Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
MMKJJ,
Mi nimependa uthubutu wako kuanzisha mada hii. Imefika wakati Watz tuwe na uthubutu wa kujadili hata yale ambayo mchana tunayapiga vita kwa nguvu zote lakini usiku tunayashabikia utadhani siyo siye!Ushoga/usagaji mbona kila mtu anajua hata wale wanaojidai kuwapinga nao huwachukua? Mashoga wenyewe huwataja hata kwa majina....sasa tunachojifanya kukataa ni nini? Kuna mangapi ni kinyume na maadili, mila, desturi, dini na bado yanafanyika?Tuyaorodheshe?
1. Ufisadi/wizi/rushwa - kila dini inakataza lakini bado yanafanywa.Mbona hatujawatenga na kuwanyanyapaa?
2. Tigo - mbona watu wanafanya uchafu huu, mbona hawajatengwa na hata wenye kufanya wengine wanajulikana.Waume wamekimbiwa na wake zao shauri ya uchafu huu; wanawake nao wapo wanaoshabikia kufanyiwa ujinga huu na inajulikana.
3.Uzinzi - mbona watu wanafanya tena sana.Dini zote zinakataza lakini bado - mimba za nje ya ndoa zinapatikana kila siku zinatoka wapi? Vitoto vidogo vinaingiliwa kinyume na maumbile kila siku, ni dini, mila gani zinaruhusu haya?
5.Ongezeeni list.
Kwa kifupi, binadamu huwezi kujidai u mtakatifu maadam hujafa.Kuna mtu kauliza, ikiwa mwanao atakuja na kukuhabarisha 'miye ni m##nge au msagaji" utammfukuza?
Tukijifanya tunatetea dini zetu, yuko wapi hata mmoja hapa asiyevunja sheria za dini yake? Wako waislam wanakula kitimoto kwa kwenda mbele, wako wakristo nao wanaovunja miiko ya dini yao.......ACHENI IZO BANA!
Sitetei ushoga lakini sipendi unafki wa watu hapa au kwenye majukwaa ya siasa.
Unachosema hapa ni kweli kabisa. Mashoga hapa Tanzania yana haki kama watanzania wengine. Yana haki kama wezi, yana haki zaidi kuliko wafungwa (kwa kuwa wafungwa hawapigi kura) yana haki ya kuwa viongozi haki ya kupiga kura etc etc. Issue ni kuwa kama mtu anafanya kosa haina maana kuwa kosa lake ni halali, lakini kuna makosa yanaweza kuvumiliwa na makosa ambayo hayawezi kuvumiliwa. Nadhani don't ask don't tell policy ni bora, kuliko kuanza kufikia hatua kama ya Uingereza. Tuna utamaduni na mila zetu, ambazo zipo kama walivyonazo waingereza na watu wa ulaya.