Mashoga wa Tanzania wana Haki zote kama Watanzania wengine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga wa Tanzania wana Haki zote kama Watanzania wengine?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 7, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijui ni kwanini watu wanashindwa kutoa jibu jepesi kabisa kwa Uingereza na Marekani kuwa katika Tanzania mashoga wanazo haki zote ambazo Watanzania wengine wanazo. Tena hakuna nchi ambayo ina uvumilivu sana wa mashoga katika Afrika kama Tanzania kwa sababu tayari katiba yetu imewawekea ulinzi kama ulivyo kwa Watanzania wengine. Kwamba 'kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Na hii "kila mtu" inajumlisha watu wa dini tofauti, makabila tofauti, rangi tofauti naam hata mwelekeo wa jinsia tofauti.

  Shoga wa Tanzania anazo haki zile zile ambazo anazo mtu mwingine:

  a. Ana haki ya kupiga kura
  b. Ana haki ya kuishi
  c. Ana haki ya kufanya kazi (wengine wameshika hata nafasi za juu tu nchini)
  d. Ana haki ya kuishi popote (shoga halazimishwi na jamii kuishi mahali asipotaka yeye)
  e. Ana haki ya kupata elimu (wapo wanasoma na wamesoma kwenye shule na vyuo vyetu)
  f. Ana haki ya kusafiri ndani na nje ya nchi
  f. Ana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yake (na wametoa hata kama yanawaudhi wengine - hatujaenda kuwafunga watu kwa kutoa maoni ya kutetea ushoga)
  n.k

  Kwa hiyo - maelezo ya Cameron na Obama hayahusu Tanzania na sioni sababu kwanini Watanzania wanashtuka sana au kukereka. Jibu letu ni jepesi - mashoga wanazo haki zile zile za binadamu ambazo wananchi wengine wanazo na hakuna sababu ya kutengeneza kundi jingine la haki nje ya zile ambazo kila Mtanzania anazo.

  Kuondoa ushoga kama kosa la kihalifu (decriminalization of homosexuality)
  Sasa wanapozungumzia "haki za mashoga" wakati mwingine wanaaminisha kuwa tuondoe kwenye sheria zetu ushoga kama kosa (a criminal offense). Sasa hili siyo jambo la Marekani au UK kwani masuala ya makosa yanaamuliwa na jamii husika na kwa hoja walizonazo. Japo sheria ipo Tanzania haitekelezi sheria hiyo na kuanza kwenda kila nyumba na chumba na kuwafunga watu ati kwa vile wameonekana wameshikana mikono au wameingia chumba kimoja. Hivi kweli kuna mtu anafikiria tunaweza kuzitekeleza hizo sheria kwa kila mji, mkoa, nyumba na mitaa? Huo uwezo uko wapi? Halafu kati ya matatizo yetu yote ambayo tunayo leo kama taifa hili la kukamata mashoga mbona halipo? Hatujasikia watu wanaenda na viboko au kuwacharaza watu kwa vile ni mashoga. Watanzania wamekuwa wavumilivu mno na wengi wamekubali kuwa hilo ni suala la mtu binafsi tena mtu mzima na Katiba inawalinda watu hao pale inaposema kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa faradha yake.

  Vinginevyo, itabidi tuunde kikosi maalumu cha Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa au hata Magereza ili kufuatilia vitendo vya ushoga (Anti-Homosexuality Police Squad). Sasa kama suala ni kuifuta sheria kwa vile haitekelezeki au kuibadilisha ili ishughulikia makosa ya sodomy, molestation n.k (ambayo tayari yako chini ya SOSPA 1998 as ammended) basi ifanyike hivyo.

  Ukweli ulio wazi ni kuwa anti-homosexuality laws are outdated and unforceable. Zipo sheria lakini hatuwezi kuzitekeleza au kuzisimamia na labda sisi wenyewe wananchi kama kweli tunakereka sana na ushoga kuliko mambo mengine tuwasisitize polisi wakusanye kodi zaidi ili waanze kuwa na vikosi vya kuangalia vitendo vya ushoga kwenye mahoteli.

  Vitendo vya ushoga ni zaidi ya vile vya watu wa jinsia moja
  Wengi ambao wanakereka na vitendo vya ushoga na kuona ni vya kuchukuliwa hatua hawajui kuwa sheria hiyo hiyo inakataza vitendo vya mwanamme kumuingilia mwanamke kinyume na maumbile (a.k.a tigo). Je, tuko tayari kuona na wanaume na wanawake wanaufanyiana hivyo -hata kwenye ndoa- wanafikishwa mahakamani kwa kuvunja sheria. Tutawatambuaje na kuwafuatilia vipi?

  Wengine wanafikiria kwa mfano ushoga ni kwa wanaume ni yule anayefanyiwa (*******) na yule anayefanya (basha) siyo shoga. Kumbe wote wawili ni mashoga (homosexuals) kwani wanavutiwa na watu wa jinsia yao whichi is the essence of what homosexuality is. Maana wengine wanapozungumzia mashoga wanawafikiria wale wanaume ambao wanaonekana kama wanawake au wanajirembesha kama wanawake lakini hawawafikirii mabasha. Je, polisi na vyombo vyetu vya sheria vifuatilie vipi hapa?

  Ndoa za mashoga
  Hata hivyo tatizo kubwa ambalo linagongana na watu wengi na kwa haki kabisa ni suala la ndoa. Kila jamii tangu kale kabisa zimetambua kuwa ndoa ni mahusiano ya mwanamme na mwanamke. Japo katika historia nyingi na jamii za kale kumekuwepo na mashoga lakini hakukuwa na ndoa za mashoga. Wagiriki wa kale walikuwa na haya mambo lakini hawakuwa na ndoa za mashoga. Na kutokana hivyo tangu kuumbwa mwanadamu ndoa imekuwa ni taasisi takatifu ambayo inahusisha wanaume na wanawake.

  Ni kutokana na hilo hata Marekani na Uingereza hakuna kitu kama ndoa ya mashoga na hata pale walipojiundia kitu chao cha kiserekikali kuwa ni "ndoa" ukweli ni kuwa taasisi za kidini na jamii kwa ujumla hawakubali kitu hicho. Ndio maana Marekani kwa mfano wamepitisha sheria ya Defence of Marriage Act (DOMA) ya 1996 ambayo ilipitishwa wakati wa Bill Clinton. Sheria hiyo inatambua kuwa ndoa ni muungano kati ya mume na mke. Sasa leo kwanini watu wafikirie kuwa Marekani inaweza kutulazimisha tuvunje mfumo wetu wa maisha kwa sababu ya misaada? Kwanini wao wenyewe wasifute kwanza sheria yao na kutambua Ndoa ya wake wengi kama sisi tunavyofanya?

  Tutofautishe "ndoa za mashoga" na 'haki za mashoga'
  Mojawapo ya matatizo ambayo Uingereza na Marekani yameleta katika hili la kuhusisha misaada na masuala ya mashoga ni kuchanganya mambo haya mawili. Hakuna kati yao aliyesema wanataka nchi zinazopokea misaada zitambue "ndoa za mashoga" kama wengi walivyotafsiri au kuripotiwa. Hawa walikuwa wanazungumzia "haki za mashoga" kwa maana ya kwamba kuna jamii au nchi ambazo zinatumia muda wao mwingi na raslimali zao kuwanyanyasa na kuwatesa mashoga. Napendekeza kwamba Tanzania siyo nchi mojawapo ya hizo.
  Hatuwatesi mashoga
  Hatuwafungi
  Hatuwakatazi au kuwanyima haki zao ambazo ni haki za kila Mtanzania

  Na wakifanya uhalifu wanaadhibiwa kama Mtanzania mwingine. Hakuna upendeleo wa mashoga. Ushoga usiwe kisingizio cha mtu kufanya uhalifu halafu akikamatwa adai kuwa ati kakamatwa kwa vile yeye shoga. Jamii yetu ina sababu ya kulinda watoto na vinana wake katika kuwapa malezi ya kifamilia na huu ni wajibu ambao hatuhitaji Marekani, China, Uingereza au Iran kutuambia. Binafsi napuuzia hoja za Cameron na Obama kwani hazihusu Tanzania labda nchi nyingine na nina uhakika hat aakiulizwa balozi wa Marekani au Uingereza atakiri tu kuwa yote wanayoyazungumzia ni nchi zile ambazo hazina haki za binadamu.

  Binafsi ningependa kusikia Uingereza na Marekani wanaunganisha haki za kisiasa (political and civil rights) na misaada. Kwa sababu hapo wataigusa na Tanzania hili la "haki za mashoga" halituhusu. Maana kama kuna haki zinavunjwa sana Tanzania ni hizo.
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  kwanini tusijiulize hayo maswali kwa wahalifu wengine kama wezi,Malaya n.k? Tufikirie namna ya kuongeza sheria za kuwabana mashoga,wezi n.k hiki si kikundi cha walemavu wanaohitaji msaada wa jamii kutambulika nafikiri tunawajadili mashoga kama tunavyowajadili walemavu which is big mistake
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ni kwamba Watanzania ni kama tumekuwa too much obsessed na hiki kitu kiasi kwamba vitu vyenyewe vya msingi hatuwi wakali hivyo. Tunaonesha unity kwenye vitu ambavyo kwa kweli kabisa havistahili muda wote lakini vile vya msingi ndio hatutaki unity. It puzzles me.
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  msije na sababu za kisayansi kudhibitisha aina hii ya ulemavu! Hata Yesu kwasisi wakristo aliwaweka mashoga kundi moja na wahalifu(wezi,wazinzi,wafir*ji n.k),mjadala uwe na msingi huo na tusijadili haya kwa mtazamo wa wazungu!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wazungu ni akina nani?
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  MKJJ,

  Ni kweli kuwa katiba yetu inawapa uhuru sawa raia wake wote pamoja na mashoga kama akina auntie Moody. Je ni kweli kuwa katiba yetu inatambua uwepo wao?? Ninavyofahamu TZ hatujawahi kusema popote kama tunatambua uwepo wa jinsia hiyo ya mashoga. Hii ya kusema kuwa rais wote wanahaki sawa haina maana kama katiba haitambui uwepo wao. Katiba nafikiri inatamka kuhusu uwepo wanaume, wanawake, watoto, vijana, wazee, vilema (may be mashoga wako huko) na posssibly albinos. Je una maana mashoga wakijamiiana ni sawa kwa sheria zetu?? Nakumbuka miaka michache iliyopita nilisikia kama kuna sheria imepitishwa ZNZ ambayo haiwatambui mashoga na wakikutwa ni lupango miaka 25.
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  Waasisi wa haki za binadamu zinazopitiliza hadi kuvunja utu!!
   
 8. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio haki za Washoga Tanzania, tatizo jamii yetu inakubali mashoga?

  Samahani lakini kwa swali langu ni mfano tu kwa Mzee Mwanakijiji na Gaijin..

  Vipi kama watoto wenu wa kiume wakiwa mashoga wakawaletea wenza wao nyumbani muwatambue kama wakwe zenu mtakuwa tayari kuwapokea?
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tena mpaka watu walikuwa wanatoka mapovu mdomoni kwa kupinga hili,viongozi wa dini waliandaa hotuba siku za Ijumaa(waislamu),Jumamosi(wasabato) na Jumapili(wakatoliki na waprotestanti) kwenye ibada zao kupinga ushoga..Linapokuja suala la POSHO ZA WABUNGE yamekaa yanauza sura.........Pumbavu!!!
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Nchi ya tanzania ishatoa msimamo dhidi ya hawa wahalifu wa kimaumbile. Kama mashoga hawakuridhika na tamko la Serikali kuwahusu, basi wakate rufaa kwa Cameroun.
  Kwa upande wa dini mashoga hawana jina linalowagaa ila mapepo machafu ambapo hayajadiliwi ila kukemewa kwa mamlaka ya jina la Yesu, na kuyafungia katika hilo shimo la giza wanakotaka kutoroka kuja kuzurura huku nuruni.
  .
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana nawe Mwanakijiji. Hatuwezi kuwa watu wa ajabu kwa kukataa au kutoshabikia mapendekezo ya kila mtu kwa vile hata vitendo vya kawaida tu basi vina mipaka yake katika uhusiano katika jamii sikwambii kitendo cha ushoga. Hata shughuli za kawaida za kibinaadamu basi zina mipaka yake inayozuia mwengine asikirihishwe nayo.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuwawekea haki katika katiba kwa kuwa leo aweza kuwa shoga kesho akaacha.......sawa na mlevi
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Usitukane viongozi wa dini kwa mambo yako ya kisiasa, kwa sababu hawajapinga posho kuongezwa bungeni basi waukubali ushoga?
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kikomo cha haki za binaadamu ni nini?
   
 15. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red; si vibaya kujifunza kwa wengine walioweza ku-enforce sheria za aina hiyo. Mfano mzuri ni taifa la Kiislamu la Saudi Arabia ambao wana hadi wizara inayoshughulika na masuala ya dhambi. Soma hapa: Committee for the Promotion of Virtue and the Prevention of Vice (Saudi Arabia) - Wikipedia, the free encyclopedia

  Hapo kwenye
  green; huu ni mchezo wa kawaida huko uswahilini. Nina uhakika wengi hawajui hili ila likijulikana litakumbana na upinzani kwani hata vitabu vya dini vinaruhusu.
   
 16. A

  Ame JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280  Hili ambalo nila msingi hawaliongelei; wao wako kuongelea tu mambo ambayo hayana msingi na kwenye needs ranking pengine siyo basic need kwa kuangalia uhalisia ya maisha ya mtanzania.

  Huo msaada mbona hawatuambii ni kiasi gani in proportion kina rudi kwetu sisi as compared to contribution ya taxes ama National Gross income ya nchi zao zinazotokana na marginal profit ya mashirika yao ya kibepari yanayo chumia nchini kwetu?

  Kiasi gani wanakitoa kwa viongozi kama bakshishi ili watoe biased deals kwa makampuni yao makubwa kupewa tenda kubwa kubwa za miradi ya maendeleo?

  Hizo haki ambazo zina kwamisha taifa kuwapa watu wake haki za msingi hawazi ongelei wako bussy kama tulivyo sisi kuongelea vitu ambavyo kwetu ni luxury kutokana na level ya development tulipo as compared to wao ambao hizo basic needs zote za mlazi/makazi; chakula na matibabu wanazo pamoja na ziada kama sheria za kulinda mashoga ambazo pengine kwenye preference zetu zinaweza kuwa tertiary na hata si secondary japo kwao kwakua na insertiable wants za human behaviour za weza kuwa primary kutokana na level ya development na civilization waliofikia.
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Natamani kujua ni vitabu vya dini gani vinaruhusu tigo kwa mke!??? Duuh kuwa uone mwanawane wengine.

  Maisha ya ukristo ambayo si dini maana hakuna dini inaitwa ukristo kuna dini zinazoitwa ukatoliki, u-protestant; Uanglikani, upentekoste, usababto, ujehova etc ambayo mimi naona kama makampuni tu ya kiroho ambayo mwanadamu kwa ubinafsi wake kajiundia; yananitaka kuiheshimu ndoa na malazi yawe safi kuanzia rohoni mpaka mwilini. Kwa maana ya kuwa umpende mke wa ujana wako na pia usikichafue kitanda chako cha ndoa kwakubeba mawazo ya machanguduo na ma sugar mami akilini mwako bali umwaze mkeo 24/7. Umpende mke wako na usimtendee vibaya kwatumia vizuri maungo yake asivyopenda ama isivyo stahili; hii pamoja na oral sex kama haipendi basi ni dhambi maana inabidi mkubaliane (hiari na uhuru wa mwenzako japo mwongozo wetu haukatazi hilo iwapo wawili wanaona si tabu kwao). hiyo tigo ni abomination kwa Mungu na kwakufanya hivyo una defile ur marital bed na unaingiza laana kwenye familia yako ikiwa ni pamoja na watoto wako.

  Kwakua mm ni preacher acha niwaambie wakristo ndoa haifundishwi na internet materials inafundishwa na Bible under hollyghost reveletion ambaye si authour of confusion and mwenye exact knowldge about every thing in this space. He is the way, the truth and life. Kunaweza kuwepo facts zinazotegemea akili ya mwanadamu katika researches zake lakini zote ziko bound to change over a space of time mwingine anapokuja na ugunduzi mwingine kwani a fact is not truth. Mfano its a fact that HIV has no cure but this is not truth that it will remain uncured for the millions of years to come.
   
 18. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  MM. Umenishangaza sana kwenye suala hili la shinikizo la haki za mashoga toka Uk. na USA. Kama nimekuelewa vizuri, unasema tusistuke na pia hakuna haja ya kukereka kwa sababu shinikizo hilo halituhusu kwa kuwa sheria zetu haziwabagui mashoga. Loooh! MM. Ukumbuke kuwa siku zote, kuna kanuni isemayo, 'mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake'. Vivyo hivyo kwa mtunga sheria, 'hujipendelea'. Sitarajii kukuta serikali yoyote kupitia baraza lake la kutunga sheria au bunge, ikitunga sheria ya kujikandamiza yenyewe. Nikirudi kwenye shinikizo la ushoga ni lazima tushtuke na tukereke. Sababu hasa ni jambo lililo kinyume na maumbile ya Mwanadam. Sheria zetu zipo wazi, ukipatikana na ushahidi kuwa umemuingilia mwanamme/mke kinyume ya maumbile, adhabu yake miaka 30 jela. Kutokuwa na uwezo wa kufatitilia sheria sio kigezo cha kuwa 'ruksa' kuvunja sheria kwa kuwa hatuna uwezo wa kuilinda sheria ifanye kazi. Hao wanaotushinikiza wananatujua pengine kuliko tunavyojijua! Pia wanajua wanachokitaka kwetu ni kipi. Wanataka uhalali wa kisheria. Pasiwe tena na tuhuma au pingamizi katika ndoa. Unaowa/unaolewa kisheria huku tukijua wazi mapema, kweupee, mbele ya halaiki na wageni waalikwa kuwa wanandoa hawa watakwenda kufanya mambo kinyume na maumbile. Jamani tuwe waangalifu na makini, hasa tunapoingia mikataba ya kisheria na hawa watu. Tusije kosea kama kwenye mikataba ya madini/umeme nk.
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  Umeeleweka nadhani wanaosema membe ni kichwa at least angeongea robi ya haya, lakini alionge pumba tupu.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Kwa watanzania nafikiri ni kama a "natural dont ask don't tell"

  Ama na wewe unazungumizia haki gani? Kwasababu hizo ulizoziorodhesha hapo juu hazina shida kabisa, mashoga wako wachache, na hawajawahi kubaguliwa kwenye nyanja hizo, at least not to my attention...

  Labda kama wanataka kuwa encourage mashoga wajitokeze kwa wingi, jambo ambalo kutokana na jamii yetu na cultures zetu, sidhani kama wale wa "down low" watajitokeza...

  Za kutokuzodolewa? AKA anti bullying?

  Hilo sidhani kama ni tatizo, na pia Taifa letu halina mashoga wengi kiasi kwamba kuwe na movement za mshoga.

  Ama kuna ushahidi kuwa wanabaguliwa?

  Hizi sheria za mashoga labda ni kwasababu naamini hawa watu wanajiandaa kurudi Afrika.

  Sidhani kama tuna tatizo la "Haki za mashoga"
   
Loading...