Wee Kilaza, kila mwandishi wa habari mwenye KITAMBULISHO, anakuwa na namba yake ambayo inamruhusu kuingia kwenye Website yao maalumu waandishi wa habari na huko kuna information nyingi sana ambazo anaweza kuzisoma kwa watu kama sisi kuzisikia kwa mara ya kwanza.
Pia kwa watu kama Whitney au Michale Jackson, habari zao nyingi sana waandika hadi kwenye vitabu vilivyo ndani ya Cover ya CD.
Kwa mfano huu wimbo nilisoma habari zake ambazo kweli kweli zinafurahisha sana.
Wakati wanatengeneza album ya MJ ya OFF THE WALL hasa wimbo wa ROCK WITH YOU, mwana dada Brandy Norwood [dada yake Ray J ambaye anasemekana kuwa alikuwa na Whitney kama mpenzi (GIGOLO?)] alikuwa hajazaliwa. Anyway, mwingine atabisha kwa sababu Album imetoka August 1979 na Brandy amezaliwa February 1979 ila ukweli nyimbo zake zilianza kupikwa na akina Mzee Queens Jones miezi kadhaa nyuma kabla binti hajazaliwa.
Wakati Quincy Jones anatengeneza album yake ya "Q'S JOKE JOINT", moja ya Album nzuri sana ya mzee QS, kama kawaida alishirikisha wanamuziki wengi sana. Mwishoni akaja mtoto wake aitwaye KIDADA (wengi walimfahamu baadaye kama Girl Friend wa Tupac Shakur ambaye walikuwa wote Las Vegas siku jamaa alipouawa) na kumuomba baba yake amshirikishe Brandy na Brandy aimbe wimbo wa Rock with you. Mzee akamkubalia Mwanae na kwenye wimbo akaletwa Marehemu Big Daddy aka HEAVY D ili kuja kuongezea uzito. Na ndani ya kitabu, mzee anasema kabisa kuwa inafurahisha kuona Brandy akiimba wimbo ambao waliuandika hata kabla hajazaliwa.
Jaribu kununua CD Original na utapata Information nyingi sana ambazo zinakuwa kwa asilimia kubwa za kweli. Pia Google utapata info nyingi pia ila zihakiki. Pia Youtube, kuna video nyingi sana kuhusu hawa jamaa na maisha yao ila badi zihakiki mara mbili kupata uhakika maana HABARI feki zipo nyingi sana.
Ok, hebu wasikilize Heavy D na Brandy kwenye Q'S Jook Joint. Ukiweza basi itafute hii album kama wapenda mziki poa.
]