Maswali yangu yaivuruga ACT-Wazalendo

Maswali yangu yaivuruga ACT-Wazalendo

Amemfuata nani?wamefuatwa wangapi ?au ni kwakuwa ni kiongozi mkuu ndio hamtaki watu wamzungunzie?
Alaaa sasa wewe ulifuata nini katika mkutano wake? tena ukazungumza na Msaliti unamuuliza maswali ili iweje?
 
Alaaa sasa wewe ulifuata nini katika mkutano wake? tena ukazungumza na Msaliti unamuuliza maswali ili iweje?

Alaaaaa,yaani kipindi cha kampeini,au mkutano wa kiongozi wa chama cha siasa kwa mtu mpenda siasa kwenda kwenye mkutano hakujalishi kama wewe ni mfuasi wa huyo kiongozi,ni sawa na mpenzi wa soka huchagui mechi za kuangalia mkuu!
 
Alaaaaa,yaani kipindi cha kampeini,au mkutano wa kiongozi wa chama cha siasa kwa mtu mpenda siasa kwenda kwenye mkutano hakujalishi kama wewe ni mfuasi wa huyo kiongozi,ni sawa na mpenzi wa soka huchagui mechi za kuangalia mkuu!
Kwa hiyo ulimfuata?
 
Alaaa sasa wewe ulifuata nini katika mkutano wake? tena ukazungumza na Msaliti unamuuliza maswali ili iweje?

... duuh, kwahyo kiongozi wenu haulizwi maswali?. kuhudhuria mkutano wa siasa ni haki ya kila mtu
 
... duuh, kwahyo kiongozi wenu haulizwi maswali?. kuhudhuria mkutano wa siasa ni haki ya kila mtu
Nilichouliza mnafuata mkasema hafuatwi mtu wakati mlikwenda kwenye mkutano wa msaliti ina maana mlimfuata msaliti kwa haki yenu au sio?.. Mnachokataa nini hapa.
 
Zitto wabunge waupinzani ni wezi maaana watapokea kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 200.

Swali: unasema pesa hizo ni zawizi je wewe utapokea? Maana katibu wa bunge alisema unahaki ya kupokea.
Zitto: Nitapokea lakini ntapeleka kusaidia maalbino.
Watu: huuuuhuuuhuuu unauhakika gani hao wabunge wengine watatumia wapi
Zitto: kwa jazba anajibu "waulizeni wao
Watu: buuubuuubuuuubuuuu

Swali la pili
Wewe ulivyo timuliwa kwenye chama chako cha zamani ndani ya siku saba ukahamia chama kingine na kubadirisha katiba kisha kujipatia cheo kikubwa.hauoni kama wewe ni mroho wa madaraka? Alfu mbona unataja vyeo vya wenzio wewe hautaji chako?
Zitto: Zitto hili swali atalijibu mwenyekii
Magwila: mfumo wetu haupo Tanzania tumeuchukua Kenya, kunakua na kiongozi wa chama na mwenye kiti
Watu: weweeee taja cheo chake, wewe na yeye nani mkubwa
Magwira: anaona aibu anacheka, ebu tuangalieni mimi na zitto nani mkubwa
Watu: wewe jibu swaliii
Zitto ana mnyan'ganya mic magwila kisha anajibu kwa jazba sisi hatugawani vyeo tunagawana majukumu
Watu: buuubuuubuuuuuuu

Swali la tatu
Kama ambavyo dr slaa alitaja list of shame vipi na wewe unaujasiri wa kutaja majina ya walio ficha fedha uswisi ukizingatia tunaenda kwenye uchaguzi na tunaweza kuwachagua hau walio ficha bila kujua
Zitto.kwani Slaa alivyo wataja kilibadirika nini majina ntayapelekwa bungeni
Watu: huuuhuuuhuuuhuu
Habibu: anamnyan'ganya mic muuliza swali.
Watu: mwachieeeee
Habibu wanao taka kujiunga na chama waje wajiunge
Watu: mnazinguaaaaaaa

Mytake: Zitto na ACT yake wajipange sana maana una watanzania ni waelewa kuliko anavyodhani.

Hajiulizi mpaka sasa kwanini hakuna mwanachadema anayehama chama na kujiunga nae.

Unatia huruma.....
 
nasema umeuliza maswali ukitegemea majibu uloyapanga na hayakuja... Unamrfananisha vipi Zitto na Dr.Slaa halafu mtu akujibu mbona Slaa likimbia mdahalo kama kweli ilikuwa kuna ushindani? Mnataka ushindani hata mahala pasipo hitajika na kila mnavyomnanga Zitto ndivyo atakavyo wamalizeni siku ya siku msivyo tumia akili wala mahesabu kiasi kwamba naanza kuamini pengine nyie ndio mlotumwa na CCM.

Mkuu Mkandara mbona umeamua kujitoa ufahamu? je mh DR SLAA angeshiriki kama nan? kwa sababu mpaka sasa CDM haijapitisha jina la mgombea URAIS
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara mbona umeamua kujitoa ufahamu? je mh DR SLAA angeshiriki kama nan? kwa sababu mpaka sasa CDM haijapitisha jina la mgombea URAIS
kwani waloshiriki wale walikuwa kina nani? mbona pale mgombea aikuwa mmoja tu na wengine wameshiriki! Mimi sijahoji Dr.Slaa kushiriki ama kutoshiriki ila nimeshangazwa na maswali ya huyu mleta mada ambaye ametoka nyumbani kwake kwenda kuuliza maswali ambayo hayajengi isipokuwa nia na lengo lake linaonekana wazi. Hivi kweli Shetani kesho akisema ana mkutano Jangwani wewe muumini wa kweli utakwenda?

Huu ni muendelezo wa kuhakikisha Ugomvi baina ya Chadema na Zitto unaendelea hadi CCM wachukue dola 2015, maana sioni sababu kwani walokwisha toka Chadema ni Zitto peke yake? Huo Usaliti kwani Kafulila hakuitwa hivyo? hao kina Cheyo, Mbatia, Maalim Seif hawakuitwa vibaraka wa CCM na vyama vyao ni CCM - B. Leo iweje ndio wawe marafiki wazuri wa kutegemea kugawana majimbo wakati CCM inachukua dola. Fumbo wafumbieni wajinga sisi werevu bado hamjatupata.
- Kwa mwoga huenda kicheko kwa shujaa kilio!
 
Tuangalie video ya tunduma kwenye thread ya msaliti mcubic
 
Atathibitisha vipi kwamba mali zitakazotangazwa na fisadi Lowassa zitakuwa za kweli!? Msaliti huyu anaweweseka sana.

Amesema atamwachia Lowassa akiamua kujiunga nao akitokea CCM,mradi tu atangaze Mali zake!!!!!!!!!!!Sielewi kama huo ndiyo ujamaa wanaousema
 
Tuangalie video ya tunduma kwenye thread ya msaliti mcubic
Kama kweli wao ni wanaharakati hawakutumwa, ebu watuonyeshe video walizo muuliza maswali Kinana maana CCM ndiye watapambana kwenye uchaguzi huu..
Najua hakuna hata mmoja wao kwa sababu hawa wote wanaifanya kazi ya CCM na ndio maana wengine wanasema bora Mwandosya, sijui Magufuli wengine Lowassa toka zizi lile lile. Huyo Dr. Slaa ni mapenzi ya uongo mtupu maana wanajua hawezi kushinda wameshabomoa ngome zote za Chadema.
 
Alaaa sasa wewe ulifuata nini katika mkutano wake? tena ukazungumza na Msaliti unamuuliza maswali ili iweje?
Mkuu wangu Mkandara hawa jamaa wanashangaza sana wanahangaika na msaliti ambaye wameishamfukuza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom