mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 45,751
- 55,792
Wana dawa wale.Pole sana Dada yangu.
Hivi inatokeaje unamkabidhi mtu vitu vyako vya Muhimu kama simu na vitu vingine?
Usiwe unapagawa ukitajiwa fedha nyingi za Bure. Wewe pita zako tu.
Wana dawa wale.Pole sana Dada yangu.
Hivi inatokeaje unamkabidhi mtu vitu vyako vya Muhimu kama simu na vitu vingine?
Usiwe unapagawa ukitajiwa fedha nyingi za Bure. Wewe pita zako tu.
Unadhani namba yake ni valid?Ndiyo niliisave cuz alisema atahitaji msaada wangu zaid kumbe alijua lazima atabaki na simu yangu
Kuwa macho Siku zote ukisikia mtu anasema ana Madini ujue ni Chain ya Matapeli. Ikiwezekana piga kelele ya mwizi wakamatwe utakuwa umesaidia wengi. Awe mzee, kijana, mchafu ni WEZI wanakuja na staili ya kuleta Wazee ili wasishtukiwe haraka. Shutka Ukisikia neno MADINI AU STAMICO AU MCHIMBAJI. Pole dada wenzako tulishalizwa siku hizi mtu akinisimamisha nisyemjua najiandaa kutapeliwa.usiamini mtu haraka
hamna hela ya haraka haraka maisha haya
Ndio.nakumbuka wakati nauza hard ware.alikuja jamaa,na bodaboda ndo kamleta ilikuwa asubuhi.jamaa akatoa oda ya vitu vya laki sita.lakini wakati naongea nae nikachange ghafla.nikawa sielewi naongeleshwa nini,naitikia tu.giza giza.Matapeli wengi wa kupiga pesa ndefu huwa wanatumia mizizi. Ukijibu tu hata salamu(kuongea nao), umejiharibia mana kizizi kimeshanasa. Fahamu zitarudi umelizwa.
Kuna siku nilikutana na matapeli wa aina hiyo Iringa nikiwa nimebeba zangu Ada ya Shule,mwanzoni nilikataa kama wewe lakini baada ya muda akatokea jamaa mmoja kavaa kinadhifu sana,baada ya kuongea mawili matatu,nikakubaliana naye kumsaidia huyo aliyejiita muuzaji wa madini kwa kumpeleka Bank,Bahati nzuri baada ya kutembea mita kama 30 hivi kuelekea Bank kuna hisia za hatari zikanijia,pale pale nika-make U-turn ya ajabu!Hawakuamini.Sijui kwanini watu wengne wanakuwa na jazba.Anyway kwa wale ambao haijawatokea please kuweni makini.
Kuwa macho Siku zote ukisikia mtu anasema ana Madini ujue ni Chain ya Matapeli. Ikiwezekana piga kelele ya mwizi wakamatwe utakuwa umesaidia wengi. Awe mzee, kijana, mchafu ni WEZI wanakuja na staili ya kuleta Wazee ili wasishtukiwe haraka. Shutka Ukisikia neno MADINI AU STAMICO AU MCHIMBAJI. Pole dada wenzako tulishalizwa siku hizi mtu akinisimamisha nisyemjua najiandaa kutapeliwa.
Pole sana dada..Habari zenu wapendwa,
Jamani kilichonikuta jana, nilikua naelekea bank ndo kukutana na jamaa kachoka anajidai yeye mchimbaji mdgo mdgo kutoka Tanga anataka kubadilisha iwe Fedha nikamwambia simwelewi maana alikua anaongea haraka, ghafla akatokea mwanamke na jamaa akamsimasha na kuomba msaada uleule ndo yule mmama kusema dada umeshindwa kumsaidia nikwamwambia simwelew lakini yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake kisa kanisimamisha wa kwanza.
Sasa yule mama ndo kujifanya anaongea na padri ambaye huwa ananunua madini na kuwauzia Wachina. Sasa nikawambia si msaidiane but yule jamaa akawa kaniganda eti mimi dada yake na hamjui mtu mjini. Ghafla huyo padri kafika na dereva na kupima huyo mzigo kama uko sawa akaona ndiyo wakasema inabd tufungue account kwa jina langu kwasababu waliniuliza nilikua naenda bank kufanya nini nikawambia kufungua account ndo kujifanya tusaidie kufungua account tuwekee hzo mil.40 lkn inabidi tuwe na mil 2 ili kukamilisha.
Hapo jamaa akawa kashasema atanipa 3 million.Sasa hapo sielew chochote mara wakaomba simu zote na hela ili jamaa tusimtapeli.. (imagine) basi hela ikawa haijakamilika ndo kutoa jiwe moja sawasawa na mil.moja na nusu. Wakaniambia nishuke nitoe copy ya kitambulisho lakini nikawambia bank mbona photocopy machine ipo wakasema tunataka tukiingia bank tuharakishe zoezi.
Kutoka stationery sikuwaona wamechukua hela yangu na simu zangu mbili zote smartphone ndo kuulizia watu hapo Mwenge wakasema dada umeliwa. I was confused nikaenda Sonara kuwaonesa jiwe wakasema ni fake hiyo na huyo mdada kunisimulia story kama hizo nyingi tu kwasababu watu kila siku wanatapeliwa.
Wapendwa, kuweni makini sana mtu akikusimamisha na kukuongelesha sana na humwelewi usimjibu wanatumia dawa au muitie mwizi. And you kama unajijua ndo zako, may Fire Strike you.
Sasa hiyo namba yake niliisave kwenye line na line yangu ni BACKUP that means nikirenew naweza ipate. Je nikiipata nifanyaje?
Kuna uwezekano unachosema ila sidhani.Matapeli wengi wa kupiga pesa ndefu huwa wanatumia mizizi. Ukijibu tu hata salamu(kuongea nao), umejiharibia mana kizizi kimeshanasa. Fahamu zitarudi umelizwa.
Wewe unayajua wengine tunayaona kwenye TV. Nawaasa wasioyajua wasiwachekee wala kuwasikiliza hao wachimbaji na wauza madini Feki. Piga kelele mwizi ukisikia neno Madini kwa Stranger ni WEZI.watanitapalije sasa madini nayajua kama sala in and out.
Wewe unayajua wengine tunayaona kwenye TV. Nawaasa wasioyajua wasiwachekee wala kuwasikiliza hao wachimbaji na wauza madini Feki. Piga kelele mwizi ukisikia neno Madini kwa Stranger ni WEZI.
....nini wewe,unawashwa?matusi ya nini..
i wish ningekuwa mod ningekupiga ban ya miaka tisa.
....nini wewe,unawashwa?
...hiyo lugha tu ya kitaa shangazi!
..haya kuwa sasa mod unipe hiyo ban!