Ndipo hapo penye siri, anakomolewa kwa lipi?
Kitu kimoja nilichojifunza awamu ya kwanza ambacho kinafanana kwa mbali na hiki, ni kisa cha Nyerere na Tiny Rowland. Ilikuwa kimchezo-mchezo kama hivi na Nyerere akasema harudi nyuma atageuka jiwe, mwisho wake ikawa majuto ni mjukuu.
Ni vyema siri ikawekwa wazi kwani uchumi wetu kwa sasa unategemea sana wawekezaji na mambo kama haya yanawatisha sana wawekezaji.
Kama Manji anauza unga na ndiyo sababu ya kufanyiwa yote haya basi ni bora iwekwe bayana la sivyo basi tunawatisha wawekezaji sana tu, wa nje na wa ndani ya nchi.