Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Naibu Waziri Nishati, Judith Salvio Kapinga ametembelea vituo vya Kuzalisha Umeme, Ubungo 1 na Ubungo 2 ili kuona hali ya uzalishaji wa umeme katika vituo hivi kwa maelekezo ya Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.
Naibu Waziri anazungumza
Kwenye Kituo cha Ubungo 2, mashine zipo tatu na kila moja inaweza kuzalisha Megawati 43, kati ya hizo moja haifanyi kazi na ipo kwenye matengenezo.
Kituo cha Ubungo 1 kuna mashine 12, zinazofanya kazi ni 6 ambazi kila mashine inazalisha Megawats 42 hadi 43, nyingine zipo kwenye matengenezo, hivyo nimewalekeza TANESCO kuhakikisha wanakuwa na mpango wa marekebisho ya muda mfupi, wa kati na mrefu.
Matengenezo ya muda mfupi yafanyike kwa wakati ili huduma ya umeme iweze kupatikana kwa wakati, hivyohivyo kwa mipango ya marekebisho ya muda wa kati na mrefu.
Kitendo cha kuwa na mashine moja nje ya huduma ni kupoteza umeme mwingi.
Leo pia kwa bahati mbaya Kituo cha Ubungo 1 kimezimika umeme kuanzia usiku hadi muda huu (mchana wa Septemba 29, 2023), mitambo sita ambayo inatakiwa kuzalisha umeme nayo haizalishi.
Wataalam wapo ‘site’ wanahakikisha umeme unarejea, nimewaambia TANESCO kuwa ndani ya saa mbili kituo kiwe kimerejea kufanya kazi na ikishindikana watafute mbadala ya kuhakikisha ndani ya saa sita zijazo uzalishaji wa umeme uwe umerejea kama kawaida ili upatikanaji umeme uimarike.