Ningependa kutofautiana kidogo na kukubaliana na wewe sehemu nyingine.Lakini ujue hata kwenda sekondari ya seminari haikuwa haikuwa rahisi. Mara nyingi waliokuwa wakifauru seminari walifauru pia kwenda sekindari za serikali.
Halafu kuacha seminari siyo sababu ya performnace tu ika wakati mwingine kutofautiana mawazo.
Moja Enzi za zamani Watu wengi walipenda kupeleka watoto Shule za seminari kutokana naweledi na nidhamu za hizo shule, Shule za serikali wakati Huo zilikuwa chache saana hivyo ilikuwa unaweza kuwa hukuchaguliwa lakini ulifaulu hivyo ilikuwa kwa mzazi mwenye kujua umuhimu wa elimu kuanza mchakato wa kupata seminari toka mtoto Yupo darasa la tano au sita kwa kupata recommendation toka kwa parokiani yako na kupewa progress report toka Shule ya primary , Shule zingine ambazo zilikuwa ni nzuri au zilihitaji juhudi binafsi za mwanafunzi ni hizi private school ikiwemo lake kwa mza, buluba shy , mzizima, na zile za Moshi ambazo zingine zilikuwa sub standard in terms ya tabia na zingine zilikuwa nzuri kibohehe, kolila kibo boys etc .
Na kubaliana na wewe kuwa kutoka Shule za semenari kunaweza kutokea kutokana na kuto kubaliana na msimamo wa uongozi wa Shule na mwanafunzi etc kwa sababu waalimu wengi wa seminari hawapendi kuwa challenged nina mfano wa mtoto wa ndugu yangu alikuwa seminari moja lakini alipishana na uongozi wa shule akafukuzwa kisa kuulizia fedha za michezo , hivyo mzazi ilibidi akate rufani jimboni na bahati nzuri alipata seminari nyingine kwa vikwazo vingi ikiwemo kwamba anakoenda performance Yao ni juu , ataiharibu etc lakini baada ya hapo yeye alikuwa anafanya vizuri kuliko hao aliowakuta