Umejiandaaje kwa kustaafu?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Mungu anaweza akakupa miaka mingi ya kuishi baada ya kustaafu kuliko hata miaka uliyofanya kazi.

Wakati mzuri wa kuanza kujiandaa kustaafu ni wakati ukiwa kazini na una kipato cha uhakika kinachotabirika.

Najua baadhi ya vijana wanaowaza kustaafu kwa hiari hata kabla ya kufika ule umri wa kisheria, hili linawezekana kama ukifanya maandalizi ya kutosha.

Ili kujiandaa vyema kustaafu, ni vyema kuanza kufikiria yafuatayo;

Ni kiasi gani cha fedha kitakutosheleza.

Je unaweza kujua ni kiasi gani unakihitaji kwa mwezi ili kutimiza mahitaji yako ya kila siku?

Huu ni msingi wa kukusaidia kujua ni kiasi gani kitakutosha ili kuendelea na kiwango cha maisha uliyonayo sasa ivi.

Usiache maisha ya kustaafu yakukute kwa mshangao. Fanya tathimini ya kiasi cha mapato utakayoweza kuyapata ukiwa umestaafu ulinganishe na matumizi yako halisi.

Ni kweli kwamba wastaafu wengi wanapata penseni ya kila mwezi, ila bado kuna haja ya kujiuliza kama kiwango cha pensheni utakayokuwa unakipata kitakidhi mahitaji yako.

Ni vizuri kuishi maisha yanayoendana na hadhi yako hata baada ya kustaafu.

Ni muhimu kupata elimu ya ukokotoaji wa kiasi cha pensheni unachostahili kulipwa, ili kupata picha ya kiasi utakachokuwa unalipwa baada ya kustaafu.

Usisubiri mpaka ustaafu ndiyo ukaulizie, ukijua mapema itakusaidia wewe kuweza kuweka mipango yako sawa sawa.

Kama pensheni haitatosheleza, kuna haja ya kufikiria mapema vyanzo vingine vya mapato vitakavyoweza kukusaidia kujazia pale ambapo pensheni haitaweza kufikia kiwango cha matumizi yako.

Tafakari kuhusu vyanzo vya mapato

Ni vizuri kuanza kuwaza kuanzisha miradi itakayokusaidia kupata kipato ukiwa umestaafu.

Tafakari namna gani ujuzi ulioupata kwa kufanya kazi muda mrefu unaweza kuutumia kukupatia kipato ukiwa mtaani.

Yawezekana ulikuwa mpishi mzuri, unaweza kufungua sehemu ya kula na ukatumia uzoefu wako kupika chakula kitamu ambacho kitavutia wateja.

Jaribu kuwaza kama kuna taasisi ambazo zitakuwa tayari kukulipa ili uweze kuwashirikisha uzoefu wako. Unaweza kupata kazi ambayo watakulipa kutokana na muda uliyofanya kazi au ukapata mkataba wa kufanya kazi kwa miaka kadhaa.

Hii itakusaidia siyo tu kupata kipato, ila itakuondolea upweke wa kuishi nyumbani tu bila kazi.

Namna nyingine ya kuongeza kipato ni kuwekeza kwenye ufugaji, kilimo na aina nyingine za biashara.

Aina hii ya uwekezaji ni vizuri uanze kufanya mapema kabla ya kustaafu, ili uweze kuwa na uzoefu na kufanya tathmini kama ni uwekezaji utakaokuleta tija.

Hii ni kwa sababu ufugaji, kilimo na biashara kwa ujumla wake zina changamoto zake, ukianza kujifunza namna ya kukabiliana nazo mapema itakusaidia kukupunguza uwezekano wa kutumia fedha zako za kiinua mgongo kwenye miradi isiyo na tija.

Unaweza pia kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za biashra.

Aina hii ya uwezekaji unahitaji mtaji mkubwa ila ukijenga kwenye maeneo sahihi, kipato chake ni cha uhakika na kinatabirika. Pia ni uwekezaji unaohitaji muda kidogo wa usimamiaji.

Tafakari kuhusu mahali utakapoishi baada ya kustaafu.

Jinsi ambavyo umri unasonga uwezo wa kuhimili usumbufu huwa unapungua.

Ukiwa na nyumba yako itakusaidia kuepukana na usumbufu wa wenye nyumba.

Ukianza kujenga nyumba mapema itakupunguzia mzigo mkubwa baada ya kustaafu.

Badala ya kuanza kujenga, kiasi cha pensheni utakachokipata baada ya kustaafu kitakusaidia kwenye masuala mengine ya uwekezaji na kukuongezea kipato.

Chagua mahali yatakaokuwa makazi yako ya kudumu, nunua kiwanja na ujenge nyumba kulingana na uwezo wa kipato chako.

Usilazimishe kujenga nyumba kubwa na ya kifahari kama kipato chako hakiruhusu.

Haujengi kwa ajili ya ukoo.

Nyumba inayoendana na uwezo wako haitachukua muda mrefu kuimaliza na hata utunzaji wake utaumudu.

Usisubiri hadi upate fedha nyingi ndiyo uanze kujenga, tafakari namna ya kuanza kujenga kidogo kidogo.

Tafakari kuhusu afya yako

Jinsi umri unavyosonga mbele ndiyo jinsi matumizi yako kwenye mambo ya afya yanaongezeka.

Ni vyema kujiandalia utaratibu wa namna ya kuweza kupata matibabu bila kupata usumbufu wa kukosa fedha.

Kwa zile taasisi ambao wafanyakazi wao wameandikishwa kwenye bima, inakuwa nafuu zaidi hasa kama bima hizo zitaendelea kutumika hata baada ya kustaafu.

Kama hauna bima inayokuwezesha kutibiwa bila malipo baada ya kustaafu kuna haja ya kuanza kufikiria uwezekano wa kuwa nayo.
 
Ahsante kwa bandiko zuri,

Vingi umeeleza vyema kabisa

Kuweka mipango ya kifedha mapema- kuchambua mapato ya kustaafu na gharama zako za kawaida

kuwekeza kwa busara na kufanya akiba ya dharura.

Kuepuka/kupunguza madeni kabla ya kustaafu.
Kutengeneza bajeti inayojumuisha mahitaji yote bila kusahau
(afya) katika chaguzi za bima ni sehemu muhimu ya mkakati wa kustaafu wenye mafanikio..hongera sana.

Tunazingatia na tutaendelea kuzingatia.
 
Usipojipanga utapangwa....Labda upate watoto kama hawa...
 
Attachments

  • VID-20240129-WA0004.mp4
    31.4 MB
Kuna watu hadi miaka hii wanaishi kwa mentality ya kuja kubadili maisha yao wakizeeka au kutumia watoto wao kama backup plan au kutegemea uchumi wa urithi.

Mambo yamebadilika sana. Tunaishi ulimwengu wa capitalism. Unaishi kwa mtaji wako in the form of assets, human assest, cash assets, investment returns, etc.

Kukosa elimu ya namna ya kuendesha maisha katika mfumo huu kutakuja kuwa na repercussion kubwa sana baadae kwa kizazi hiki watapozeeka.
 
Mungu anaweza akakupa miaka mingi ya kuishi baada ya kustaafu kuliko hata miaka uliyofanya kazi.

Wakati mzuri wa kuanza kujiandaa kustaafu ni wakati ukiwa kazini na una kipato cha uhakika kinachotabirika.

Najua baadhi ya vijana wanaowaza kustaafu kwa hiari hata kabla ya kufika ule umri wa kisheria, hili linawezekana kama ukifanya maandalizi ya kutosha.

Ili kujiandaa vyema kustaafu, ni vyema kuanza kufikiria yafuatayo;

Ni kiasi gani cha fedha kitakutosheleza.

Je unaweza kujua ni kiasi gani unakihitaji kwa mwezi ili kutimiza mahitaji yako ya kila siku?

Huu ni msingi wa kukusaidia kujua ni kiasi gani kitakutosha ili kuendelea na kiwango cha maisha uliyonayo sasa ivi.

Usiache maisha ya kustaafu yakukute kwa mshangao. Fanya tathimini ya kiasi cha mapato utakayoweza kuyapata ukiwa umestaafu ulinganishe na matumizi yako halisi.

Ni kweli kwamba wastaafu wengi wanapata penseni ya kila mwezi, ila bado kuna haja ya kujiuliza kama kiwango cha pensheni utakayokuwa unakipata kitakidhi mahitaji yako.

Ni vizuri kuishi maisha yanayoendana na hadhi yako hata baada ya kustaafu.

Ni muhimu kupata elimu ya ukokotoaji wa kiasi cha pensheni unachostahili kulipwa, ili kupata picha ya kiasi utakachokuwa unalipwa baada ya kustaafu.

Usisubiri mpaka ustaafu ndiyo ukaulizie, ukijua mapema itakusaidia wewe kuweza kuweka mipango yako sawa sawa.

Kama pensheni haitatosheleza, kuna haja ya kufikiria mapema vyanzo vingine vya mapato vitakavyoweza kukusaidia kujazia pale ambapo pensheni haitaweza kufikia kiwango cha matumizi yako.

Tafakari kuhusu vyanzo vya mapato

Ni vizuri kuanza kuwaza kuanzisha miradi itakayokusaidia kupata kipato ukiwa umestaafu.

Tafakari namna gani ujuzi ulioupata kwa kufanya kazi muda mrefu unaweza kuutumia kukupatia kipato ukiwa mtaani.

Yawezekana ulikuwa mpishi mzuri, unaweza kufungua sehemu ya kula na ukatumia uzoefu wako kupika chakula kitamu ambacho kitavutia wateja.

Jaribu kuwaza kama kuna taasisi ambazo zitakuwa tayari kukulipa ili uweze kuwashirikisha uzoefu wako. Unaweza kupata kazi ambayo watakulipa kutokana na muda uliyofanya kazi au ukapata mkataba wa kufanya kazi kwa miaka kadhaa.

Hii itakusaidia siyo tu kupata kipato, ila itakuondolea upweke wa kuishi nyumbani tu bila kazi.

Namna nyingine ya kuongeza kipato ni kuwekeza kwenye ufugaji, kilimo na aina nyingine za biashara.

Aina hii ya uwekezaji ni vizuri uanze kufanya mapema kabla ya kustaafu, ili uweze kuwa na uzoefu na kufanya tathmini kama ni uwekezaji utakaokuleta tija.

Hii ni kwa sababu ufugaji, kilimo na biashara kwa ujumla wake zina changamoto zake, ukianza kujifunza namna ya kukabiliana nazo mapema itakusaidia kukupunguza uwezekano wa kutumia fedha zako za kiinua mgongo kwenye miradi isiyo na tija.

Unaweza pia kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za biashra.

Aina hii ya uwezekaji unahitaji mtaji mkubwa ila ukijenga kwenye maeneo sahihi, kipato chake ni cha uhakika na kinatabirika. Pia ni uwekezaji unaohitaji muda kidogo wa usimamiaji.

Tafakari kuhusu mahali utakapoishi baada ya kustaafu.

Jinsi ambavyo umri unasonga uwezo wa kuhimili usumbufu huwa unapungua.

Ukiwa na nyumba yako itakusaidia kuepukana na usumbufu wa wenye nyumba.

Ukianza kujenga nyumba mapema itakupunguzia mzigo mkubwa baada ya kustaafu.

Badala ya kuanza kujenga, kiasi cha pensheni utakachokipata baada ya kustaafu kitakusaidia kwenye masuala mengine ya uwekezaji na kukuongezea kipato.

Chagua mahali yatakaokuwa makazi yako ya kudumu, nunua kiwanja na ujenge nyumba kulingana na uwezo wa kipato chako.

Usilazimishe kujenga nyumba kubwa na ya kifahari kama kipato chako hakiruhusu.

Haujengi kwa ajili ya ukoo.

Nyumba inayoendana na uwezo wako haitachukua muda mrefu kuimaliza na hata utunzaji wake utaumudu.

Usisubiri hadi upate fedha nyingi ndiyo uanze kujenga, tafakari namna ya kuanza kujenga kidogo kidogo.

Tafakari kuhusu afya yako

Jinsi umri unavyosonga mbele ndiyo jinsi matumizi yako kwenye mambo ya afya yanaongezeka.

Ni vyema kujiandalia utaratibu wa namna ya kuweza kupata matibabu bila kupata usumbufu wa kukosa fedha.

Kwa zile taasisi ambao wafanyakazi wao wameandikishwa kwenye bima, inakuwa nafuu zaidi hasa kama bima hizo zitaendelea kutumika hata baada ya kustaafu.

Kama hauna bima inayokuwezesha kutibiwa bila malipo baada ya kustaafu kuna haja ya kuanza kufikiria uwezekano wa kuwa nayo.
Kuna mstaafu mmoja mlevi alipostaff akafungua kiwanda kikubwa msituni cha kutengeneza gongo haramu kinachonuka polisi wakamvizia wakapiga marungu kiwanda chake na msoto ukaanzia hapo.
 
Back
Top Bottom