Naibu Waziri Kapinga - Mtwara na Lindi Wapate Umeme wa Kutosha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

NAIBU WAZIRI KAPINGA - MTWARA & LINDI WAPATE UMEME WA KUTOSHA

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amelihimiza Shirika la Umeme Tanzania - (TANESCO) kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha Mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wa kutosha.

Kapinga ameyasema hayo leo September 14,2023 wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia cha Mtwara ambacho kina mitambo 13 yenye uwezo wa kuzalisha umeme MW 30.4 lakini kwa sasa kinazalisha MW 19 kutokana na mitambo mitatu kuwa katika matengenezo na kinahudumia Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Naibu Waziri ametembelea kituo hicho ili kuangalia halisi hali ya mitambo na uzalishaji wa umeme kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa Wananchi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Amemuelekeza Meneja wa Kituo hicho kuhakikisha wanafanya jitihada za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo ili kukidhi hamu ya Wakazi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi ya kupatiwa umeme wa kutosha akisema jukumu walilonalo ni kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika.
 

Attachments

  • F6ABjQBXEAEvGvY.jpg
    F6ABjQBXEAEvGvY.jpg
    69.8 KB · Views: 1
  • F6ABmDjWkAAQZOI.jpg
    F6ABmDjWkAAQZOI.jpg
    73.1 KB · Views: 1
  • F6ABmDjWkAAQZOI.jpg
    F6ABmDjWkAAQZOI.jpg
    73.1 KB · Views: 2
  • F6ABnZvXEAAuwxr.jpg
    F6ABnZvXEAAuwxr.jpg
    73.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom