Masoud Kipanya alimaanisha nini kwenye mchoro huu?

Umesema kweli mkuu, huyu jamaa amepoteza mwelekeo, kazi iliyo baki ni kukashifu na kudhihaki, nadhani hii yote ni njaa, anaona bila kuchora katuni za kukashifu na kudhihaki hawezi kupata mafao ya kutosha.
sasa atajimaliza mwenyewe
Wewe hunaga akili

Endelea kumtetea jackline mengi upate mgao wako
 
Simple sn huyo vampire ni mwendazake ,hio draft ni Samia anacheza na sukuma gang ukiangalia kete ni ngoma droo wametaitiana either mama atoe droo au awape sukuma gang ,hio glass ni damu ccm wao Ni kuua,kufunga hawajali kitu
Mkuu angalia vizuri Hilo draft anayetakiwa kusukuma kete ni mama na kwa namna jinsi alivyotegwa kila kete atakayo igusa inaliwa
 
Hii nimetoka kapa,ila kwa wanaojaribu kung'amua wazingatie haya-
-Jamaa ana damu,inaonekana yeye ndiye mtumiaji wa hicho kicnywaji chekundu
-Jino la jamaa la mbele limeacha alama kwenye glass,kwa maana hiyo jamaa anakunywa kinywaji mpaka akatafuna na glass!
-Jamaa ana fegi
-Glass iko ndani ya draft
-jamaa kavaa protecting gear masikioni
-Jamaa ana mashine pembeni
-Kuna kitu cheupe kwenye draft
-Jamaa ni skeleton
-Jamaa inaonekana ana kete nyingi
-Jamaa kakunja nne
-Ni zamu ya maushungi kucheza
-Kila kete atakayosukuma inaliwa
Kiufupi jamaa yuko comfortable kuliko Maushungi,details nyingi ziko upande wa jamaa!
Kazi kwenu
 
Hii nimetoka kapa,ila kwa wanaojaribu kung'amua wazingatie haya-
-Jamaa ana damu,inaonekana yeye ndiye mtumiaji wa hicho kicnywaji chekundu
-Jino la jamaa la mbele limeacha alama kwenye glass,kwa maana hiyo jamaa anakunywa kinywaji mpaka akatafuna na glass!
-Jamaa ana fegi
-Glass iko ndani ya draft
-jamaa kavaa protecting gear masikioni
-Jamaa ana mashine pembeni
-Kuna kitu cheupe kwenye draft
-Jamaa ni skeleton
-Jamaa inaonekana ana kete nyingi
-Jamaa kakunja nne
-Ni zamu ya maushungi kucheza
-Kila kete atakayosukuma inaliwa
Kiufupi jamaa yuko comfortable kuliko Maushungi,details nyingi ziko upande wa jamaa!
Kazi kwenu
Hicho kitu cheupe ni Ganja au Msuba, yani kifupi jamaa ameonyesha ubabe wa hali ya juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uyo skeletoni mwenye uhai ni wana Ccm kindaki ndaki wale waliotengwa ila wananguvu ndani yao, kwamba wameshasogeza kete ya kumbana Mama alafu wamewasha sigara kuashiria ushindi ,Mama awezi kuvuruga drafti maana uyo skeleton atainua mtutu kipanya anamtonya Mama kwamba hii miaka yake iliyobaki aisogeze vyema akikosea imekula kwakeeee atakalishwa mwingine apo ktk kiti
 
Kuna makundi mawili ya CCM yaani ile ya sukuma gang ambayo inawakilishwa na kofia na headphone, kofia imepauka ikiwa na rangi ya kijani na mistari miwili ya njano kuonesha ni CCM inayoendelea kuamini falsafa za mwendazake,ile headphone inasadifu tabia ya mwendazake kuongoza kwa mkono wa damu na bila kusikiliza ushauri wa yeyote yule na ile inayovutwa ni bange ikionesha ubabe ubabe na ukosefu wa hekima na subra na ile bunduki ni mkonowa chuma.Lile draft linaonesha kuwa wote wawili yaani chief hangaya na mwendazake wanatumia CCM ambacho ni chama chao kuendelea kuitawala Tanzania bila kujali maslahi ya taifa bali ya CCM. Na ile glasi ambayo iko juu ya drafti upande wa mwendazake inaonesha jinsi utawala ule ulivyokuwa wa mabavu na hatimaye ukaishia njiani ndio maana glasi imepasuka.Zile kete tatu ni mambo matatu yaliyoitesa awamu ya tano ndio yanaendela kwa awamu ya sita kwa maana ya Katiba mpya,makundi ndani ya CCM na uwanja huru wa kuendesha siasa. Zamu ya mwendazake iliisha ndio maana unamuona chief Hangaya akifikiria acheze vipi kete ili ashinde game. Kipanya anashangaa na yanayoendelea ila yuko upande wa mama.
 
Kete ni nne kwa nne na mwenye zamu ya kucheza ni alovaa ushungi. Kila atakayocheza itakiwa!!

Katika hali ya zamani, katuni hii ingekuwa kesi tayari!!
 
Wauwaji wanywa damu zawatu wahuni wavutabangi waloziba maskio hawaskii lamtu wanamchezesha biushungi mchezo asoujua huku yeye amechoka hanahamu...mpambe yupo kumtia moto!!
 
Inaonesha hao ni wanaccm ambao bado ni wafuasi wa marehemu (skeleton) wakiwa wanachuana na mama ndani ya ccm (draft la kijani) huku wakiwa hawataki kusikia au kuelewa kile anachokisema mama (wameziba masikio), alafu inaonekana wana plan B(bunduki) endapo ndani ya chama (draft) watashindwa. Kwa ufupi wanataka washinde kwa njia yoyote hata kwa kumwaga damu
 
Kila kitu kikitumika blia nidhamu kina madhara, tatizo vijana wengi wanakimbilia mmea kwa pupa...ndio wanaofanya uchelewe kuhalalishwa
We unafikir sababu ya msingi ya pot kuchelewa kuhalalishwa ni hiyo?
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom