Masoud Kipanya ameamka na biashara za wachina

Masoud Kipanya ameamka na biashara za wachina

Mkuu, hapa ninapoishi nilikuwa nanunua mayai tray moja sh 12,000, juzi nimepata chimbo, tray sh 8,000, na naletewa hadi nyumbani, hapo mchina hajatia mguu.
Huyo anaekuuzia 8 elfu nadhani ni mzalishaji anakuku wake bei haiwezi kuwa sawa na yule mlanguzi. Ndiomaana kwenye biashara ili upate wepesi wa kuifanya machimbo mhimu ni lazima
 
Kwa hakika tuna ya kujifunza,
1. Kuna haja ya kuweka mipaka na kuisimamia kati ya maeneo wanayoweza kafanya biashara wazawa na yale ambayo tunawahitqji wageni ili kuimarisha sekta na wafanyabiashara wadogo wa ndani.
2. Kuna haja ya wafanyabiashara wetu kujifunza ubunifu na perseverance ya wenzetu kutoka mabara mengine
3. Tujifumze kufanya partnership na wachina na tusikubali kutumika kama vibarua for short term earning badala yake tufanye partnership nao ili sisi tuwe distributors na wao wake upande wa producers na ikiwezekana wazalishie hapa Tanzania.
 
Wananchi wao wanataka mayai na mchina anauza mayai ya kila mdudu, bundi, kenge, mamba, kuku, kanga, n.k ili mradi tu watu wapate kula mayai. Tusubiri vifo tu.
Tutakula hayo hayo so long tunamudu bei, wabongo chips mayai, viazi havifiki hata viwili na yao la 300 unamuuzia mtu 3000, yaani unaweka faida ya 2000 kwa sahani moja, bora mchina anaweka faida ndogo mzunguko mkubwa, mchina kaiga kwa mchaga.
 
Ni og kabisa ni kama muuza karanga mkulima anaetoa shambani na ww unaenunua uuze upate faida hapo kwenye ushindani wa bei lazima ugaragazwe
MFANO MZURI LAKINI SI HAI. WACHINA wamekuwa msaada mkubwa sana, hatuwezi kuendelea na mabwanyenye wenye ngozi nyeusi.
Soko la nyumba limepanda kwa malanguzi meusi, chumba kimoja ambacho zamani kilikuwa kinaingia kitanda 6 kwa 6 sasa kinakatwa kinajengewa choo ndani unambiwa self na ulipe laki 400,000/- yani unalala na kinyesi kinanukia na unalipa laki nne,.Dalali anamwambia mwenye nyumba nita kupatia tu mpangaji. Waje wachina tumechoka na mafedhuli meusi.
 
Wabongo tunaweka bei zisizo halisi. Siku hizi hoteli haina hadi soda 5,000, bia 10,000 ?

Wachina waje tu , waondoe walanguzi.
Tulikuwa na Fast Jet- Nauli Dar-Arusha 75,000 wazalendo wakaziua na kuleta ndege ya wazalendo nauli ya Dar-Arusha 400,000/= .
Soko huru, kila mtu achague pa kula.
mwendokasi😔
 
Back
Top Bottom