Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Sidhani km matamshi makali toka kwa mtikila ..kwa lowasa ni makali kuliko aliyowahi waambia engine.
 
Kwako mleta mada, inaonekana wewe unafahamu chanzo cha ajali na kwamba kifo chake hakikusababishwa na hiyo ajali. Hivyo tayari unajaribu kuingilia uchunguzi wa polisi. Nakushauri jipeleke mwenyewe polisi ukatoe maelezo huko kwani huko kutafaa zaidi kuliko kuishia kuelezea humu jf.
 
Huu mwili wa marehemu haupo jinsi alivyokuwa mara tu baada ya ajali. Inaelekea kuna mtu tena mwenye fani ya uuguzi/ udaktari aliyejaribu kumpa huduma ya kwanza , amelala chali, position ya kufanyiwa CPR, mikono pembeni, mkanda wa suruali umefunguliwa, na amefanyiwa last office ambayo hufanyiwa marehemu mara tu baada ya kufa, ambayo ni hiyo tai iliyotumika kumfunga mdomo.

Wape ushirikiano wako polisi basi
 
Mchungaji Mtikila, mtetezi halisi wa Tanganyika, mtetezi wa Katiba, Mtetezi wa Haki za Binadamu, Mungu akulaze mahala pema peponi na kama kuna mkono wa mtu basi Mungu amuweke wazi hadharani kablka jogoo hajawika. umekuwa ni mpambanaji halisi ambaye ulidiriki kuweka usajili wa chama chako rehani kwa kuitetea Tanganyika.

I salute you.

Tukubali tukatae tz tumempoteza mnogeshaji wa siasa ya vyama vingi. Kwa vyovyote ilivyotokea MUNGU MWENYE UWEZO NA ASIYEDANGANYIKA atatoa hukumu ya haki kwa jinsi anavyoona inafaa. Sisi wote ni waja wake. Hakuna atakayeishi milele kwenye hii dunia ya Mungu Tuishi kwa amani na upendo bila ya kukanyagana
 
Mmeanza kutuletea conspiracy theories zenu.
Cc: kombani&john komba
 
Tukubali tukatae tz tumempoteza mnogeshaji wa siasa ya vyama vingi. Kwa vyovyote ilivyotokea MUNGU MWENYE UWEZO NA ASIYEDANGANYIKA atatoa hukumu ya haki kwa jinsi anavyoona inafaa. Sisi wote ni waja wake. Hakuna atakayeishi milele kwenye hii dunia ya Mungu Tuishi kwa amani na upendo bila ya kukanyagana

Uwe wazi una mana gani bila kukanyagana?
 
Kwako mleta mada, inaonekana wewe unafahamu chanzo cha ajali na kwamba kifo chake hakikusababishwa na hiyo ajali. Hivyo tayari unajaribu kuingilia uchunguzi wa polisi. Nakushauri jipeleke mwenyewe polisi ukatoe maelezo huko kwani huko kutafaa zaidi kuliko kuishia kuelezea humu jf.

anaweza
 
yaani mtu anauliza nani kapiga picha na trafic wapo hapo?
huu ufala wa kujifanya forensic detectives muuache.
 
Anayepaswa kutujibu hatuponaye duniani yeye huishi mbinguni. JAMANI TUMWAMINI Mungu.
 
Kweli we ndio mmoja wa wale wa kupima akili.

Kwaiyo una maanisha kuwa kafa katika mazingira ya kishirikina, kanyongwa au kapigwa sumu? hueleweki mbona? kwani mwili si huwa unapimwa tu na majibu yote yaliyopelekea umauti yanaonekana?
 
Kufa n Kufa tu

Maswali mengine hayana maana. Tunafanya kazi ya madaktari? Wewe unayesema nguo hazijachanika na blabla nyingine umeuona mwili wake au hizo picha? na eneo la Chalinze unalosema liko bize ni chalinze ipi? unaambiwa amepata ajali maeneo ya Msolwa na Msolwa ni kijiji kidogo sana kama unaelekea Morogoro toka Chalinze na kabla ya kufika Msolwa ukitoka Chalinze kuna Pori na pia baada ya Msolwa kuelekea Mdaula napo pana pori . Unajuaje kama hiyo ajali imetokea eneo gani hapo Msolwa. Acha kuaminisha watu kuwa ajali imetokea chalinze town. Ni mapema mno kujua chanzo cha ajali. Hivi wewe ushawahi kuendesha gari? Sababu pekee ya gari kuacha njia ni kupasuka tairin tu? Unajua mwendo kasi nayo husababisha gari kuacha njia? Unajua barabara zetu zilivyo na manundu na kusababisha gari kuyumba? Unajuaje kama dereva alisinzia kwa uchovu wa kuendesha gari usiku? Hizo zote ni dodoso tuache kudhani dhani na kifo kila mtu kaandikiwa cha aina yake
 
upande wa dereva ndo umepondeka zaidi Mtikila tu ndo wakufa hapo hapo? uchunguzi ufanyike juu ya hiki kifo hapana kwa kweli hainiingii akilini kabisa

Nafikiri ungfikiria walioongozana nao wanapishana kiumri kiasi gani na hayati Mchungaji Mtikila. Ukubwana misukosuko kama ajali kuna baadhi mshituko pekee unaweza kusimamisha mwendo wa mapigo ya moyo.
 
Historia ipo ili watu wajifunze kwayo, kila tukio linalotekea ni funzo kwa mwenye akili…

Mwaka 1985 tarehe 7 April, Afisa mstaafu, Mwanasheria na Mwanaharakati maarufu nchini Uingereza mwenye asili ya usikochi Willie MacRae ambaye alikuwa Makamu mwenyekiti wa SNP, aliyekuwa akipambana na Unyonyaji wa waskochi masikini na makundi ya mafia yenye kumiliki makampuni makubwa nchini humo alipata ajali ya gari na kufariki katika milima ya Scot.

Ajali yake ilizua mjadala mkubwa kuwahi kutokea nchini humo kutokana na mambo yafuatayo;

1.Wajihi wa Willie na vita yake dhidi ya MAFISADI.
2.Utata wa Ajali yake.
3.Ripoti ya Polisi.

WAJIHI WA WILLIE NA VITA YA UFISADI.
Willie kama walivyo wanaharakati wengi duniani alikuwa ni sauti ya wasio na sauti, wanyonge wa nchi ambae alitangaza wazi wazi vita dhidi ya Wanyonyaji na Mafisadi nchini mwake, akiwa kama Mpinzani ambaye aliweza kuwashambulia na hata kufungua kesi mara kadhaa mahakamani kupinga operation za makampuni makubwa ya Nuclear yanayomilikiwa na Mafia wenye mikono mirefu Serikalini ambao walinunua vyama vya siasa na wanasiasa kuwatetea.

Willie akiwa mstari wa mbele kupinga Kitendo cha Kampuni ya Dounrey Nuclear Power Development kumwaga takataka baharini, alifungua kesi na kuandaa vidhibiti vya kisheria kuthibitisha kuwa jambo hilo lina athari kubwa kwa wananchi, na kutokana na vitisho na sensitivity ya vidhibiti hivyo ilimbidi awe anatembea navyo kila wakati na kila anapokwenda hakuwahi kuziacha sehemu hata ofisini kwake ingawa baada ya kifo chake haikujulikana Document hizo zilipotelea wapi.

UTATA WA AJALI.
Watalii wawili watalii wa Ki-australia waliona gari aina ya Volvo katika bonde la Glenmoriston, na watalii wale walisogelea na kukuta mwili wa mtu kwenye gari hiyo ukiwa umejaa damu kuanzia kichwani na mwili mzima, mikono ikiwa imeshika usukani wa gari, kichwa kimelalia bega moja na hakuwa amevaa mkanda wa gari (seatbelt)
Wakasogea barabarani na kusimamisha gari ambayo ndani yake kulikuwa na Diwani wa Chama Cha SNP ambaye alimtambua WILLIE na kutambua pia kuwa alikuwa HAJAFA bado, wakamuwaisha Hospitali Aberdeen Royal infirmary ambapo alifariki na hospitali hapo iligundulika alipigwa risasi kichwani, kabla ya gari yake kutumbukia kwenye korongo hilo.


RIPOTI ZA POLISI
Ilikuwa kitendawili kikubwa kwa kuwa ripoti ya kwanza ilisema kuwa alitumbukia bondeni kwa kukosa kulimiliki gari kutokana na spidi, lakini ripoti ya hospitali inasema alipigwa risasi ya kichwa kabla ya kutumbukia kwenye korongo na kwa kuwa kioo cha gari hiyo hakikuwa na tundu la risasi ikabainika kuwa mpigaji wa risasi hiyo alikuwa ndani ya Gari hiyo kisha akashuka na kulisukuma gari kwenye Korongo.
Uchunguzi pia ulibaini kuwa bastola aina ya Wesson 45 Calibre ilipatikana mita chache kutoka ilipookotwa gari ya Willie, lakini hakukuwa na alama zozote za vidole kwenye bastola hiyo jambo lililofanya isitumike kama ushahidi katika upelelezi wa kesi hiyo.

TUKIO SIKU YA KIFO CHA WILLIE
Siku ya Kifo cha Willie ambacho kilikuwa ni gumzo kilifuatiwa na tukio la Wanasiasa wawili maarufu na wabunge wa Chama Cha Ulster Unionist kujiuzulu, Ulster ni Chama ambacho kilikuwa kinapingana na harakati za WILLIE. Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni Decoy..,kuwaondoa wananchi katika mjadala wa kifo cha WILLIE.

‘’NCHI zingine Duniani Serikali zina Mafia lakini TANZANIA mafia wana Serikali..” Dr Slaa Nov,2009 on response to Richmond Scandal’s.

R.I.P Mtanganyika Rev. Christopher Mtikila…Hivyo ndivyo ulivyo mwisho wa wanaharakati wa kweli duniani.
 
ila kingunge alikuwa na haraka gani kuongea leo wakati wa msiba wa siasa uliotokea asubuhi tu! connect dots.
 
Back
Top Bottom