Maswali ya Papo kwa Papo Kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Aulizwe Maswali, Ajibu Maswali na Kama ni Ufafanuzi wa Jambo Lolote, Waziri Mkuu Huru Kufafanua

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Tangu Bunge la Bajeti lianze, Alhamisi ya leo ndio kwa mara ya kwanza Waziri Mkuu anautumia muda wa kujibu maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.

Sasa kwanza wenye access kualia Bunge live, angalieni maswali ya leo kwa Waziri Mkuu, kisha nitawaeleza kitu



Karibuni

UTANGULIZI
Tanzania tumepata uhuru wetu kutoka kwa wakoloni Waingereza hivyo kila kitu tumeiga kwa Waingereza kuanzia Katiba, sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji wa Serikali, Bunge, na Mahakama pamoja na taasisi zake hivyo kuna vitu mule vimeandikwa sisi tunavifuata bila hata kujua ni kwanini tunavifanya, just copy and paste!.

Katiba
Kama ilivyo kwa ulimwengu, Mwenyezi Mungu ndie the Supreme Being, kwenye uendeshaji wa nchi,
Katiba ndio the supreme being!.

Hata katiba yetu ya 1977 ina baadhi ya vipengele vya cut and paste, vimo ndani ya katiba yetu, tumevipachika tuu kwasababu ya copy and paste bila kujua mtunga katiba alidhamiria nini kuweka kifungu fulani.

Mfano katiba yetu inasema katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba itakuwa ni sheria batili.

Ubatili huu ni umebatilishwa na katiba yenyewe na sio na Serikali, Bunge, au Mahakama!. Serikali yetu imetunga sheria kibao batili!, Bunge letu likazipitisha hizo sheria batili!, Mahakama kazi yake ni kutafsiri tuu sheria na kuzitangaza kuwa sheria fulani ni batili, na tangu siku ya tangazo la Mahakama kuitangaza sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, from that moment, there and then, sheria hiyo inakuwa imeishabatilika kwa kubatilishwa na katiba!, kilichobakia ni taratibu tuu za kuzi scrap from the books of laws!, lakini kwa Tanzania hali sio hivyo kutokana na cut and paste bila kujua dhamira ya mtunga katiba ndio maana sio tuu tuna sheria batili, bali ubatili huo umechomekewa kiubatili hadi ndani ya katiba yetu!, hivyo katiba yetu ni katiba voidable kutokana na ubatili huo!.

Bunge
Pia uendeshaji wa Bunge letu ni copy and paste ya Bunge la Uingereza, Westminster's Style, ambapo kule Waziri Mkuu ndie Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni.

Kwenye Bunge la Mswekwa kuna siku Kanali Nsa Kaisi aliwahi kutolewa Bungeni kwa kosa la kuvaa suruali ya jeans!.

Bunge la Spika Sitta kuna siku Amina Chifupa (RIP), aliwahi kutolewa Bungeni kwa kosa la kofia ya English Suit bila gloves!, kanuni za Bunge zimekuwa copy and paste hivyo hivyo!. Wenzetu kwao wanawake huvaa gloves kutokana na baridi ya winter season, gloves kwenye Joto la Dodoma ni ya nini?.

Kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali ikiwemo kuunda kamati mbalimbali za uchunguzi, matokeo ya kamati hizo hujadiliwa na Bunge na kutolewa Azimio la Bunge na kuipa serikali kwa utekelezaji, Bunge lilipopokea taarifa fulani na kuikimbiza Ikulu bila kujadiliwa na Bunge na kutoa Azimio la Bunge, nikauliza kitu, matokeo yake sitaki hata kuyakumbuka!.

Bunge likatoa Azimio batili kuwa halifanyi kazi na CAG na halitapokea ripoti ya CAG, ni mpaka tulipo washtua humu nini kingetokea, ndipo wakaipokea ripoti hiyo kimya kimya huku lile Azimio batili lao bado liko kwenye hansard!.

Kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu ndio the most important session, hakuna shughuli yoyote ya kiserikali inaweza kupangwa na kusababisha session hiyo isiwepo!.

Hii nayo tume copy and paste, ila huku kwetu ni Waziri Mkuu atajibu maswali ya wabunge pale anapopata nafasi!, as if maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu ni an optional session!.

Leo katika hii session, Waziri Mkuu kaamua kuitumia kujibu hoja zozote za serikali. Session ya maswali ya Papo kwa Papo na Waziri Mkuu, ni session ya wabunge kuuliza maswali na Waziri Mkuu kujibu hoja. Na ikitokea kuna swali ambalo linahitaji majibu ya kina, ndipo Waziri Mkuu anaweza kuitumia session ya maswali ya Papo kwa Papo kutoa ufafanuzi wa ziada wa hoja yoyote iliyotokana na maswali ya wabunge na sio kuutumia muda huo wa thamani kwa Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi wa jambo lolote!.

Waziri Mkuu ndie Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni, hivyo kama ana hoja yoyote muhimu, anaweza kuiwasilisha wakati wowote, lengo la watunga kanuni ya maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, ni Waziri Mkuu ajibu maswali ya wabunge and not the other way!.

Naomba kuwasilisha

Paskali
 
Maswali ya Papo kwa hapo yako Bunge la Uingereza

Jaribu kuangalia kila Jumatano Sky news

Waziri mkuu anaulizwa maswali hadi anataka kukimbia!!
 
Back
Top Bottom