Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limetoa ripoti ya kile kilichoelezwa kuwa ni sababu zilizopelekea ajali iliyopelekea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mch. Christopher Mtikila na kuainisha sababu hizo kuwa ni pamoja na:
1. Ubovu wa gari kwa kuwa lilipata ajali oktoba 3, moja ya sehemu muhimu zilizoharibika ni mfumo wa usukani, hivyo inawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia ajali hiyo ya pili.
2. Mtikila kutovaa mkanda wa usalama na hivyo kusababishwa arushwe nje kupitia kioo cha mbele.
3. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu ya kuendesha gari mchana na usiku na kabla ya safari kurudi alikuwa akishughulikia matengenezo ya gari hivyo hakupata muda wa kumpumzika.
4. Mwendo kasi.
maswali tata baada ya ripoti ya Polisi
1. Kutofunga Mkanda na hivyo kurushwa nje kupitia kioo cha mbele ni sababu ya ajali au ni yatokanayo na ajali hiyo?
2. Mwili wa Mch. Mtikila haukua na jeraha sehemu yoyote ya mwili, unaweza kurushwa nje kupitia kioo cha mbele hata usichubuke? Ripoti ya Daktari inasema marehemu alivunjika mbavu nane, unaweza kuvunjika mbavu 8 bila kujibamiza popote? Na kama alijibamiza, unaweza kujibamiza na jeraha lisionekane?
3. Mtikila amesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Njombe na kurudi kuja kupata ajali Mkoani Pwani. Mbona ripori ya ya kifo chake imetolewa Mapema sana isivyozoeleka?
4. Daktari aliyechunguza safari za kifo chake ni wa Hospitali ya Tumbi alikopelekwa mara ya kwanza au wa Muhimbili alikohamishiwa?
Kifo cha Mtikila kimekuja baada ya Serikali ya Rwanda inayoongozwa na rais Paul Kagame, rais anayetajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa kushutumu Mtikila kumpa hifadhi kiongozi wa jeshi la waasi la FDLRnchini humo, Brigedia Jenerali GRATIEN KABILIGI(
EXCLUSIVE: Tanzania hosts more meetings for FDLR with ICTR convicts News Of Rwanda – Rwanda News)
Aidha, tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM ambapo Lowassa naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro na hata alipohamia Ukawa, Mtikila amempinga waziwazi kuwa hana sifa za kwenda ikulu kwa sababu ya ufisadi na afya yake. Mtikila alitoa waraka unaosomeka"MTIKILA ATOA WARAKA MKALI KUMHUSU LOWASSA, ADAI NI BALAA"(
#Urais 2015: Mtikila atoa waraka mkali sana kuhusu Lowassa, adai ni balaa kwa taifa ~ Kulikoni Ughaibuni)
Mambo hayo mwili yanahusishwa na kifo cha Mch. Mtikila hususan kupitia mitandao ya kijamii. Watu wamekwenda mbali na kusema namna ambavyo mwili wa Marehemu Mtikila ulivyokuwa umelazwa ndivyo hulazwa maiti za watu waliyouwawa kwa sababu ya kuikosoa serikali ya Kagame.