Masikini kuwaza kujenga nyumba ya kuishi ni umasikini pia

Kiplayer

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,000
1,571
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
 
Ukitaka kuona Umuhimu wa Kujenga, Kufa alafu uache watoto wako 3 ama 4 kwenye nyumba ya Kupanga.

Hata kama unadhani ni umasikini kuanza kujenga lakini ni muhimu sana Kaka. Tafakari kwenye hilo

Hakuna Baba mwenye gari ila kuna Baba mwenye nyumba.
Wangapi wanawacha watoto ila baada ya mwezi nyumba inauzwa na ndgu au watoto kilipa madeni ya marehemu......
 
Lakini ni mara chache sana kushuhudia Kesi za namna hiyo.

Ukishakuwa Baba, automatic unaanza kuwawazia zaidi Watoto pamoja na kesho yao.

Wacha kuwafanya wategemezi wako wanyanyasike kwenye nyumba za kupanga mara baada ya kifo chako cha ghafla.
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Kusomesha watoto Vs kuwajengea nyuma. Kipi bora zaidi ikuwa umekufa?
 
Nimezunguka sana nyumba za kupanga faida niliyoipata ni kukosa furaha na amani ndani ya nyumba hizo..

Sasa nipo kwangu wanangu wanazunguka ndani ya fensi Kwa furaha mtambuka...

Kupanga ni kuchagua. Over
Maneno kama ya jamaa hapo aongee mtu mwenye uchumi mkubwa sio wakati au wa kubangaiza.
Unapanga masimango kibao, unkaa home si dharau hizi. Hajui kama formula za maisha ziko nyingi. Watu wanajenga kwa kusua sua hata nyumba 5. Kwa mbinde mbinde...

Huyu jamaa wa Masaki na apartment nn hela karithi Hadi na mawazo
 
Kujenga ni muhimu hata Kama hauna Familia.

Then MAZINGIRA ya Biashara kwa nchi Kama TANZANIA sio consistentlce so unaweza kufanyiwa sabotage na serikali ukajikuta unabaki 0-0

Binafsi Napenda kujenga jumba kubwa kibaha kufika 2025 liwe limekamilika .
 
Wote mko sahihi ila pia kujengea mikopo ni ufala fulani maanake labda uwe na mkopo mkubwa million mia ili ukamilishe kbs sio unajenga then unaishia lenta papara miaka mitano...mpk mkopo uishe haya hata hela ya akela inakushinda ya kodi ambayo haizid laki tano kwa mwaka nako inakushinda.
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Uzi huu umeandika ukiwa kwenye nyumba ipi? Ya kupanga au yako?
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Upo sahihi kamili mkuu...😝
Maana kama duniani tunapita, kwanini ujenge njiani..🤔??
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Unaponda walio jenga wakati huo unaishi kwenye nyumba iliyo jengwa na wanaume wenzio hivi una akili kweli?

Kama kujenga hakuna maana mbona hujaenda kuishi juu ya mti?
 
Back
Top Bottom