Profesa shida ya nchi yetu ni kutokutii sheria zilizopo na kutojali mipango tuliyojiwekea. Inasikitisha kuona miji mingi nchini ikikua kwa kasi-holela...kila mtu anajenga anavyotaka na hakuna mamlaka inayojishughulisha kuzuia hali hiyo.
Kama ulivyosema kupanga ni kuchagua. Nyie mliopewa nafasi ya kusimamia miji yetu ndiyo mnapaswa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa na kila raia. Pia wizara yako na halmashauri au manispaa zijitahidi kupima, kuuza na kusimamia uuzaji ardhi hasa za mijini kwa wananchi kuliko kuachia kila mtu auze kiholela hali inayopelekea ujenzi holela kuendelea kuwa tatizo kwenye miji yetu.
Hata sielewi kilichowavutia ktk master plan ya Singapore kwasababu kwenye dunia ya kwanza hicho ni kitu cha kawaida yaani safari zote mnazochoma pesa za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa mmejifunza master plan! Hivi hatuna architecture engineer tanzania? Nafikiri tatizo ni serikali isiyokuwa na mipango, ufisadi na uvivu wa kujituma, nchi inazalisha wasomi kibao kwenye kilimo Lakini watu wanakufa njaa hili nalo tunataka watu waje kutufundisha kulima! Ni kitu gani tunachoweza Kama watanzania? Gossip na ngonjera, tanzania itajengwa na sisi watanzania, Hakuna nchi duniani iliyojengwa na wageni.
Why Kigamboni? Nikiangalia Resources zinazokwenda hapo sipati justification.
La swali la msingi, tunataka kufanya Land Reclamation Tanzania? Kwa nini?
Na kama hatuhitaji, kwa nini mlienda kujifunza?
Kuna case moja ya TZ na mikaratusi Australia nayo ilikuwa hivi hivi
1:Muheshimiwa Prof Anna Tibaijuka vipi kuhusu lile ghorofa la kariakoo uliloahidi kuwa litavunjwa kutokana na kutokukidhi vigezo, mbona kimya kimetanda na jengo bado lipo tu?
2: Serikali inamipango gani makini juu ya upangaji miji kwenye mikoa mingine tofauti na Dar ambayo imeanza kuonyesha dalili za kupanuka kwa haraka kutokana na ongezeko la watu au kutokana na kuongezeka kwa vivutio vya kiuchumi ili kuepuka hapo baadae mikoa hiyo isijekuwa na poor planning kama Dar es salaam?
mkuu hapa ndiyo umechoma penyewe; kuna watu ndani ya serikali watafaidika na mradi huu kamwe serikali haitajitoa kwanza wana ugomvi na halmashauri ya wilaya ya Temeke nani asimamie mradi huu. Hii ndiyo Tanzania bwana....Mama Anna Tibaijuka,
Nakushauri kuwa Serikali ijitowe katika huu mradi na iwawachie "real estate developers" wa Kimataifa, wenye uzoefu wa hizi kazi.
Serikali yetu haina uzoefu wa hizi kazi na historia inatuonesha Serikali imeshindwa ku-manage mradi wowote wa maana wa kibiashara. Hata NHC inawashinda ni uozo mtupu, ilhali majumba yalikuwa ya kudhulumiwa watu.
Ikiwa Serikali imeshindwa kuendesha viwanda vya umma, leo itaweza kuendesha project ya "magnitude" ya jiji? Jiulize.
Tusipoteze wakati, tuwawachie wenye utaalaam, na uzoefu wafanye haya mambo, wazo ni zuri, watendaji hatuna, tuna wizi tu Tanzania.
Leo ni zaidi ya miaka 6 tunasikia hii lelemama ikiimbwa tu, hebu ondoeni ukiritimba muwape wenye uwezo, kama hamjui pa kuwapata mnaweza wasiliana na mimi kwa PM.
wameshawaahidi wananchi kuwalipa 35,000 kwa 1 sqm ya mraba, nyumba 700,000 kwa 1 Sqm. sasa kumbe bado hata hawajawatafuta wawekezaji. Juzi Jumamosi wafanyakazi wa mama Tibaijuka wametimuliwa na mapanga pale mtaa wa Kifurukwe, wakurya wamewaambia wasiwaone tena maeneo yao ; mama anadanganywa na madiwani kwamba wananchi eti wameshirikishwa. kila mtu ameshakuwa msanii nchi hii.Hii habari ya mji wa Kigamboni mbona maneno mengi vitendo sifuri? Yaani mpaka sasa ndio tupo kwenye hatua ya kuahidiwa kusaidiwa na watu wa Singapore! Je, ni aina gani ya msaada tunayotaka? What was our plan kabla wasingapore hawajaahidi kutusaidia? What are the timelines of implementation?
aafu pia kwa nini hawawalipi watu fidia stahiki? tatizo ni kwamba kuna uhuni unaendelea usioshirikisha wananchi wa uuzaji wa ardhi, sisi hatuwezi kukubali kuacha ardhi yetu bila kushirikishwa na kulipwa fidia stahiki. tunapenda kufuata vitu vya nje ila utekelezaji waloufanya hao wenzetu hatuufuati.Lakini mh. Kwanini mumeshindwa kuboresha huu mji tulionao sasa hivi na munaanza kutafuta mpya wakati bado hamjachelewa? Tunahitaji tuone mabadiliko hapa tulipo sasa, Hizi sheria ndogondogo za miji zinafanya kazi?
Mtu kuweka maeneo ya mjini vibanda, parking ziko ndani ya barabara ukipita maeneo yote ya mjini sehemu za kupita watu na magari zimepakiwa gari na barabara inakua finyu. Majumba mjini yamekua kama magovu je hakuna sheria ya kuwaagiza wamiliki kuyarekebisha kila kipindi inapofika?
Mh. Tibaijuka,
Ndio hii kwenye link hii -> http://www.ura.gov.sg/skyline/skyli.../URA_Designing our City Supplement_July12.pdf
Kama ndiyo hiyo, nashauri wadau wengine waipakue ili mjadala uwe mpana zaidi. Lakini ninyi wanasiasa ndio wanaochelewesha maendeleo ya Tanzania.