Ndiye aliyekuwa mmowapo kama siyo mtu wa kwanza kabisa kuwa anaendesha pikipiki hiyo kwa tairi moja. Alikuwa akijiskia tu, anakuja anatoa shoo ya ukweli. Pia alikuwa na boti yake alikuwa ameiandika na kuiita "Queen Duluthi", kila wakati utamuona ameifunga kwenye cruiser yake anaelekea kwenye ziwa Duluth kula bata nk. Enzi hizo pia kulikuwepo na party pale ziwa Duluth kila mwaka kama sikosei. Kiukweli yule jamaa hakuwa na hata chembe moja ya uoga kwenye damu yake. Mpambanaji wa ukweli na mchagga halisi!