Mashirika na Taasisi za Umma zinazostahili kufutwa na zile zinazostahili kuunganishwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,362
145,411
Wakati serikali ikiendelea na zoezi la kuunganisha na kufuta baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma, nashauri tutoe maoni na mapendekezo juu ya mashirika na taasisi zinazostahiili kuunganishwa pamoja na zile zinazostahili kufutwa.

Nia na madumuni ni kuishauri serikali ili isije kufanya makosa (kama hawatafuata ushauri wa wadau) na pia tuwe na haki ya kuja kuwakosoa huko mbeleni iwapo watafanya makosa katika huu mchakato.

Pia, wenye utaalamu/ufahamu, watupe faida na hasara za jumla za zoezi hili zima pamoja na hasara na faida za kuunganisha na hata kufuta kabisa baadhi ya taasisi na mashirika.

Karibuni.
 
Mimi naanza na TARURA na TANROADS.

Binafsi sioni umuhimu wala ulazima wa kuwa na hizi taasisi mbili zaidi ya kuongeza idadi ya mashangingi ya kuhudumia wakurugenzi na vigogo wengine wa hizi taasisi mbili zinazofanya kazi ya aina moja(ujeni wa barabara) na gharama nyinginezo za kuhudumia hizi taasisi.
 
Wakati serikali ikiendelea na zoezi la kuunganisha na kufuta baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma, nashauri tutoe maoni na mapendekezo juu ya mashirika na taasisi zinazostahiili kuunganishwa pamoja na zile zinazostahili kufutwa.

Nia na madumuni ni kuishauri serikali ili isije kufanya makosa(kama hawatafuata ushauri wa wadau) na pia tuwe na haki ya kuja kuwakosoa huko mbeleni iwapo watafanya makosa katika huu mchakato.

Pia, wenye utaalamu/ufahamu, watupe faida na hasara za jumla za zoezi hili zima pamoja na hasara na faida za kuunganisha na hata kufuta kabisa baadhi ya taasisi na mashirika.

Karibuni.
Tungeanzia hapa DC & DED, tuwe na DED Tu Kwa wilayani
 
Back
Top Bottom