Maswali kuhusu elimu ya awali ya Dr. Joseph Magufuli

Maswali kuhusu elimu ya awali ya Dr. Joseph Magufuli

Enzi hizo miaka ya 1967 mwaka wa masomo ulikuwa unaanza November na kumalizika Oktoba mwaka unaofuata. Hivyo ni sahihi kwamba alisoma miaka saba shule ya msingi kutoka Novemba 1967 hadi Oktoba 1974.

Waliosoma miaka hiyo wanaweza kuthibitisha hilo.
 
Mi nimeona hili:
Alizaliwa kijiji cha Chato ,sasa ni kijiji cha Mlimani!
Wilaya Biharamulo sasa ni Wilaya ya Chato!
Mkoa wa Kagera sasa ni mkoa wa Geita!
 
Mtoa mada jiandaye kutumbuliwa. Jamaa hata jana alsema hana uvumilivu
 
Mmmh wabongo...seminar kwenda lake....mmmmhhh
 
Tumuache mkono wa chuma akili za chuma....na ameshasema hana uvumilivu na hataki kukosolewa!! Ina maana ataendesha kama robot na hataki kushauriwa! Kuna siku tutarudia hapa kuja kujadili tena! Kwa nini hapendi kushauriwa au kukosolewa?
 
Utakuwa kizazi cha sasa kisichofanya utafiti kabla ya kuamini jambo. Kwa ufupi kuna kipindi elimu ilikuwa tofauti na iliyopo sasa. Fanya utafiti.
umesema kweli mkuu.
Mimi nilianza primary mwaka 1974 Oktoba halafu tukaenda likizo ya krisma. tuliporudi january 1975 tukaambiwa utaratibu umebadilishwa na serikali kwamba kuanzia 1975 shule za msingi zitaanza mwaka wa shule mwezi January na kumaliza oktoba na ndiyo iliyobaki mpaka hawa watoto waliozaliwa wakati huu ww kuku wa kisasa mnapata vipara kabla ya muda wenu. Kwangu mimi ninaweza kusema nilianza primary mwaka 1974 na kumaliza 1982 ama 1975 hivyo ni bora kufanya research kabla kuanza kutoa kashfa. Ni bora huyu mtoa mada akafanya utafiti.
 
umesema kweli mkuu.
Mimi nilianza primary mwaka 1974 Oktoba halafu tukaenda likizo ya krisma. tuliporudi january 1975 tukaambiwa utaratibu umebadilishwa na serikali kwamba kuanzia 1975 shule za msingi zitaanza mwaka wa shule mwezi January na kumaliza oktoba na ndiyo iliyobaki mpaka hawa watoto waliozaliwa wakati huu ww kuku wa kisasa mnapata vipara kabla ya muda wenu. Kwangu mimi ninaweza kusema nilianza primary mwaka 1974 na kumaliza 1982 ama 1975 hivyo ni bora kufanya research kabla kuanza kutoa kashfa. Ni bora huyu mtoa mada akafanya utafiti.
Yeyote ambaye ameshindwa kuvifikia viwango vilivyowekwa vya ufaulu katika shule za seminary, huondolewa. Kwa siku za huko nyuma, ukiondolewa seminary, mahali pekee pa kwenda ilikuwa ni private schools. Ni rahisi sana kupoteza mwaka wakati wa kutafuta shule.
 
Huna hoja ya msingi manake kuanza kusoma shule flan hulazimishwi kumaliza hapo ukiona mazingira sio unahama kabisaaaaa unatafta yatayokufaa
 
Baada ya kidato NNE hakuchaguliwa kwenda kidato cha 5 hivyo ilibidi aende kusoma ualimu akitokea kidato cha nne
 
Zamani primary school ilikuwa miaka 8. Na ndiyo maana utasikia watu wa zamani form 1 wanaita darasa la 9.
 
Issue ya kutoka Seminary na kwenda Lake Secondary iko wazi kabisa kwamba SEMINARY wanautaratibu kuwa mtu ambaye performance yake darasani inakuwa poor huwa hawataki kuendelea naye na humfukuza shule mhusika, the same thing happened to MAGU, Baada ya kuwa ametimuliwa ilibidi MZAZI wake amtafutie nafasi pale LAKE Sec ili aendelee na masomo ya SECONDARY. Kipindi hicho most of private schools zilikuwa zinachukuwa wanafunzi waliokosa nafasi kwenye shule za serikali( failures wa mtihani wa Std 7).Kwa hiyo kipindi kile mtu anayesoma private school ni mtu ambaye alifeli Mtihani wa Darasa la Saba ila kwa sasa hivi imekuwa tofauti sana.

Lakini ujue hata kwenda sekondari ya seminari haikuwa rahisi. Mara nyingi waliokuwa wakifahulu seminari walifahulu pia kwenda sekondari za serikali.

Halafu kuacha seminari siyo sababu ya performnace tu ila wakati mwingine kutofautiana mawazo.
 
.
Je, kwanini alisoma shule ya msingi miaka 8?
Au kipindi hicho system ya kurudia darasa la nne ilikuwepo?
Na ilikuwaje kuacha seminary na kwenda kumalizia kitaa?
.
Tahadhari: Askofu ambaye ni mshauri mkuu wa chama chako, kwa sasa ana PhD, alisoma shule ya msingi miaka 9 baada ya kurudia mwaka darasa moja. Kuwa makini...
 
Back
Top Bottom