Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #41
MKJJ,
Ni kweli kuwa katiba yetu inawapa uhuru sawa raia wake wote pamoja na mashoga kama akina auntie Moody. Je ni kweli kuwa katiba yetu inatambua uwepo wao?? Ninavyofahamu TZ hatujawahi kusema popote kama tunatambua uwepo wa jinsia hiyo ya mashoga. Hii ya kusema kuwa rais wote wanahaki sawa haina maana kama katiba haitambui uwepo wao. Katiba nafikiri inatamka kuhusu uwepo wanaume, wanawake, watoto, vijana, wazee, vilema (may be mashoga wako huko) na posssibly albinos. Je una maana mashoga wakijamiiana ni sawa kwa sheria zetu?? Nakumbuka miaka michache iliyopita nilisikia kama kuna sheria imepitishwa ZNZ ambayo haiwatambui mashoga na wakikutwa ni lupango miaka 25.
Katiba haitambui uwepo wa Zeruzeru je Zeruzeru hawana haki kama 'mtu'? Katiba haitambui uwepo wa walevi je walevu hawana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa "utu" wao. Katiba inatumia neno "kila mtu" it includes everybody and excludes no one.