Masikini Manji, kabanwa kila kona!

Masikini Manji, kabanwa kila kona!

Yote haya kayataka Makonda,Pole sana mlioajiriwa Quality Group

Kweli kabisa mkuu halafu wanavyojifanya wanamtaja Mungu Mungu kila neno inatia hasira sana hawafikirii ni watanzania wangapi wanaumia,makonda na magufuli vilio vya watu vitawafata mpk siku ya kiama kuweni na huruma kuweni na utu kwa wazalendo inatia uchungu sana
 
Kosa ni nini Hasa la kumhujumu huyu jamaa kila kona siasa zingine hazifai
 
Siku zote akili za maskini ni kumfitini mwenye nacho!! Hela ya Manji mbona ya kurithi hiyo kutoka kwa mababu zake? Kama amekuzidi akili ya kutafuta huna budi kuwa mpole tu! Fitina za kijinga hizi!
 
Arudi India, hicho kipeperushi si ndio kilikuwa kimeanza kampeni ya kupambana na Makonda - Ndo yale yale ya WanaCUF wa DW kutaka kupambana na Magufuli wakati matangazo yao wanategemea kuyarusha kupitia Radio Free, na kilichotokea matangazo yao siku hizi yanakata kata sana hayana ladha, mwishowe hata hao mabosi wa DW Watawashtukia na vibarua vyao vitaota nyasi - Mimi ninachompendea Magufuli siyo mnafiki kabisa, Ukipambana naye, ni lazima naye atapambana nawe back "Battle - battle"
Hao wana cuf wa DW watasababisha tuache kuwasikiliza katika local radio
 
Arudi India, hicho kipeperushi si ndio kilikuwa kimeanza kampeni ya kupambana na Makonda - Ndo yale yale ya WanaCUF wa DW kutaka kupambana na Magufuli wakati matangazo yao wanategemea kuyarusha kupitia Radio Free, na kilichotokea matangazo yao siku hizi yanakata kata sana hayana ladha, mwishowe hata hao mabosi wa DW Watawashtukia na vibarua vyao vitaota nyasi - Mimi ninachompendea Magufuli siyo mnafiki kabisa, Ukipambana naye, ni lazima naye atapambana nawe back "Battle - battle"
Kama unayoyasema ni ya ukweli basi suala la Mkuu wa mkoa wa Dar alishughulikie....... au unasemaje kwenye hilo?
 
Hao watumishi wanaoteseka ni watanzania wenzetu na familia zao wakati Manji hawezi lala na njaa. Tunahitaji kupimwa akili zetu hizi za chuki
Mkuu kuna watu wana akili kama za kuku, wametawaliwa na wivu wa kimasikini ..hufurahia mabaya ya wenzio hata kama hawapati faida yoyote
 
Kwahiyo,huko kwenye viwanda tunaenda kwa kuvuruga kwanza biashara za matajiri,harafu tunatafuta wafanyabiashara wengine,waje wawekeze kwetu?
 
Kama unayoyasema ni ya ukweli basi suala la Mkuu wa mkoa wa Dar alishughulikie....... au unasemaje kwenye hilo?
Makonda ni binadamu na ana matatizo yake - CHADEMA pia ina biff na Makonda tangu enzi za bunge la katiba. Kosa kubwa wanalofanya ni kujaribu kupambana na Makonda anapokuwa amewabana - Mfano kuleta hili suala la vyeti vya Makonda kwa sasa haliwezi kufanikiwa kwasababu hata Magufuli mwenyewe atajua ni mapigo tu na hujuma za watu waliotajwa kwenye orodha ya watumiaji wa madawa na atalipuuza suala hilo hata kama ni kweli - Poor timing
 
Tatizo, hapa wengi wanaochangia hii mada wanasema kulingana na taarifa za magazeti, redio, TV na hata watu kama hii mada inasema chanzo ni wafanyakazi wa QG.

Laiti, kama moyo wa Manji ungekuwa kama kioo mkaangalia live ndiyo mngeelewa.
Sema kwa sababu, mioyo yetu ni siri zetu basi tutapinga kelele sana.

Ila kwa kifupi, serikali siyo wapumbavu kama tunavyofikilia na kuhukumu kwa yanayoendelea.

Naomba, niishie hapa maana ......
 
Back
Top Bottom