Dkt. Biteko: TANESCO hamtalala usingizi hadi wananchi wapate Umeme

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufikiri kila itakayoweza kutatua tatizo la upungufu wa Umeme Nchini na kama wasipofanya hivyo atahakikisha hawalali usingizi

Pia, Dkt. Biteko amekiri kuwa TANESCO inakabiliwa na matatizo ambayo yako nje ya uwezo wao lakini anashangazwa na kitendo cha kukuta Mashine ya kuzalisha Umeme katika Kituo cha Gesi Asilia ikwia imeharibika kwa miaka miwili huku chanzo cha Umeme kwasasa kikiwa ni 65%

Ameongeza kuwa TANESCO imejilimbikizia Mamlaka yote kutoka Mikoani na hakuna wanachokifanya huku akitoa onyo kwa kitengo cha Manunuzi cha Shirika hilo kuwa kijitafakari kabla hajaenda kukitembelea
 
kwani serikali isiruhusu makampuni mapya yazalishe umeme?

Wanang'ang'ana wao tu. tuleteeni wawekezaji tujue moja.
 
Kila siku wanakuja na visingizio vipya kuhusu kukosekana umeme hapa nchini. Mwanzo walisema ni upungufu wa maji, mvua zinanyesha kola kona ya nchi wamebadili gia wanasema mashine mbovu.

Huu uhuni utaisha lini watu tunakaa kwenye giza bila sababu za msingi?
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufikiri kila itakayoweza kutatua tatizo la upungufu wa Umeme Nchini na kama wasipofanya hivyo atahakikisha hawalali usingizi

Pia, Dkt. Biteko amekiri kuwa TANESCO inakabiliwa na matatizo ambayo yako nje ya uwezo wao lakini anashangazwa na kitendo cha kukuta Mashine ya kuzalisha Umeme katika Kituo cha Gesi Asilia ikwia imeharibika kwa miaka miwili huku chanzo cha Umeme kwasasa kikiwa ni 65%

Ameongeza kuwa TANESCO imejilimbikizia Mamlaka yote kutoka Mikoani na hakuna wanachokifanya huku akitoa onyo kwa kitengo cha Manunuzi cha Shirika hilo kuwa kijitafakari kabla hajaenda kukitembelea
Porojo tu johnthebaptist
 
Back
Top Bottom