Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Biteko Awasha Umeme

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
MHE. DKT. BITEKO AWASHA UMEME KIJIJI CHA NTANGA NA KASHARAZI - NGARA

✔️ AENDELEA NA MCHAKAMCHAKA WA KUWASHA UMEME VIJIJINI​

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameendelea na ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imejumuisha kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Biharamulo, na leo amewasha umeme katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na wanachi katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi, amesema kuwa, Wilaya ya Ngara ina vijiji 75 ambapo mpaka sasa vijiji 43 tayari vina umeme na kwa vijiji ambavyo bado havina umeme, amewaagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa, vijiji hivyo vinapelekewa umeme na baadaye kuanza mpango wa kupeleka umeme kwenye vitongoji.

"Wilaya ya Ngara ina vijiji 75 ; vijiji 43 tayari tumeshapeleka umeme , bado vijiji 32 havina umeme, Mhe. Rais ametoa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya kuwaletea umeme watu wa Kagera mkiwemo watu wa Ngara ". Dkt. Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini mkoani Kagera ikiwemo wilaya ya Ngara hivyo amewaahidi wananchi kuwa umeme utafika kwenye maeneo yote.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wakandarasi wa umeme kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele cha matumizi ya vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi ikiwemo nguzo, mita na transfoma.

“Nchi hii tulihamasisha ujenzi wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya umeme, lakini muda mwingi utaona tunajishughulisha na kununua vifaa nje ya nchi, tunatumia Dola nyingi kuagiza vifaa vya umeme wakati tuna viwanda vipo ndani, natamani mjengee uwezo viwanda vyetu vya ndani ili viweze kuzalisha zaidi na hivyo tukuze uchumi wa watu wetu.”amesema Dkt. Biteko

Amesema kuwa, viwanda hivyo vimejengwa ili viweze kusambaza vifaa kwa TANESCO, REA na wakandarasi wa umeme hivyo si sahihi kwa vifaa hivyo kuagizwa kutoka nje ya nchi.

Akiwa katika Kijiji cha Kasharazi, Dkt. Biteko ametoa kompyuta 10 kwa shule ya sekondari Rusumo B ambayo imeunganishwa na umeme ili kuanzisha darasa la kompyuta katika shule hiyo ambapo pia amewaasa wanafunzi hao kuwa kuwa na nidhamu na juhudi katika masomo.
 
Attachments

  • F7NHPErWgAAxRpF.jpg
    F7NHPErWgAAxRpF.jpg
    71.5 KB · Views: 2
  • F7NHnN-XAAAuPDn.jpg
    F7NHnN-XAAAuPDn.jpg
    58.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-30 at 11.18.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-30 at 11.18.14.jpeg
    44.2 KB · Views: 2
  • F7NIZYSXgAASed_.jpg
    F7NIZYSXgAASed_.jpg
    48.8 KB · Views: 1
  • F7NHygwXEAA6nAh.jpg
    F7NHygwXEAA6nAh.jpg
    82.2 KB · Views: 2
MHE. DKT. BITEKO AWASHA UMEME KIJIJI CHA NTANGA NA KASHARAZI - NGARA

AENDELEA NA MCHAKAMCHAKA WA KUWASHA UMEME VIJIJINI​

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameendelea na ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imejumuisha kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Biharamulo, na leo amewasha umeme katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na wanachi katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi, amesema kuwa, Wilaya ya Ngara ina vijiji 75 ambapo mpaka sasa vijiji 43 tayari vina umeme na kwa vijiji ambavyo bado havina umeme, amewaagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa, vijiji hivyo vinapelekewa umeme na baadaye kuanza mpango wa kupeleka umeme kwenye vitongoji.

"Wilaya ya Ngara ina vijiji 75 ; vijiji 43 tayari tumeshapeleka umeme , bado vijiji 32 havina umeme, Mhe. Rais ametoa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya kuwaletea umeme watu wa Kagera mkiwemo watu wa Ngara ". Dkt. Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini mkoani Kagera ikiwemo wilaya ya Ngara hivyo amewaahidi wananchi kuwa umeme utafika kwenye maeneo yote.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wakandarasi wa umeme kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele cha matumizi ya vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi ikiwemo nguzo, mita na transfoma.

“Nchi hii tulihamasisha ujenzi wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya umeme, lakini muda mwingi utaona tunajishughulisha na kununua vifaa nje ya nchi, tunatumia Dola nyingi kuagiza vifaa vya umeme wakati tuna viwanda vipo ndani, natamani mjengee uwezo viwanda vyetu vya ndani ili viweze kuzalisha zaidi na hivyo tukuze uchumi wa watu wetu.”amesema Dkt. Biteko

Amesema kuwa, viwanda hivyo vimejengwa ili viweze kusambaza vifaa kwa TANESCO, REA na wakandarasi wa umeme hivyo si sahihi kwa vifaa hivyo kuagizwa kutoka nje ya nchi.

Akiwa katika Kijiji cha Kasharazi, Dkt. Biteko ametoa kompyuta 10 kwa shule ya sekondari Rusumo B ambayo imeunganishwa na umeme ili kuanzisha darasa la kompyuta katika shule hiyo ambapo pia amewaasa wanafunzi hao kuwa kuwa na nidhamu na juhudi katika masomo.
Ujinga tu,mm nilidhani ameondoa mgao kwa kiki za CCM.
 
Back
Top Bottom