Nchaby
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 797
- 259
Wana Jf habari ni kuwa wale vinara waliokamatwa na mzigo mkubwa wa sembe huko SA wenye thamani ya 6.8 bilion sasa wataachiwa huru kwani imeonekana kuwa mzigo huo haukuwa ni madawa ya kulevya bali ephedrine ambazo haziko kwenye kundi la dawa za kulevya
Habari zinasema ephedrine ambayo inasemekana ndiyo waliyoisafirisha akina dada hao inaangukia ktk kundi la vibashirifu yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
Hivyo basi kesi yao haina nguvu tena na wanatarajiwa kupewa dhamana wakati wowote kutoka sasa.
Source:Gazeti la Raia Mwema Sep.18, 2013
Huu ni mweleka wa hali ya juu sana aliopigwa Dr.Mwakyembe!!
Hakika imeniacha na maswali mengi pasipo
majibu!!!
Ikumbukwe kabla ya taarifa hizo mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya Alfred Nzowa alienda SA kwa kile alichodai kwenda kuangalia kama watanzania hao wanatendewa haki ktk kesi yao!!!
Mimi nikajiuliza hivi wako watanzania wangapi wanaotuhumiwa na sembe China, Hong Kong na kwingineko, kwa nini huyu mkuu aende SA tu?????
Ni Nzowa huyo huyo baada ya kutoka SA alisema kuwa watuhumiwa wamewataja watu waliowatuma mzigo huo na ni mnyororo mrefu sana. Hivyo ataufanyia kazi. Ina maana watuhumiwa walitaja majina ya wauza apples!!!!
Lakini taarifa za nyuma zilisema kuwa watuhumiwa waliingizwa katika chumba cha mateso baada ya kutoonyesha ushirikiano kwa polisi SA wa kutaja wahusika wa mzigo. Lakini baada ya kuingizwa ndani ya chumba hicho walisema kila kitu!!!!!
Najiuliza, inamaana watuhumiwa waliteswa kabla ya kuthibitisha kwa uhakika mzigo walioubeba ndani kulikuwa na nini?
Hakika vita ya kupambana na madawa ya kulevya ni ngumu mno. Wampambanaji ndio wanaomiliki,wanaoratibu,wanaosafirisha,wanaosimamia na kuendesha biashara hiyo ya sembe.
Ni lini Tanzania italivalia njuga kwa dhati tatizo la dawa za kulevya????
========================
UPDATE
========================
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Hukumu

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevyaView attachment 112868
WATANZANIA wawili Agness Gerard ‘Masogange' na Melissa Edward wameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg baada ya kutakiwa kulipa faini ya Sh 4.8 milioni (Randi 30,000) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni (R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
"Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa," alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni methamphetamine.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
- Mwakyembe: Awamu iliyopita aliyetuwezesha kukamata 99% ya madawa ya kulevya aliishia jela
- Jeshi la polisi Tanzania laamua kumfuata Agness Masogange Afrika Kusini...!!
- Polisi aeleza alivyohangaika na Masogange
- Kamanda Sirro: Mbowe jisalimishe Polisi; Masogange, Chid Mapenzi, Wallis Nasher tumewakuta na madawa
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
- Mwakyembe aagiza wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wakamatwe!
- Masogange awataja wamiliki wa mzigo aliokamatwa nao SA
- Hatimaye Masogange amtaja aliye mtuma mzigo wa dawa za kulevya
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!
- Mahakama yashindwa kusoma kesi ya Masogange; adaiwa kuwa mgonjwa
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!
- Dawa za Kulevya: Wema adai Makonda anatembea na Agnes Masogange ndio maana hakamatwi
- Kesi ya Masogange yakwama kusikilizwa tena
- Kisutu: Korti yakataa vielelezo vya ushahidi kesi ya Wema Sepetu. Masogange akutwa na kesi ya kujibu
- Muendelezo Vita Dawa ya Kulevya: Masogange apelekwa kwa Mkemia Mk
- Mahakama yakubali kuutumia mkojo wa Masogange, yasema fomu za mkemia zilifata sheria
- Sampuli ya mkojo wa Agness Masogange wakutwa na Heroin
Hukumu