Mashoga wa Tanzania wana Haki zote kama Watanzania wengine?

Mzee Mwanakijiji said:
Binafsi ningependa kusikia Uingereza na Marekani wanaunganisha haki za kisiasa (political and civil rights) na misaada. Kwa sababu hapo wataigusa na Tanzania hili la "haki za mashoga" halituhusu. Maana kama kuna haki zinavunjwa sana Tanzania ni hizo.
Ndiyo hapo ukiwaambia hiyo misaada itizameni kwa makini, wao pamba masikioni...

Kwa ujumla serikali ya CCM wana act kama waafrika halisi, yani wasiopenda maendeleo ya wenzao!

Mambo yote wanayokubaliana na hao mabepari kutuletea ni ya kuturudisha nyuma na kutufanya watumwa kwenye nchi yetu wenyewe!

Huwa nahisi kuwa CCM kwamakusudi hawataki wananchi waendelelee na kuwa na ufahamu zaidi na kujuwa haki zao simply kwasababu hawataki kuachia madaraka.

Kwahiyo hata kama wakiambiwa wananchi wote wapewe sumu kasoro watoto zao wanaweza wakakubali hawa!
 
Mwanakijiji mimi huwa ni mpezi mkubwa wa article zako, i wish watanzania wangukuwa na uwezo kama wako wa kufikiri especially viongozi wetu basi tusingesikuwa na shida hizi lukuki, sijui tatizo nini??

inashangaza kuona kiongozi mtu mzima sijui anaupungufu wa akili (membe, shein,) na wengine wakitokwa na mapovu kuwa kama misaada yao basi ushonga kwetu no wakati ukienda zanzibar wamejaa tele njoo dar mpaka madisko wapo tena wanahaki zote tena hawajawahi buguthiwa kama dada zetu (dada poa). hawa viongozi wetu wanashindwa kutofautisha kati ya "haki za mashoga" na "ndoa za mashoga"

kuna vitu muhimu sana kama political rights na civil rights ndio tungezipa huo msisitizo na si ushoga!
 
Mwamkili said:
kuna vitu muhimu sana kama political rights na civil rights ndio tungezipa huo msisitizo na si ushoga!

Tatizo liko kwa nani hapo?

Kwa upande wa viongozi wetu, madai hayo yatakuwa ni sawa na "kunoa panga la kukata shingo yako"

Ni swala ambalo halina manufaa kwa pande zote, only kama upande wa viongozi utawakosea hao mabwana zao,then kwa unafiki wanaweza kusapoti movements kama hizo.

Tofauti na hapo ukweli ni kwamba we're stuck, mwananchi hana metetezi wa kweli kati ya hao anaowatumainia, yani serikali na wafadhili...thats the way i see it!

"Nimejifunza kukubali mambo nisiyoweza kuyabadilisha"!
 
MM. Umenishangaza sana kwenye suala hili la shinikizo la haki za mashoga toka Uk. na USA. Kama nimekuelewa vizuri, unasema tusistuke na pia hakuna haja ya kukereka kwa sababu shinikizo hilo halituhusu kwa kuwa sheria zetu haziwabagui mashoga. Loooh! MM. Ukumbuke kuwa siku zote, kuna kanuni isemayo, 'mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake'. Vivyo hivyo kwa mtunga sheria, 'hujipendelea'. Sitarajii kukuta serikali yoyote kupitia baraza lake la kutunga sheria au bunge, ikitunga sheria ya kujikandamiza yenyewe. Nikirudi kwenye shinikizo la ushoga ni lazima tushtuke na tukereke. Sababu hasa ni jambo lililo kinyume na maumbile ya Mwanadam. Sheria zetu zipo wazi, ukipatikana na ushahidi kuwa umemuingilia mwanamme/mke kinyume ya maumbile, adhabu yake miaka 30 jela. Kutokuwa na uwezo wa kufatitilia sheria sio kigezo cha kuwa 'ruksa' kuvunja sheria kwa kuwa hatuna uwezo wa kuilinda sheria ifanye kazi. Hao wanaotushinikiza wananatujua pengine kuliko tunavyojijua! Pia wanajua wanachokitaka kwetu ni kipi. Wanataka uhalali wa kisheria. Pasiwe tena na tuhuma au pingamizi katika ndoa. Unaowa/unaolewa kisheria huku tukijua wazi mapema, kweupee, mbele ya halaiki na wageni waalikwa kuwa wanandoa hawa watakwenda kufanya mambo kinyume na maumbile. Jamani tuwe waangalifu na makini, hasa tunapoingia mikataba ya kisheria na hawa watu. Tusije kosea kama kwenye mikataba ya madini/umeme nk.


Umesoma makala ya mwanakijiji vizuri? hili ndilo tatizo la watanzia wengi mnasoma hamuelewi!! vivyo ndio nyie mnatupeleka kwenye mikataba mibovu. nakuakikishia ndugu yangu wewe sio tatizo lako ni mfumo wa tanzania na shule zake zinatuletea watu kama nyie wavivu wa kusoma vitabu, kuchambua kuelewa maudhui.

mwanakijiji hazunguzii sheria, maana sheria zipo na hazifuatwi na hao wenye dola, lini umewahi kuona shoga kakamatwa na polisi na tunakuwa nao kila siku kwenye madisko? mbona wanaokamatwa ni akina dada zetu(dada poa), kama hawana mbinu na vifaa kwa nini wasitengeneze kitengo maalumu au wakawapa baadhi ya polisi utaalamu wa kuwakamata na kuwafikisha kwenye mahakama ili hiyo sheria unaisema ichukue mkondo wake?

dola linachojua ni kupiga marufuku watu kuandamana iwe vyama vya siasa au asasi mbalimbali, na kujiaandaa na mabomu ya machozi na magari ya kuwasha? kwani haya magari yalikuwepo jamani si yaliletwa wakati wa mkapa? dola iliona umuhimu wa kuiongezea polisi vifaa? kwa nini sasa wasiwaongezee ujuzi na vifaaa vya kuwakamata mashoga?

mwanakijiji amekupa mfano wakati wa serikali ya clinton walivyoweza kuongezea vipengele kwenye sheria zao za ndoa, hapa kwetu zipo na huko pia zipo mbona tunao watu mitaani mwetu wanaishi mume na mke wote wa jinsia moja yaani wanaume? mbona hawajakamatwa? ukiwashogelea watakuambia ni marafiki? utamzuia rafiki angu kulala kwangu hahahaaaaa

wantanzaia- wadangayinka
 
Wanaume kuoa wanawake na wanawake kuolewa na wanaume its a taboo, tumezaliwa na tumeona ni kama utamaduni, hakuna ushahidi wa kisayansi unao-prove kuwa ndoa ya mwanamke na mwanaume ipo biologically.
Kama tunaheshimu tamaduni, mbona kuna customs na traditions ambazo tumezibadili mfano ukeketaji, fashion styles, songs, language e.t.c?
Kila mwanadamu ana haki ya kuishi, hata kama ni kilema, masikini, muumini wa kishetani, au mtuhumiwa.

Hatujui kutofautisha matter of pure opinion and not matter of fact. We believe in things without facts and logics.

Kwa huyu mdudu wa dependency theory of development the law will be established because we are poor and we dnt want to change.

Dont u knw that kuna watu wengine wamezaliwa na kilema cha kupenda jinsia moja? Im not a gay but i thnk its not fair to hate them, mbona wasagaji hamuwasemi sana? Kinachoniuma ni kuwa kuna mambo mengi hapa tanzania ya kijinga kuliko haya tunayoyakazia misimamo.

''IF U WANT TO CHANGE, U HAVE TO UNDERVALUE UR CULTURE'' - by Socrates!
 
hivi kwenye ndoa za ushoga kuna masuala ya posa, mahali, mshenga, kitchen party,send off n.k?........ mambo ya baba nimepata mchumba nataka kuolewa?
 
hivi kwenye ndoa za ushoga kuna masuala ya posa, mahali, mshenga, kitchen party,send off n.k?........ mambo ya baba nimepata mchumba nataka kuolewa?
Duh!

Kama hizo ndo haki ambazo wanazozungmumzia mbona itakuwa shughuli!

Hii itakuwa inaingiliana na cultures, na kama nilivyosema, sisi hatujafikia hatua hizo kwasababu hata wao wanachopingana ni kuhusu the "sanctity" of the marriage.

Yani kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke, period!

Wabadilishe kwanza za kwao, na wakimaliza ndo wajaribu kwetu, kama kwao kuna wanaopinga, inakuwaje wawalazimishie wasiokuwa wa kwao?
 
Hii haina ubishi kabisa kuwa Mashoga Tanzania wanapeta.

Nilipata habari kuwa miezi kadhaa hapo Tabora mjini, kulikuwa na Harusi na wakaja Mashoga (Ndugu).

Walifanya vituko sana kama kubusiana nk nk jambo ambalo hata Mke na Mume kwa Tabora hutaona hadharani.

Watu waliangalia na hakuna mtu aliyerusha jiwe ingawa UKAKASI ulikuwepo.

Maria Salome, wimbo wa Saida Karoli watu wengi waliucheza na kuupenda ingawa humo ndani kuna maneno yamekaa kama kuwatetea Mashoga "......... Khalidi Na Philemone walipendana na mapenzi yao yakadumu, wenye wivu wajinyonge."

Hebu angalia kuanzia 3:05.............

 
Last edited by a moderator:
Hawana haki kama heterosexual. Kuna stigma kubwa sana against mashoga, iwe politica au social stigma na wanaochangia wengi ni politica and religious figures, wakijifanya kuongea kwa niaba ya watanzania wote.
They are molested and categorized and segregated jus for who they have sex with, shida ambayo wewe huipati.
Mbaya zaidi wakiamua kwenda kufungua kesi bado watatukanwa tena for daring. Soma hapa:
Homosexuality is not only openly condemned by powerful social actors such as church leaders and politicians but is also illegal.

In his open letter to the Anglican Diocese of Central Tanganyika Mdimi denounced the violent prosecution, hate and ostracism that gay Tanzanian had to face (Mdimi, 2007). Anyamele mentioned in his 2005 report on Sexual minorities (recognized and co-funded by the world bank) that Tanzanian Homosexuals were being segregated professionally and socially and mentioned that ‘adverse comment' were made regularly against homosexuals by senior politicians, including head of state. (Anyamele 2005)

Sexual activities between men are punishable of 14 years in prison (no mention of inter female sex) and celebration of a gay union in a way that approximate marriage is punishable of 7 years in prison (section 154 to 157 of the Tanzanian Penal code).

 
Sijui ni kwanini watu wanashindwa kutoa jibu jepesi kabisa kwa Uingereza na Marekani kuwa katika Tanzania mashoga wanazo haki zote ambazo Watanzania wengine wanazo. Tena hakuna nchi ambayo ina uvumilivu sana wa mashoga katika Afrika kama Tanzania kwa sababu tayari katiba yetu imewawekea ulinzi kama ulivyo kwa Watanzania wengine. Kwamba 'kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Na hii "kila mtu" inajumlisha watu wa dini tofauti, makabila tofauti, rangi tofauti naam hata mwelekeo wa jinsia tofauti.

Shoga wa Tanzania anazo haki zile zile ambazo anazo mtu mwingine:

a. Ana haki ya kupiga kura
b. Ana haki ya kuishi
c. Ana haki ya kufanya kazi (wengine wameshika hata nafasi za juu tu nchini)
d. Ana haki ya kuishi popote (shoga halazimishwi na jamii kuishi mahali asipotaka yeye)
e. Ana haki ya kupata elimu (wapo wanasoma na wamesoma kwenye shule na vyuo vyetu)
f. Ana haki ya kusafiri ndani na nje ya nchi
f. Ana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yake (na wametoa hata kama yanawaudhi wengine - hatujaenda kuwafunga watu kwa kutoa maoni ya kutetea ushoga)
n.k

Kwa hiyo - maelezo ya Cameron na Obama hayahusu Tanzania na sioni sababu kwanini Watanzania wanashtuka sana au kukereka. Jibu letu ni jepesi - mashoga wanazo haki zile zile za binadamu ambazo wananchi wengine wanazo na hakuna sababu ya kutengeneza kundi jingine la haki nje ya zile ambazo kila Mtanzania anazo.

Kuondoa ushoga kama kosa la kihalifu (decriminalization of homosexuality)
Sasa wanapozungumzia "haki za mashoga" wakati mwingine wanaaminisha kuwa tuondoe kwenye sheria zetu ushoga kama kosa (a criminal offense). Sasa hili siyo jambo la Marekani au UK kwani masuala ya makosa yanaamuliwa na jamii husika na kwa hoja walizonazo. Japo sheria ipo Tanzania haitekelezi sheria hiyo na kuanza kwenda kila nyumba na chumba na kuwafunga watu ati kwa vile wameonekana wameshikana mikono au wameingia chumba kimoja. Hivi kweli kuna mtu anafikiria tunaweza kuzitekeleza hizo sheria kwa kila mji, mkoa, nyumba na mitaa? Huo uwezo uko wapi? Halafu kati ya matatizo yetu yote ambayo tunayo leo kama taifa hili la kukamata mashoga mbona halipo? Hatujasikia watu wanaenda na viboko au kuwacharaza watu kwa vile ni mashoga. Watanzania wamekuwa wavumilivu mno na wengi wamekubali kuwa hilo ni suala la mtu binafsi tena mtu mzima na Katiba inawalinda watu hao pale inaposema kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa faradha yake.

Vinginevyo, itabidi tuunde kikosi maalumu cha Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa au hata Magereza ili kufuatilia vitendo vya ushoga (Anti-Homosexuality Police Squad). Sasa kama suala ni kuifuta sheria kwa vile haitekelezeki au kuibadilisha ili ishughulikia makosa ya sodomy, molestation n.k (ambayo tayari yako chini ya SOSPA 1998 as ammended) basi ifanyike hivyo.

Ukweli ulio wazi ni kuwa anti-homosexuality laws are outdated and unforceable. Zipo sheria lakini hatuwezi kuzitekeleza au kuzisimamia na labda sisi wenyewe wananchi kama kweli tunakereka sana na ushoga kuliko mambo mengine tuwasisitize polisi wakusanye kodi zaidi ili waanze kuwa na vikosi vya kuangalia vitendo vya ushoga kwenye mahoteli.

Vitendo vya ushoga ni zaidi ya vile vya watu wa jinsia moja
Wengi ambao wanakereka na vitendo vya ushoga na kuona ni vya kuchukuliwa hatua hawajui kuwa sheria hiyo hiyo inakataza vitendo vya mwanamme kumuingilia mwanamke kinyume na maumbile (a.k.a tigo). Je, tuko tayari kuona na wanaume na wanawake wanaufanyiana hivyo -hata kwenye ndoa- wanafikishwa mahakamani kwa kuvunja sheria. Tutawatambuaje na kuwafuatilia vipi?

Wengine wanafikiria kwa mfano ushoga ni kwa wanaume ni yule anayefanyiwa (*******) na yule anayefanya (basha) siyo shoga. Kumbe wote wawili ni mashoga (homosexuals) kwani wanavutiwa na watu wa jinsia yao whichi is the essence of what homosexuality is. Maana wengine wanapozungumzia mashoga wanawafikiria wale wanaume ambao wanaonekana kama wanawake au wanajirembesha kama wanawake lakini hawawafikirii mabasha. Je, polisi na vyombo vyetu vya sheria vifuatilie vipi hapa?

Ndoa za mashoga
Hata hivyo tatizo kubwa ambalo linagongana na watu wengi na kwa haki kabisa ni suala la ndoa. Kila jamii tangu kale kabisa zimetambua kuwa ndoa ni mahusiano ya mwanamme na mwanamke. Japo katika historia nyingi na jamii za kale kumekuwepo na mashoga lakini hakukuwa na ndoa za mashoga. Wagiriki wa kale walikuwa na haya mambo lakini hawakuwa na ndoa za mashoga. Na kutokana hivyo tangu kuumbwa mwanadamu ndoa imekuwa ni taasisi takatifu ambayo inahusisha wanaume na wanawake.

Ni kutokana na hilo hata Marekani na Uingereza hakuna kitu kama ndoa ya mashoga na hata pale walipojiundia kitu chao cha kiserekikali kuwa ni "ndoa" ukweli ni kuwa taasisi za kidini na jamii kwa ujumla hawakubali kitu hicho. Ndio maana Marekani kwa mfano wamepitisha sheria ya Defence of Marriage Act (DOMA) ya 1996 ambayo ilipitishwa wakati wa Bill Clinton. Sheria hiyo inatambua kuwa ndoa ni muungano kati ya mume na mke. Sasa leo kwanini watu wafikirie kuwa Marekani inaweza kutulazimisha tuvunje mfumo wetu wa maisha kwa sababu ya misaada? Kwanini wao wenyewe wasifute kwanza sheria yao na kutambua Ndoa ya wake wengi kama sisi tunavyofanya?

Tutofautishe "ndoa za mashoga" na 'haki za mashoga'
Mojawapo ya matatizo ambayo Uingereza na Marekani yameleta katika hili la kuhusisha misaada na masuala ya mashoga ni kuchanganya mambo haya mawili. Hakuna kati yao aliyesema wanataka nchi zinazopokea misaada zitambue "ndoa za mashoga" kama wengi walivyotafsiri au kuripotiwa. Hawa walikuwa wanazungumzia "haki za mashoga" kwa maana ya kwamba kuna jamii au nchi ambazo zinatumia muda wao mwingi na raslimali zao kuwanyanyasa na kuwatesa mashoga. Napendekeza kwamba Tanzania siyo nchi mojawapo ya hizo.
Hatuwatesi mashoga
Hatuwafungi
Hatuwakatazi au kuwanyima haki zao ambazo ni haki za kila Mtanzania

Na wakifanya uhalifu wanaadhibiwa kama Mtanzania mwingine. Hakuna upendeleo wa mashoga. Ushoga usiwe kisingizio cha mtu kufanya uhalifu halafu akikamatwa adai kuwa ati kakamatwa kwa vile yeye shoga. Jamii yetu ina sababu ya kulinda watoto na vinana wake katika kuwapa malezi ya kifamilia na huu ni wajibu ambao hatuhitaji Marekani, China, Uingereza au Iran kutuambia. Binafsi napuuzia hoja za Cameron na Obama kwani hazihusu Tanzania labda nchi nyingine na nina uhakika hat aakiulizwa balozi wa Marekani au Uingereza atakiri tu kuwa yote wanayoyazungumzia ni nchi zile ambazo hazina haki za binadamu.

Binafsi ningependa kusikia Uingereza na Marekani wanaunganisha haki za kisiasa (political and civil rights) na misaada. Kwa sababu hapo wataigusa na Tanzania hili la "haki za mashoga" halituhusu. Maana kama kuna haki zinavunjwa sana Tanzania ni hizo.

Ni kweli kaka na pia kama atachaguliwa na wananchi kuwaongoza basi ataapishwa kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania!

 
Na kama mashoga wapo ndani ya jamii zetu mnataka wapelekwe wapi ni vizuri mkajadi uwepo wao ili kuweza kujua nini cha kufanya na si kukurupuka na kuanza kulaumu marekani na uingereza
 
Tanzania ni moja ya Nchi ambyo ni ya aina yake kwa kweli,uwa ikitokea Mtanzania akasema No anamaanisha Yes na akisema Yes anamaanisha No.

Ushoga na Matendo mengineyo ya kishoga ndani ya ardhi ya Watanzania halisia na ndani ya Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni matendo ambayo yamekuwepo toka zama na zama.

Kwa wakazi wa maeneo ya mijini mambo haya ni mambo ambayo yako chini ya neno maalufu kama KAWAIDA,ambyo uendelea mpaka NGAZI YA MAZOEA kisha uitimisha safari yake ndani ukikomo wa neno TABIA.

Hivyo kwa baadhi ya watanzania kukemea kimataifa tabia ambayo ni sehemu yao ya Maisha ni UNAFIKI.wale wote tulionao mitaani mwet u tunawaona na kuwatuhumu mitaani mwetu mbona hatuwakani na kuwaponda kwa hayo.Hakika binafsi uwa sina risasi ya kidole dhidi ya watu wanaoitwa mashoga,kwa kuwa swala laushoga ni la mtu binafsi na hukumu yake anayo Mungi na sio Mimi Mwanadamu.

Hivyo ni lipi lilotusukuma viongozi wengi wa kada zote kupiga kelele kwa mambo ambayo kwa uasilia tunayo na tunaishi nayo kwa amani kwenye mitaa na viunga vyetu vya mijini na majiji yetu.Hivyo ni kweli MM ulichosema Marekani na Uingereza ambao sheria zao dhidi ya aina hii ya tabia kwa raia wake ziko wazi na wana baraka zote mpaka baraka za kuona.

Kwa Watanzania mashoga wana haki sawa na raia wengi,na wengine wanaheshimika kwenye jamii kwa kuwa wamepata kuwa madaraka na wengine wanamadaraka ndani ya jamii yetu ya Watanzania na lakini hatukupata kuwanyoshea risasi kidole kama kipindi hichi cha sasa.

Tanzania tuna utamaduni wetu wa kuishi na wanajamii hawa wenzetu wenye haiba hiyo,lakini kuna vile tunavyoviona hadharani lakini kwa malezi na haiba yetu huwa hatuna tatizo navyo navyo,vitu hivyo ni kama vile mitembeo,mavazi yani muonekano wa uvaaji,sauti n.k.Kwa Mwanajamii yoyote yule shoga, wanajamii wenzie hawana tatizo nae daima vitu vyake hivyo kuvionyesha hadhalani.

Lakini hili la Ndoa Watanzania hawana mazoea na kwa imani ya dini zao jambo hilo ni chukizo kwa Mungu wao, hivyo hilo jambo halina ushabiki chanya [Positive] hivyo jamii daima haina uwezo nalo kwa kuwa NDOA kwa dini na uafrika ni watu wenye jinsia mbili tofauti kuishi pamoja na hatimae kuzaa na kuwa na familia ambayo ndio watoto.Hivyo kwa mantiki hiyo kwa Mashoga walioko Tanzania kupewa haki hizo kisheria kwa sasa sio rahisi na sio leo wala kesho na haitatokea kwa kuwa utamaduni wa kitanzania umewapa fulsa na haki zote za msingi ambazo Mtanzania mwingine yoyote anazo.Na kama ikitokea basi Imani ya Kidini na utamaduni Katika Taifa hili lenye waumini wa dini ya Kikirsto, Uislamu na kijadi utakuwa umepungua nguvu na hivyo kufanya baadhi ya baadhi ya vizazi kuhalalisha kwa kuzingatia hizo husika nyakati.
 
Hawana haki kama heterosexual. Kuna stigma kubwa sana against mashoga, iwe politica au social stigma na wanaochangia wengi ni politica and religious figures, wakijifanya kuongea kwa niaba ya watanzania wote.
They are molested and categorized and segregated jus for who they have sex with, shida ambayo wewe huipati.
Mbaya zaidi wakiamua kwenda kufungua kesi bado watatukanwa tena for daring. Soma hapa:
Homosexuality is not only openly condemned by powerful social actors such as church leaders and politicians but is also illegal.

In his open letter to the Anglican Diocese of Central Tanganyika Mdimi denounced the violent prosecution, hate and ostracism that gay Tanzanian had to face (Mdimi, 2007). Anyamele mentioned in his 2005 report on Sexual minorities (recognized and co-funded by the world bank) that Tanzanian Homosexuals were being segregated professionally and socially and mentioned that ‘adverse comment' were made regularly against homosexuals by senior politicians, including head of state. (Anyamele 2005)

Sexual activities between men are punishable of 14 years in prison (no mention of inter female sex) and celebration of a gay union in a way that approximate marriage is punishable of 7 years in prison (section 154 to 157 of the Tanzanian Penal code).

Yote tisa lakini tukitaka kufuata haki na uchunguzi ktk swala hili la USHOGA halikuanza kwa mapenzi ya wahusika. Historia ya ushoga inaanza na watoto waliokuwa abused na ndugu, jamaa na watu waliokuwa wakiwaamini wakawaingilia kimapenzi. Kwa hiyo mwanzo wa kupiga marufuku Ushoga ulitokana na sio tu mila na desturi bali kuwalinda watoto wetu ktk vitendo hivyo kama tunavyowalinda watoto ktk maswal ya mapenzi ya kawaida. Ushoiga haukuanza kwa mapenzi ya wahusika bali kuingiliwa kwa nguvu na ushawishi wa matamanio ya baadhi ya watu wazima.

Sasa maadam siku hizi Ushoga umekuwa baina ya watu wazima waliopendana, hii haikatazwi isipokuwa jambo moja tu linalonichanganya. - SHOGA hawezi kuwa shoga bila kufanya kitendo cha kuingiliana kimwili na mtu wa jinsia moja.. Yaani kitendo ndicho tu kinampa identity mtu, kiasi kwamba mtu yeyote hawezi kudai yeye shoga ikiwa hajawahi kuingiliwa ama kuingilia mtu wa jinsia yake!...mmmmhnnn!. Hapa ndipo Utata unapokuja na hakika kinacholaani wa ni kitendo lakini sio WATU..

Kwa nchi zetu ushoga haupokelewi vizuri lakini kama alivyosema Mwanakijiji, huwezi kudai haki za Mashoga wakati mashoga wanazo haki zote kutokana na kwamba sisi hatulaani WATU bali tunalaani kitendo na ndio mila na desturi zetu. Hivyo haki zinazodaiwa haziwezi kuwa applied kwetu kwa sababu mashoga ni watu baina yetu wanaopendwa kama watu wengineo isipokuwa inapofikia swala la kuhalalisha ndoa zao hapo tena huchukiwa hata wahusika wenyewe maana tunahalalisha KITENDO..

Na nchi kaa Uingereza, Marekani na Canada hjawawezi kutulazimisha tukubali ndoa za mashoga kama haki ya mashoga wakati wao wenyewe sehemu kubwa ya Utawala wao hawana sheria inayoruhusu ndoa za mashoga. Ndoa za mashoga ni swala la kijamii na litapewa uzito kulingana na wahusika ktk mazingira yao wenyewe lakini haliwezi kuwa swala la kimataifa..
 
Tatizo ni tabia ya mashoga kutaka kujionyesha "displaying behaviour". Pia kufanya movement ya kuwahamasisha watoto kuwa ni haki ya msingi ya binadamu.

Wazungu wana mambo yao wanaona ni haki zao za msingi na hatuwaingilii. Wao wanaona kuwa homosexualism ni haki yao. Sisi tuna haki zetu tunazoziona kuwa ni za msingi. Wasituingilie. Sisi tunaona ndoa za wake wengi na jambo la sifa na la msingi. Sisi bado tunanguvu kubwa za kiume na twaweza kuwaridhisha wake zetu hata wakiwa wanne. Wao hata mmoja ni issue ndo maana wanataka kungilia haki za wanawake!!!!! Wao wamefanya kosa la jinai kuoa mke zaidi ya mmoja wakahalalisha ndoa za jinsia moja nasi tumehalalisha wake wengi tuzuie ushoga. Tusiwanyime kina mama haki yao ya ku.....
 
Ukiona watu wazima wanaanza kuongelewa vitu vya kipuuzi ujui ni watu wa ovyooo!

ni uppuzi kuongelea, kuandika, upuuzi huu..

kinachotakiwa ni kupuuzwa tena kudharauliwa na kutengwa..oops
 
Mashoga hawana haki Tanzania! Uingereza saizi serikali inakubali ndoa za mashoga na inatoa hati za ndoa za mashoga na wanatambulika kisheria..

Tanzania bado haki hiyo muhimu kwa mashoga hakuna..

Kwa hiyo Tanzania Mashoga hawana haki.
 
Mashoga hawana haki Tanzania! Uingereza saizi serikali inakubali ndoa za mashoga na inatoa hati za ndoa za mashoga na wanatambulika kisheria..

Tanzania bado haki hiyo muhimu kwa mashoga hakuna..

Kwa hiyo Tanzania Mashoga hawana haki.
Kwa leo nakuunga mkono Ritz. Nashangaa sana watu kusema kua mashoga wana haki kama watanzania heterosexuals.
Hivi ni nani kati yetu anapewa identity kufatana na jinsia ya sexual partner wake? Maana this is true kwa mashoga na mabasha.
Ikiwa you have sex with people of your gender in Tanzania hiyo inakua sababu ya watu kukuangalia tofauti, kuwaambia watoto wao wakuogope, kujadili mambo yako publicly, kupigwa ,kuwa segregated kikazi etc.
Huwezi ku-adopt, huwezi kuoa wala kuolewa, huwezi kuvaa nguo unazo taka na kujitetea haki yako.
Hata nchi za njie zinashindwa kuingia in touch na gay lesbian and transexual community sababu they are ILLEGAL! huwezi kuanzisha kikundi cha wanachama GLT sababu vyama kama hivyo havisajiliwi!
Nashangaa Mkadara ananambia kua 'culture yetu' haijawa tayari kupokea ndoa ya watu wenye jinsia moja. Yetu sisi kina nani? nani anasema kwa jina la watanzania wote? mbona hao gays lesbians and transexual tunao waongelea ni tanzanian pia? Hivi tukisema kila mtanzania anahaki ya kuoa/kuolewa kwa nini tunataka ku-restrict anaoa/anaolewa na nani?
Anaendelea kwa kusema mashoga walianza kwa kuwaingilia watoto wetu alafu maswala ya mapenzi yakaja baadae. Huvi unajua watoto wengi hulaitiwa na ndugu zao (kaka, mjomba, baba mdogo au baba, and sometimes mama, dada etc)? na hao watu wanafanya hivo bila kua shoga au basha, ni tabia zao mbaya tu. Na mapenzi kati ya jinsia moja yalikua tu, ni vigumu kusema yalianza lini.
Tuwe wazi, haki hizi hazipo na "culture" is only a pretext we use, a cover.
 
Usitukane viongozi wa dini kwa mambo yako ya kisiasa, kwa sababu hawajapinga posho kuongezwa bungeni basi waukubali ushoga?

Mimi ni mkristo..upumbavu sio tusi,ila ni tabia ya binadamu kutokubaliana kuwa hajui,na kwa hiyo hafundishiki....ni pumbavu!!
 
Back
Top Bottom