Mashoga wa Tanzania wana Haki zote kama Watanzania wengine?

ushoga ni chukizo mbele za MUNGU, pia kuna machukizo mengine kama vile kutamani mwanamke asiye mke wako, kutembea naye na mengine mengi

na watu wanaozaliwa na kilema cha mapungufu ya homoni wanadhambi? Kwahiyo ukilema ni dhambi? Wewe kama unaamini kula kwa mkono wa kushoto ni vibaya je ambaye amezaliwa hana mkono wa kulia auawe? We have to find the reason, why ushoga na usagaji upo? Maana scientificaly kuna ushahidi kuwa kuna watu hawana homoni za kutosha.
 
Yesu hakuzungumzia ushoga.... lete mistari usipayukepayuke tu.

haelewi huyo. Hata bible inaonyesha kuwa Yesu hakuwatenga wadhambi, alikuwa nao pamoja mf Maria Makdalena aliyekuwa malaya, pia katika kuwateua watakatifu hakuangalia kigezo cha kazi mf yule mt. alikekuwa fisadi. Ukristu haufundishi kuwatenga watu.
 
EQUALITY FOR ALL!

I am pro-equality for all. All people, regardless of race, gender, religion (even satanists), or sexual orientation, are all deserving of the same rights, and to live life the way they choose, provided that it is not harming another!
 
Tunakataza mtu na dadake kuwa na sex au mama na mwanae kuwa na sex au mtu mzima na mtoto kuwa na sex au baba na binti yake kuwa na sex na yote ni makosa; tufute hayo pia kwa sababu watu wanataka kupeana raha?

kuna ushahidi katika genetics kuwa kuzaa ndani ya familia kuna madhara makubwa. Jiulize, mtoto wa Adam na Hawa alizaa na nani?
 
Mzee Mwanakijiji,
Huwezi kushinda ktk mijadala inayotazama interest za watu wengine. hakuna sababu ya kubishana ikiwa mtu anayetumia swala la penzi kuwa sababu lakini huyo huyo anapinga mama na mwanaye waliopendana kuoana akiwa na umri zaidi ya miaka 18. Sasa ajabu ni kwamba watakwambia sababu za kisayansi lakini sababu zozote za kisayansi kuhusu tendo la kujahiana jinsia sawa hawazikubali na watatumia sababu za madhara yake hata ktk jinsi tofauti kwani nako sii salama. Ili mradi basi tu binadamu tumeumbwa na matamanio na haya matamanio huzua utafiti unaohalalisha kila kitu. Majuzi tu niliona mwanamke huko UK akifunga ndoa na mbwa kwa mapenzi tena kanisani sijui kanisa gani hilo Yarabi! mambo kama haya wasituletee kwetu..

Hivyo hakuna mshindi isipokuwa swala hili ni kuliweka kama nguruwe, mimi Muislaam sili nguruwe na huwezi kunambia tuhalalishe nguruwe ila kama wewe unakula kula usipike nyumbani kwangu wala kuwakaribisha ndugu zangu..Sasa hayo ya kusema niwaache watoto wangu wenyewe waamue wale ama wasile, hilo wanaliona wao kwa sababu yule anayesema niwaache watoto wangu waamue hatakubali kuona watoto wake wakienda msikitini na mimi...

Ubishi huu hauna maana kabisa kwani huyo huyo waziri mkuu wa Uingereza anapinga ndoa za mashoga lakini anataka Tanzania tuwape haki mashoga ambazo kwao hazikubaliki isipokuwa kwa kipande cha karatasi..
 
Umesema kweli kabisa na hapa ndio mgogoro ulipo. Kinachotajwa kuwa ni haki za mashoga hasa TZ ni kuwa tutambue haki yao ya kufunga ndoa. Maana ukweli ni kuwa mambo mengine wanafanya na hakuna mtu anayenda kwenye majumba yao na kuwavuta. Nilikuwa naangalia show Al-Jazeera kuhusu mauaji ya Albino Tanzania kwamba kwa miaka kama 3 wameuawa karibu 60 hivi. Nikajiuliza hivi ni lini tumesikia Tanzania shoga kauawa? hivi kati ya haki za albino kuwa haki na haki za kushoga kufanya kuoana ni ipi haki ya msingi inayovunjwa? Lakini tunatakiwa tuamini kuwa ati haki za binadamu za mashoga ndio zinavunjwa sana lakini siyo haki za albino.
 
Kuzua mijadala na vitisho vya kukatisha misaada nchi maskini kama Tanzania kwa kuzua suala la haki za mashoga wakati wengi wa wenyeji wa nchi hizi wamekosa huduma za msingi kama chakula, afya, maji, makazi, elimu, nishati na kadhalika is immoral, obscene and leaves a lot to be desired, especially given their timing. It should be clear that Obama and the democrats are simply pandering to powerful pro gay-rights lobby courtesy of Hollywood and Wall Street billionaires who funded their 2008 campaign.
 
Umesema kweli kabisa na hapa ndio mgogoro ulipo. Kinachotajwa kuwa ni haki za mashoga hasa TZ ni kuwa tutambue haki yao ya kufunga ndoa. Maana ukweli ni kuwa mambo mengine wanafanya na hakuna mtu anayenda kwenye majumba yao na kuwavuta. Nilikuwa naangalia show Al-Jazeera kuhusu mauaji ya Albino Tanzania kwamba kwa miaka kama 3 wameuawa karibu 60 hivi. Nikajiuliza hivi ni lini tumesikia Tanzania shoga kauawa? hivi kati ya haki za albino kuwa haki na haki za kushoga kufanya kuoana ni ipi haki ya msingi inayovunjwa? Lakini tunatakiwa tuamini kuwa ati haki za binadamu za mashoga ndio zinavunjwa sana lakini siyo haki za albino.
Samahani mkuu, siyo kwamba nakufuatafuata bali mind sets zetu zipo tofauti kidogo.

Ukisema kuwa mashoga Tanzania wana haki sawa na watanzania wengine unakosea.Binadamu wote ni sawa..... huu ni msemo wa jamii nyingi tu, karibu zote lakini kama mnahalalisha sheria za kuwanyima uhuru kundi fulani la binadamu ambao tofauti zao zipo natural na haziaffect uhuru wa binadamu mwingine kuishi maisha yake, hapo tutakuwa tunajidanganya!!
Ushoga,ulemavu,kabila, rangi ya ngozi na utaifa ni vitu ambavyo vipo beyond human control, ni kwamba vipo vimetokea bila wewe kuomba au kujimanipulate ili vitokee.
Vitu kama incest sioni kwanini mtu atazuiwa kumuoa mama yake au dada yake kama wamependana na wameridhia.. let them marry each other!!! ili mradi usiingilie uhuru wa watu wengine kuishi au wasiaffect persue of happiness. Ila huwezi kumuoa mnyama kwa sababu mnyama hana utashi, je, utamuulizaje mnyama kama ameridhia au la?... so that one is just dumb.
Nitaendelea kukusitizia kuwa Mashoga hawana haki sawa na watu wengine Tanzania, hata walemavu na wanawake hawana haki sawa na watu wengine, ubinadamu wao unadharaulika sana kwa level tofauti depending on the family, tribe na vitu vingine.

Thats just a fact, na naweza kukuwekea sheria nyingi tu zinazowanyanyasa mashoga.
Kwa wenzetu, huwezi kuwa na Public building ambayo haina disabled access...it's illegal!
Hata madarasani, first row is a prioritized row kwa disabled..... legally!!!
Sisi bado tupo nyuma sana kwenye hili
 
Mzee Mwanakijiji,
Mashoga hawana haki ya kuwa huru, usitudanganye na maneno yako yaliyojaa politics (or at least falsafa feki)! Mashoga wanatakiwa wawepo "behind bars" wakila sahani moja na Babu Seya! Kama unafikiri kuwa mashoga wako huru kama raia wengine wa Tanzania waambie wajitokeze, wajitangaze hadharani kama hawataishia lupango!
 
Mbona sijasikia mtu amekamatwa ma kufungwa kwasababu ni shoga?

Sana sana huwa wanawaita ma "anti"

Na wengi wao ni mashuhuri tu mjini, sema marafiki zao wengi wao ni wanawake.

Zaidi ya hapo sijaona kama mashoga wanaishi bila uhuru wowote, ama ni uhuru gani unaouzungmzia ulio nao wewe ambao hawana?

Kila jamii ina level yake ya kimaendeleo,na hivyo hakuna anayemwingilia mwingine, ama sijasikia mauwaji ama ubaguzi hapo bongo kisa mtu ni shoga.

Kwenye kumbi za starehe, everywhere wako, ni wao wenyewe wanachagua pa kwenda.

Kwenye nyumba za ibada mara nyingi hawako,labda wale wa "down low"

Ama wale ambao ni waanglikana kama sikosei.
 
Thats just a fact, na naweza kukuwekea sheria nyingi tu zinazowanyanyasa mashoga.
Kwa wenzetu, huwezi kuwa na Public building ambayo haina disabled access...it's illegal!
Hata madarasani, first row is a prioritized row kwa disabled..... legally!!!
Sisi bado tupo nyuma sana kwenye hili

Wewe unaangalia usawa wa vitu fulani fulani ambavyo mtu anasema ndivyo alivyonavyo. Ushoga siyo kitu ambacho mtu anaweza kudai kuwa amezaliwa nacho - hakuna ushahidi wa kisayansi conclusively kuwa iko hivyo na hata ungekuwepo wenyewe hautoshi kuifanya jamii kutolerate. Kwani wapo watu ambao they genetically disposed to anger, na wapo wanaoamini kuwa psychopaths wana some form of genetic au neurological disorders na kwamba wanavyovifanya vinatokana na vitu ambavo ni nje ya uwezo wao je tukubali kuwa sasa pyschopaths walindwe?

Nisichokubali ni kuwa kuna watu wengine wanataka kuwa na haki zaidi ya binadamu wengine. Ndio maana taifa letu halikwenda huko na hata hizo nchi nyingine ambazo unafikiri ziko mbele sana ya haki tunaweza kusema hawana haki kama sisi. Kwa mfano Marekani, ndoa ni ya mume na mke mmoja tu; inakuwaje kama watu zaidi wanataka kuoana kwenye ndoa moja kama ilivyo TZ? Je Tanzania iende na kuwaambia Wamarekani kuwa hawaheshimu haki za 'binadamu' kwa sababu hairuhusu Waislamu au mtu mwingine yeyote ndani yake kuoa /kuolewa na mume/mke zaidi ya mmoja? Jaribu kuwaambia Wamarekani kuwa hiyo ni "haki" ushangae!

Hata huko Marekani kuna sheria zinazokata vitendo vya ushoga - sodomy laws. Na sheria hizo zipo na ziko effective. Na sheria nyingi za homosexuality zilikuwa ndani ya hizo na hata miaka kama arobaini tu nyuma homosexuality ilikuwa ni sehemu ya magonjwa ya kiakili au na awapo ambao wanachukulia expressions zake kama Sexual Identiy Disorders. Na wapo wanaojaribu kubadilika na wapo ambao wameacha hiyo - Ann Heche mfano wa haraka haraka.

Kwamba jamii zina standards tofauti tofauti hilo si tatizo kwani ndivyo ilivyo. Hakuna jamii zinazofanana duniani na kuamini kuwa tafsiri ya wengine kuhusu nini permissable basi lazima tukikumbatie bila kuhoji au kujaribu kuelewa ni udhaifu wetu. Leo hii, Wamarekani na sehemu nyingine wanahii movement ya die with dignity au wengine wanaita 'assisted suicide'. Wao wenyewe hawajakubaliana na ni nchi kama Netherland na Uswisi zinazo - siyo Marekani, Canada, Ufaransa wala Uingeza ambazo zinazo. Na sisi hatuna. Sasa wakubwa wakishafikia mahali kuwa wasema vitu hivyo ni sawa na sisi inabidi tufuate?

Unapozungumzia haki - unazungumzia vitu ambavyo kila mtu anastahili kutokana na utu wake na kwenye huo utu jamii inaamua ni vitu gani proper na ni haki zipi za msingi. Nimesema kuwa Katiba ya TAnzania inamlinda kila Mtanzania that is a FACT. Katiba yetu haibagui mwanamme au mwanamke n.k

Kusema kuwa 'incest' ifanyike tu ndio eventual outcome of a flawed reasoning. Unaamini kuwa hakuna mipaka na jamii haiitaji kujiwekea mipaka alimradi watu wanapeana raha. Hao wanaosema incest ifanyike tu sidhani kama wao wenyewe wako tayari kulala na mama, baba au dada zao. Jamii inayo mipaka yake na familia zinazo mipaka yao ya yale ambayo mtu anaweza kufanya. Hata mtu abaye ni permissive atajikuta anamlinda mtoto wake vile vile asidhurike; atuamuonya na kujaribu kumsaidia. Hatumwachi mtu mlevi awe mlevi tu kwa vile ni starehe yake. Jamii inayo haki ya kujiwekea mipaka na jamii hiyo ikishawishiwa kwanini mpaka uhamishwe basi ni jamii inaamua. Hiyo ni haki ya jamii.
 
Jiulize, ukimuita mfanyakazi mwenzio faggot! au nigger!.... nini kitakutokea kazini?
Hakuna Taifa lolote lililomkataza mtanzania kuweka mipaka ya haki za kijamii. Ila, usitangazie watu kwamba Tanzania watu wote ni sawa kikatiba, ila wanaume wakibusiana na kupata denda kwenye bustani wanahatarisha maisha yao kwani wanaweza kwenda jela kwa homosexual relationship au kupigwa na kutukanwa kwa sababu mila zetu zinakataza.

Bi. Clinton hajawakataza kuchagua mipaka ya haki, ila kama mnataka misaada, kuna masharti amewawekea, kwa hiyo msijidai kuhalalisha haki za gays based on constitutionalty while mnatunga sheria za kuwakandamiza na hamtungi sheria za kuwa protect.

Whether homosexuality is natural or not, you be the judge.
 
Jiulize, ukimuita mfanyakazi mwenzio faggot! au nigger!.... nini kitakutokea kazini?

Well inategemea, watu wataona kuwa ni kosa fulani lakini hawatampeleka mahakamani kwani atadai analindwa na Katiba - free speech.

Hakuna Taifa lolote lililomkataza mtanzania kuweka mipaka ya haki za kijamii. Ila, usitangazie watu kwamba Tanzania watu wote ni sawa kikatiba, ila wanaume wakibusiana na kupata denda kwenye bustani wanahatarisha maisha yao kwani wanaweza kwenda jela kwa homosexual relationship au kupigwa na kutukanwa kwa sababu mila zetu zinakataza.

Watanzania wote ni sawa kikatiba that is a FACT; siyo mimi natangaza. Sasa kuwa "sawa" haina maana hakuna mipaka hata hizo nchi ambazo zinasema watu wako "sawa" bado wana mipaka yao.

Bi. Clinton hajawakataza kuchagua mipaka ya haki, ila kama mnataka misaada, kuna masharti amewawekea, kwa hiyo msijidai kuhalalisha haki za gays based on constitutionalty while mnatunga sheria za kuwakandamiza na hamtungi sheria za kuwa protect.

Whether homosexuality is natural or not, you be the judge.[/QUOTE]
 
Tena juzjuz nilisikia bbc swahili,wakifanya mahojiano na baaz ya uganda,kuwa kuna baadh ya shule zinazomilikiwa na wagen,wanafundisha watoto ushoga,wanawaambia jambo la kawaida tu kua shoga
 
Naona Mwanakijiji hujaelewa Hoja za Cameroun na Obama, wanachotaka wao kuona Mashoga wanaoana na wanatembea freely wakiwa na Mabwana zao. Ndoa zao zikubalike kwenye Jamii kama ndoa za wengine, ni kitu kisichowezekana kwenye Utamaduni wetu wa Kitanzania. Movie inaendelea :lol:
 
SOBY,

Nafikiri kuna tofauti kubwa sana kati ya kutukana mtu kwa neno lisilokubalika na kuitafuta haki ya wahusika. Ukiwmita mtu Shoga ina maana tusi hilo limetokana na MATENDO yake...Na tuseme ukweli ya kwamba mtu mweusi leo akiitwa Nigger ni tusi kwa sababu leo hii sii mtumwa tena lakini tuliitwa Nigger kutokana na Utumwa. Lilikuwa neno ama jina lililotumika tulipokuwa watumwa na hatukuona ubaya wowote wakati ule..

Ila baada ya kupiga marufuku UTUMWA - Yaani udhalilishaji wa mtu mweusi ktk utumwa ndipo hata neno hili limeharamishwa matumizi yake maana sii watumwa tena. Lakini njoo kwa Mashoga wao wanapenda tena wanaona Pride kuitwa MASHOGA na wanajitambulisha kama washoga kama babu zetu walipokuwa utumwani waliamini Utumwa umebarikiwa na Mwenyezi Mungu as if established by decree of Almighty God..Na hapa ndipo watu wengi huweka shaka kubwa ktk vitabu vya dini vilipohalalisha Utumwa.

Sasa Utumwa uliharamisha kama sii haki ingawa baadhi ya babu zetu waliamnini ni jambo la Muingu kumtumikia mzungu, sasa inakuwaje kuharamishwa Ushoga iwe kuwanyima haki Mashoga ambao wanaona Pride kufunga ndoa. Tena kuna baadhi ya watu siku hizi wanasema bora utumwa ungeendelea tukazaliwa nasi Ulaya kuliko adha tunazopata leo Afrika.. Hizi zote ni wishful thinking ambazo zinatazama picha kwa uzuri wake pasipo kuitafuta message iloyotolewa na picha hiyo..Nafikiri hili wasanii wanaweza kulieleza vizuri zaidi..

Mwisho, Mashoga kwetu hawana sababu ya kulalamika hata kidogo. Binadamu wote ni sawa kwa maana ya mahitaji muhimu na kuwa treated sawa lakini usawa hautokani na matamanio, kesho wale Mapadre na mabaradhuli nao watakuja dai haki ya kwa kutopenda kuoa ama kuwa ktk relationship ya kimwili ila Urafiki usiohusioana na kitendo..

Ni ajabu kubwa sana binadamu sote tunatakiwa kuheshimu mawazo ya mwenzko na kuwapa haki hiyo lakini inakuwaje sisi tunaposema Ndoa ni baina ya mwanamme na mwanamke - Mashoga hawataki kukubali... Na isionekane wao hawaheshimu maamuzi yetu sisi isipokuwa yao ndio yawe yenye maana zaidi?..Haya wengine ndio hivyo tayari wanasherehekea na wanyama basi ili mradi hili neno Mapenzi - LOVE linatumika kwa tafsiri zetu zenye malengo ya kupata kitu fulani na sii mapenzi ya kweli kutoka moyoni. Mimi nadhani haki hizi sasa hivi zimepitiliza, zamani ilikuwa Usinifanyie kibaya ambacho wewe hutapenda ufanyiwe ndio msingi wa kuitafuta HAKI na Usawa wa binadamu, siku hizi - Nipendacho mimi usiniwekee masharti, nayo imeongezwa ktk haki za binadamu.
 
Umeongea vizuri sanaaa,huyo anayesema suala la haki za mashoga kuheshimiwa ana harufu ya ulaya ulaya,huu ndio ukweli kabisa.Mimi nafikiri tunge jadili ni vipi tabia ya ushoga inaweza kukomeshwa ktk jamii zetu,ni vema wanasayansi pamoja na kutambua sababu za watu kuingia kwenye ushoga ni vema sasa wakatafuta dawa ya kuwatibu,ikiwezekana ipatikane chanjo(tehe tehe tehe tehe) vinginevyo vijana wetu ambao sasa hivi wanavaa suruali kata 'K' wataanza sasa kuvaa kata Goti alafu mambo yataharibika muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom