ambaye huwa ananunua madini na kuwauzia Wachina. Sasa nikawambia si msaidiane but yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake na hamjui mtu mjini. Ghafla huyo padri kafika na dereva na kupima huyo mzigo kama uko sawa akaona ndiyo wakasema inabd tufungue account kwa jina langu kwasababu waliniuliza nilikua naenda bank kufanya nini nikawambia kufungua account ndo kujifanya tusaidie kufungua account tuwekee hzo mil.40 lkn inabidi tuwe na mil 2 ili kukamilisha.

Hapo jamaa akawa kashasema atanipa 3 million.Sasa hapo sielew chochote mara wakaomba simu zote na hela ili jamaa tusimtapeli.. (imagine) basi hela ikawa haijakamilika ndo kutoa jiwe moja sawasawa na mil.moja na nusu. Wakaniambia nishuke nitoe copy ya kitambulisho lakini nikawambia bank mbona photocopy machine ipo wakasema tunataka tukiingia bank tuharakishe zoezi.

Kutoka stationery sikuwaona wamechukua hela yangu na simu zangu mbili zote smartphone ndo kuulizia watu hapo Mwenge wakasema dada umeliwa. I was confused nikaenda Sonara kuwaonesa jiwe wakasema ni fake hiyo na huyo mdada kunisimulia story kama hizo nyingi tu kwasababu watu kila siku wanatapeliwa.

Wapendwa, kuweni makini sana mtu akikusimamisha na kukuongelesha sana na humwelewi usimjibu wanatumia dawa au muitie mwizi. And you kama unajijua ndo zako, may Fire Strike you.

Sasa hiyo namba yake niliisave kwenye line na line yangu ni BACKUP that means nikirenew naweza ipate. Je nikiipata nifanyaje?
Mjinga mkubwa wewe mtu umekutana nae Leo Leo anakutuma atakako unaenda bwege
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom