Masogange na Melisa kuachiwa huru!!!!!!

Masogange na Melisa kuachiwa huru!!!!!!

Madawa ya kulevya inahusisha mlolongo wa watu wenye nguvu na pesa nyingi sana hapa duniani, yan better kila mtu amaind biashara zake maana no one can win this war!!

Shame!!
 
Tanzania kweli tuna rais???????????
Hii nchi inatia hasira sana lakini sasa tumechoka,kwa ujinga kama huu hakuna atakayevumilia

THEY TAKE ENOUGH FOR THE OWNER TO NOTICE

Mkuu nenda magogoni uchungulie. Yupo rais!!!
 
masogange huru.jpg
WATANZANIA wawili Agness Gerard ‘Masogange' na Melissa Edward wameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg baada ya kutakiwa kulipa faini ya Sh 4.8 milioni (Randi 30,000) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni (R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
"Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa," alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni methamphetamine.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
MASOGANGE NA MDOGO WAKE WAACHIWA
HURU, SO HAWANA KESI.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo,
Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg,
nchini Afrika Kusini imemwachia huru mrembo
huyo baada ya kulipa faini ya R30,000 ambazo ni
sawa na shilingi milioni 4.8 za Tanzania, kubeba
kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za
kulevya.
Naye Melissa Edward ameachiwa huru na
mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi
wowote wa kumtia hatiani.
Habari hiyo kwenye gazeti la Mwananchi
inaeleza kwa urefu:
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa
ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul
Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa
huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba
dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa, Melissa hana hatia
kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza
Masogange, ambaye alimwomba amsaidie
kubeba mzigo huo.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu
kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini
hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la
Agness Gerald na si Melissa,” gazeti la Mwananchi
limemnukuu Kapteni Ramaloko.
Alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa
amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana
ndani ya ndege na Masogange alimwomba
amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa
mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali
zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la
jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru
Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi
30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini
ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini
wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba
zinazobaki amalizie baadaye.
Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha
hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi
atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
Masogange na mwenzake walipokamatwa na
SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za
kulevya aina ya
Methamphetamine, lakini Mahakama juzi
ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya
Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha
Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey
Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi
alisema mzigo walioubeba Masogange na
mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni
kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa
Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS),
Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina
uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5
ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.
Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao
wameachiwa huru baada ya kulipa faini na
mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama
imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine
bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na
kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi
yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi
yeye hana la kusema zaidi.
“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu
inayopitishwa uwanja wa ndege, kama
Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya,
hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi
yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa
huru kwa Watanzania hao, alionyesha
kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu
ndogo.
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo
wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini
ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo
biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema
Nzowa.
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza
kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake
hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu
wanaweza kujitetea kuwa tayari
walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha
Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao
anaweza kukata rufaa.
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata
rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo
ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema
Nzowa.
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati
mapambano ya biashara hiyo yakiwa
yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao
wanaachiwa.
“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu
ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi.
Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa
nchini,” alisema.
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini
tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao
ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la
kuisaidia polisi.
Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni
kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema
mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na
alikuwa amemsaidia.
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa
walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa
wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za
kulevya aina ya Methamphetamine zenye
thamani ya Sh6.8 bilioni.
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi
makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango
kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS
ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa
makubwa duniani.
Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao
zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani
na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere.
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao
ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa
wakati Masogange na Melissa walipokuwa
uwanja wa ndege.
Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo
Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel
Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya
kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na
tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili
mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku
hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya
dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi
kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol)
kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa
kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za
kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya
dawa hizo huko Afrika Kusini.
 
Sielewi mzigo huo, ambao kwanza ulithibitishwa kuwa dawa za kulevya, na wao kukamatwa na watu wenye ujuzi wa kutambua dawa za kulevya, kugeuka na kuwa si dawa za kulevya! Hilo ni swali ambalo wengi wetu tutakuwa tunajiuliza siku zote, na hata atakaporudi huku Tanzania, kila siku watu watakamuona, au jina lake kutajwa, wataendelea kujiuliza swali hilo. Jinamizi la kuhusishwa na madawa ya kulevya litamuandama siku zote, na si yeye tu, bali pia wote wale ambao walishirikiana naye ambao jamii imekuja kuwatambua. Wajue wazi kuwa hakuna kosa ambalo halina adhabu yake. Iko siku haki itatendeka.
 
Mwakyembe awaludishe kazini wale aliowafukuza kwa issue ya masogange, awape na fidia kwa kuwadhalilisha.
 
Agnes Masogange.jpg Johannesburg. Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya. Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.


Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.

"Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa," alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.

Kitabu kamili kipo (www. kila leo .com)
 
Kwa mtindo huu tindikali haitakoma,mahakimu wanaweza kuendelea kuchomwa visu!!!!!

Labda mimi muoga iala naona dalili kubwa sana watu kuanza kufanya vitu hatari sana mitaani humu
 
Huruma kwa Mwakyembe, alikuwa haijui ngoma anayoicheza, ona sasa kageuka mmbea. Alifikiri kina Nzowa wanahangaika bure kwenda south? Wakubwa walikuwa waumbuke live
 
Kwa mtindo huu tindikali haitakoma,mahakimu wanaweza kuendelea kuchomwa visu!!!!!

Labda mimi muoga iala naona dalili kubwa sana watu kuanza kufanya vitu hatari sana mitaani humu

Point yako nini hapa watu wanongelea Agness wewe unaleta habari za tindikali au unataka kusema Masogange yeye ndio muhusika wa tindikali?
 
Kweli kanisa mahakimu wataendelea kutendewa ndivyo sivyo...lakini hii ndy afrika bana hakuna kisichowezekana aisee
 
Huruma kwa Mwakyembe, alikuwa haijui ngoma anayoicheza, ona sasa kageuka mmbea. Alifikiri kina Nzowa wanahangaika bure kwenda south? Wakubwa walikuwa waumbuke live

Wakubwa gani waumbuke live?mbona mnapenda kurukia tu kuna mkubwa gani anae ishi south africa au anae fanya kazi mahakama ya south africa?wabongo na kelele ndio mnazo zijua ndio mana hata haki zenu hamzijui mnabaki kulalamika tu
 
Si nadhani tu labda atarudi tena kuuza au alikuwa hauzi?
 
Sielewi mzigo huo, ambao kwanza ulithibitishwa kuwa dawa za kulevya, na wao kukamatwa na watu wenye ujuzi wa kutambua dawa za kulevya, kugeuka na kuwa si dawa za kulevya! Hilo ni swali ambalo wengi wetu tutakuwa tunajiuliza siku zote, na hata atakaporudi huku Tanzania, kila siku watu watakamuona, au jina lake kutajwa, wataendelea kujiuliza swali hilo. Jinamizi la kuhusishwa na madawa ya kulevya litamuandama siku zote, na si yeye tu, bali pia wote wale ambao walishirikiana naye ambao jamii imekuja kuwatambua. Wajue wazi kuwa hakuna kosa. Hiyo..ambalo halina adhabu yake. Iko siku haki itatendeka.


Nimewaza hadi akili imekauka!! Kauli ya huyo mkaguzi ndo imeniacha mdomo wazi maana mkubwa akisema ndo imetoka
 
Mwakyembe awaludishe kazini wale aliowafukuza kwa issue ya masogange, awape na fidia kwa kuwadhalilisha.

Namhurumia sana mwakyembe maana hiyo contradiction iliyotokea inamfanya aonekane irresponsible wakati ndo kilichotakiwa.
 
Back
Top Bottom